Biashara ya nafaka ina umafia mwingi. Kwa wanaotarajia kuanza kuuza nafaka chukueni tahadhari

Uko sahihi. Kuitwa mfanyabishara ni uzoefu siyo kuwa na fedha za kununulia mali. Infact kwenye biashara uzoefu ni kitu kigumu kupata kuliko mtaji.
Yes,thus why wastaafu wengi huwa wanafungua biashara kwa kutumia hela za mkupuo walizopata kisha wanafirisika kwa haraka sana na hawajui pesa imeenda wapi
 
Changamoto ni sehemu ya maisha ya mfanya biashara unatakiwa ubuni mbinu zitakazo wezesha kukabiliana na changamoto
 
Biashara ya mahindi ni nzuri sana kama ukiuzia nje ya nchi,mfano kenya au sudan kusini, ikiwa uko mikoa ya arusha au manyara ni bora zaidi, ila sasa! Ni hadi uunge chain na wafanyabiashara wazoefu,wakubali kukupa ushirikiano na kukupa hints kadha wa kadha,otherwise hawa ndiyo ma mafia wenyewe,nipo kwenye circle ya biashara hiyo,ila kwa angle tofauti,kuna jamaa alijiingiza kibabe kwenye game bila kusajiliwa kwenye chama cha wafanyabiashara ya nafaka huko arusha, kilichomkuta alijuta, mzigo wa tani 30 ulizuiliwa mpakani namanga,akaambiwa yana aflatoxin,marufuku kuingia kenya, alipambana kuhonga na nini lakini hakufanikiwa kuuingiza,, ipo hivi=mfanyabiashara wa mazao anayeuzia kenya anapaswa kuwa na namba za askari wa barrier zote kutokea arusha mpaka sokoni kenya,na pale border vilevile, kwa hiyo mzigo ukifika kabla haujafika barrier askari wanajua mzigo wa fulani unakuja,border vilevile,na wanakuwa kwenye payrol yako,unakuwa unawatoa kwa chochote kitu, sasa kama hujulikani wale wazoefu wakijua unapeleka mzigo, simu zinapigwa kote, zuieni huo mzigo! Baba hupiti!! Ukivuka barriers zote safari yako inaishia namanga, utatoboka hela hadi mzigo unakupiga hasara takatifu, pale border mwishoni watakuja wafanyabiashara wazoefu, wakukatishe tamaa kabisa, kisha wakuambie uwauzie wao kwa bei ya hasara, ukikubali(probably utakubali tu) wao wanayanunua, na kuyavusha kiulaini kabisa,unarudi home na hasara yako.
 
Bora anayenunua mahindi kuliko mpunga aise
Bora anayenunua mpunga kuliko Mahindi.

Mpunga huwa haushuki bei kupita kiasi lakini pia hauharibiki haraka kuliko mahindi.

Ipo mikoa mingi ambayo haizalishi mpunga ila mahindi yanalimwa kila mahali.

Mpunga unaweza kuutunza stoo hata miaka mitano ila mahindi siyo rahisi.
 
Inaelimish lakini pia inakata tamaa kwetu tunaotaka kuuza mazai nje ya nchi,

Vp kwa mtu anaetaka kuuza matunda ya mapasheni, anakutana na hii adha ?
 
Hiyo tunaita mjasiriamali na yanayomzinguka maanake kumbe kabla hujafanya biashara unatakiwa uwe na mpango wa biashara ambao yote hayo yanakuwa sehemu ya mpango wako wa biashara, Mimi nimebobea kwenye elimu ya ujasiriamali
 
Hata biashara ya wanyama ni mbaya. Niliwahi kununua Ng'ombe Mia kutoka Mbeya kwa ajili ya kuja kuuza Dar.

Kufika Iringa nikakuta Ng'ombe wote wamekonda.

Sijui wale wahuni waliwapiga sindano wale.

