Biashara ya nafaka ina umafia mwingi. Kwa wanaotarajia kuanza kuuza nafaka chukueni tahadhari

Niliwahi kufanya biashara ya mafuta ya alizeti..

Wahuni wakanichanganyishia na maji kwenye madumu ya njano.

Nafikisha sokoni juu mafuta chini maji.. dadeki nilijifunza kitu! Umakini na kufanya kazi kwa watu makini
Aisee , hizi roho za kishetani wabongo sijui huwa tunazitolea wapi
Mbongo ni mwizi na mharibifu sana ,sasa imagine Kenge aliyefanya hivyo na short aliyokupigisha , yaani jitu halioni aibu wala huruma
 
Aisee umeandika kitu kizito ,mwaka juzi nilikuwa nataka kuanza hii biashara
Vipi ,bado unapeleka nafaka kenya ?
 
Soko la mahindi kenya ni kubwa sana hasa Mombasa na Nairobi ,
Vipi kwa sasa Mzigo wa mahindi bado unaenda mombasa ?
 
Hapa ndipo waKenya wanapotupiga bao
 
Hongera sana ndugu muelimishaji, uwepo wako ni muhimu sana.

Vipi kwa sasa hivi unafanya biashara gani Mkuu?
 
Hongera sana ndugu muelimishaji, uwepo wako ni muhimu sana.

Vipi kwa sasa hivi unafanya biashara gani Mkuu?
Nauza akili, (selling services), ni fundi wa vifaa vya kielecktroniki ,(general electronics repair), simu software and hardware, radio and tv repair, labda niseme chochote kinachopita mbele yangu km akili yangu ikiamua kuamsha ubongo wangu nitaweza
 
😂😂😂
 
Maisha ni Biashara Usipofanya biashara utafanywa ww Biashara uamuzi ni wsko uwe upande gani wa mfanya Biashara au mfanywa Biashara na kila upande una changamoto zake kubwa tena na hakuna upande ulio Salama kote ni Shida.

Nilichokigundua ww jamaa ni mkata tamaa mapema sana changamoto kidogo tu tayar ushazira na umekuwa mshauri nasaha hivi unafikiri biashara ni rahisi et. Mfanyabiashara inatakiwa uwe na roho ya kikomandoo usiwe lele mama life ni gumu sana chaliii yangu.

Ww ulitaka uchukue mpunga uwe mzuri upige hela au uchukue mchele uwe safi upige hela life lisingekuwa gumu jombaa pambana na roho ngumu, uwe mnyama.

Mimi nafanya izo biashara za nafaka nachukua mchele na Asali Tabora tena nachukulia mjini wala sijawahi kuenda shambani napeleka Dar na Zenj na mambo yanakwenda kiubishi ubishi na wala mm sio mzoefu kivile kwa industry.

Kuwa mjanja, jichanganye, jua namna ya kutengeneza chawa ili akupe habari , madalali hawaepukiki, be creative na uwe na initiative sio kulia lia hakikisha unapata codes sahihi na uwe too much inquisitive.

All in all biashara ya mchele ni nzuri na inalipa hasaa ujinga wako ndio hasara yako.

Na ukiendelea na Tabia ya kukata tamaa Mbinguni utapasikia tu
 
Niliwahi kufanya biashara ya mafuta ya alizeti..

Wahuni wakanichanganyishia na maji kwenye madumu ya njano.

Nafikisha sokoni juu mafuta chini maji.. dadeki nilijifunza kitu! Umakini na kufanya kazi kwa watu makini
Nahisi Kwenye Tano Bora ya utapeli TANZANIA tupo
 
Mkuu kubali hukuwa mwenyeji. Kuna jamaa nilikutana nae anahitaji kununua mchele mashineni kipindi hicho nilikuwa nakoboa gunia 4 zangu kisha niuze na akaniomba nimuuzie ....nilimwambia bado sijajua kama utatoka vziei unaweza kuvunjika japo hii ni mbegu nzuri.

Hivyo akasubiri hadi nikakoboa kupima kisha akanilipa ikabidi aulize kama niano mwinginge kule home na ninauza nikamwambia upo ila siuzi.Tukaenda mahali kupiga story yeye alikuwa mganda nilimshauri kitu kuwa kama anahitaji mchele quality kabisa aende kijijni anunue mpunga kwa wakulima kisha aanike then akoboe na kupaki hapo atapata faida nzuri na mchele utakuwa mzuri sana.

Jamaa akasema hana mwenyeji kwa sasa yule aliyemleta katika maeneo hayo alimtapeli kama nitakuwa na nia ya kumsaidia yupo tiyr kweli tuliingia kijijni yeye akapanga senta tuligawa hela kwa watu 5 tu maarufu na tukaongeza 5000 kwenye gunia la debe6 tofauti na wenzetu wao walikuwa chini ya hio bei hivyo ndani kama ya wiki tu magunia yapo ya kutosha kabisa na jamaa hakuamini.

Kwa kifupi jamaa alinipa mtaji wa m3 namimi nikaanza baishara hiyohiyo japo msimu ulikuwa umeisha nikawa na nunua kama wewe unalivyokuwa unanunua mashineni hapo ndo kunaumafia sasa wa kila aina sema mimi nilikuwa najua kila uhuni wao hadi wanacheka tu.

Ukiamua kufanya biashara hii fanya hivyo nenda kanunue mpunga kama sio mwenyeji tafuta mwenyeji utafaulu
 
Aisee , hizi roho za kishetani wabongo sijui huwa tunazitolea wapi
Mbongo ni mwizi na mharibifu sana ,sasa imagine Kenge aliyefanya hivyo na short aliyokupigisha , yaani jitu halioni aibu wala huruma
sio mbongo sema ngozi nyeusi
 
Aiseeee
Hata biashara ya wanyama ni mbaya. Niliwahi kununua Ng'ombe Mia kutoka Mbeya kwa ajili ya kuja kuuza Dar.

Kufika Iringa nikakuta Ng'ombe wote wamekonda.

Sijui wale wahuni waliwapiga sindano wale.

Kufikika Kibaha nilikokuwa napaki 21 wakafa.
ee
 
Ushawahi kufanya biashara ya Mbao wewe? Omba Mungu sana yasikukute😀😃😄😁

Vipi kuhusu Malimbichi? We dalali uliyenidhulumu Mahindi yangu ya Gobo niliyohangaika nayo miezi 4 huku Makete Mungu anakuona.
Biashara ya mbao inashida gani mkuu !?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…