Kufikika Kibaha nilikokuwa napaki 21 wakafa.
ahahaa hiyo kali uliuziwa vipulizio nin
 
Wabongo ni Kenge sana
 
Hata biashara ya wanyama ni mbaya. Niliwahi kununua Ng'ombe Mia kutoka Mbeya kwa ajili ya kuja kuuza Dar.

Kufika Iringa nikakuta Ng'ombe wote wamekonda.

Sijui wale wahuni waliwapiga sindano wale.

Kufikika Kibaha nilikokuwa napaki 21 wakafa.
Hiii ndio bongo. Halafu mtu unaumiza kchwa ufanye biashara gan, kwa staili. Hii unafanya biashara za nini, bora kuweka UTT tu au fixed deposit
 
Niliwahi kufanya biashara ya mafuta ya alizeti..

Wahuni wakanichanganyishia na maji kwenye madumu ya njano.

Nafikisha sokoni juu mafuta chini maji.. dadeki nilijifunza kitu! Umakini na kufanya kazi kwa watu makini
Dah inasikitisha na kuchekesha at the same time.
Yaani wabongo kila mahali wanabuni mbinu ya kuchakachua
 
Yeah hili ni la muhimu sana kama unataka biashara ya uhalali
Mimi ni muelimishaji ujasiriamali naandika pia kitabu cha ujasiriamali ambacho nadhani ni fikirishi kinajaribu kutafakari kwanini biashara zinakufa na suluhu inayowezekana kwakifupi kinamuelimisha msomaji kujenga biashara ya kudumu kuna mambo mengi hayako sawa kwenye jamii ya waafrika kuhusu ujasiriamali na biashara hasa jinsi ya kukabiliana na tusiyoyatarajia ktk maishani na biashara
 
Mkuu iko hivi,ujasiriamali au kufanya biashara ni tabia ya mtu,yaani ili uwe mfanya biashara mzuri inatakiwa biashara iwe ni tabia yako ya kila siku na miaka yote.
Sasa kinachotucost waafrika hasa hasa Tanzania huwa tunadhani wakati sahihi wa kufanya biashara ni baada ya kuachishwa kazi,kukosa ajira,kupata pesa ya ghafla kwa mkupuo hili ndilo kosa kubwa tunalofanya.
Biashara inataka miaka mingi ya kujifunza kujua gaps zinatokea vipi,faida inatokea vipi hasara inatokea vipi,kisha kazi yako inakuwa ni kurekebisha hizo weaknesses polepole hadi unafikia kile kiwango unachohitaji(hiki ni kipindi ambacho hata ukilala nyumbani ukamuachia mtu hawezi kukuibia,unajua mauzo ya siku hata kabla hujafungua ofisi)
 
Nikweli kuhusu sifa za mjasuriamali km huna hata sifa Moja huwezi kufanya biashara lakini tatizo la biashara nyingi kufa nikwasababu jamii imeshindwa kubuni mbinu za kukabiliana na yasiyoyatarajiwa
 
Nikweli kuhusu sifa za mjasuriamali km huna hata sifa Moja huwezi kufanya biashara lakini tatizo la biashara nyingi kufa nikwasababu jamii imeshindwa kubuni mbinu za kukabiliana na yasiyoyatarajiwa
Ndio tunarudi palepale sababu kuu ni ukosefu wa zoefu,mfanyabiashara mzoefu huwa anajua mbinu za kukabiliana na jambo lolote litakalotokea.
Unless otherwise labda hilo janga liwe limetokea dunia nzima kama ilivyotokea Covid hapo sawa atachemka.
 
Ndio tunarudi palepale sababu kuu ni ukosefu wa zoefu,mfanyabiashara mzoefu huwa anajua mbinu za kukabiliana na jambo lolote litakalotokea.
Unless otherwise labda hilo janga liwe limetokea dunia nzima kama ilivyotokea Covid hapo sawa atachemka.
Binadamu ndiye msababishi mkuu wa yasiyoyatarajiwa katika biashara
 
Pole sana lakini siku nyingine tumia😜👈.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…