Biashara ya Nafaka mtaji mkubwa faida kiduchu

Ni sahihi kuna msimu wa faida kubwa na msimu wa faida kidogo ata hivyo inatakiwa ustick mwaka mzima kwenye bashara pia uwe mtafiti mzuri wa masoko na machimbo ya kununus mzigo usilenge eneo moja tu hapo utafulu kwenye hii biashara


😁😁 ila mkuu nilivoona neno KUJUMUA nikajua lazima utakua pande hizo mbeya/songwe 😂 maana hili neno limewakaa na unalikuta mikoa hiyo tu😃
 
Ndi ghwa nkatefu kabisa 🤣
 
Mkuu vipi ukinunua mzigo ukausagavuuze unga, hapa faida yake vipi na kipi rahisi kupiga pesa
 
Hii biashara inataka uwe unachukua mzigo mkubwa sana kwa Mara1 .
 
Mkuu vipi ukinunua mzigo ukausagavuuze unga, hapa faida yake vipi na kipi rahisi kupiga pesa
Inawezekana pia, lakini kuna ushindani mkubwa sana , lazima uwe na mtaji wa kufanyia Promotion ya soko, sababu viwanda vya unga ni vingi sana, ukiwa na Mashine 1 tu umemaliza kila kitu!!


Fursa kubwa hapo ni wewe kuwauzia hao wenye viwanda, wanaosagisha , wanahitaji sana Nafaka .
 
50 ni kubwa sana kwenye biashara asikudanganye mtu
Acha 50 hata Tshs 5 ni kubwa kama kuna uhakika wa percent mia moja..., sasa issue ya ukipata sana faida ni 50/= na haichelewi siku nyingine kukata mtaji hio tena sio biashara bali kiwanda cha stress...
 
Acha 50 hata Tshs 5 ni kubwa kama kuna uhakika wa percent mia moja..., sasa issue ya ukipata sana faida ni 50/= na haichelewi siku nyingine kukata mtaji hio tena sio biashara bali kiwanda cha stress...
upo sahihi kikubwa kuongeza bidii
 
Mkuu vipi ukinunua mzigo ukausagavuuze unga, hapa faida yake vipi na kipi rahisi kupiga pesa
Ni vizuri, ila mwanzo si unajua mgumu ndugu.

Hapo kikubwa unatakiwa uwe na soko kubwa.

Lazima uwe na jina la kampuni yako.

Uwe na vifungashio vinavyo kutangaza.

Kuwa na mashine yako sio lazima, kwa7b ni mwanzo unaweza kuelewana na mwenye mashine anakuwa anakusagia unga we unaweka kwenye vifungashio vyako.

Unatakiwa uwe na ofisi yako(fremu) ila nayo sio lazima kama huna pesa ya fremu, unakuwa una hifadhi kwa mwenye mashine.

Pia unatakiwa uwe na mashine ya kushonea mifuko(lazima) ila nayo pia ina tegemea kama mwenye mashine ya kukoboa na kusaga anayo, utatumia hiyo hyo kwa makubaliano yenu.
Unatakiwa ununue mzani wako ule wa kukalisha mzigo (wa utosi) 200kg au 300kg.
Mifuko yako inatakiwa uweke ujazo huu…
2.5kg
5kg
10kg
25kg.

Kikubwa: Tafuta soko la uhakika kwanza la watu wa kuwauzia bidhaa yako…

Hoteli au migahawa.
Shule, bweni au chuo.
Maduka ya jumla.

Tafuta namna nzuri ya KUJITANGAZA…
Unaweza kutumia redio au ukaanzisha kombe la mpira wa miguu, kwa vijana wagombanie mbuzi, ng'ombe au pkpk nk.
Pia kwenye hilo kombe unaweka logo yako au unaliita kwa jina lako la biashara.

Nna uhakika ukitumia njia hizo unaweza kufika mbali kiuchumi.

Sijajua vibali huko TRA.

Changamoto nyingine utaziona na kuzitatua ukiwa kazini.

Kumbuka: kuna faida nyingine hapo huwezi kuziona kwa haraka haraka kama kuuza pumba za mahindi nk.
 
Nina milioni 5 nimeipata kwenye kazi zangu za umeme nilikuwa nawaza niingie kwenye biashara ya nafaka hasa maharage niyatafute vijijini huko niyalete mjini

Ila naona ninavunjika moyo na hizi comment za watu wengi.

Ngoja niendelee kufikiria biashara ya kufanya
 
Nina milioni 5 nimeipata kwenye kazi zangu za umeme.

Ngoja niendelee kufikiria biashara ya kufanya.
Fanya biashara ya mahindi kichele, nunua mashambani au vijijini huko kisha peleka mjini.

Kazi yako una nunua na kuuza jumla jumla.

Pia hii kazi unatakiwa uwe na mzani wako ili usipigwe kwenye kilo huko utakapofika kuuza.

Kikubwa uwe na watu wa uhakika wa kuwauzia mzigo huko MJINI.

Pia uwe na taarifa za uhakika kuhusu bei ili usipate hasara.
__________________________

Kama barabara nzuri na usafiri hausumbui na hata hao mabosi wako watakao nunua hayo mahindi yako huko mjini hawasumbui, utapiga BAO.

Hiyo biashara ni nzuri kama utakuwa hukai siku nyingi kukusanya na kupata mzigo huko vijijini.

Pia kuhusu bei ya kununua huko vijijini inatakiwa upange ww kama utaona bei ya mjini hailipi, maana mahindi yanatabia ya kupanda na kushuka BEI wakati wowote.

Nakutakia kila la kheri.
 
Nunua viwanja au kiwanja pembeni mwa Dar Es Salaam au nje kidogo ya Dar Es Salaam

Hela inayobaki kapande miti
 
It is almost 10%
Fikiria mtu aliyewekeza 300milion kwenye nyumba za kupangisha atapata only 1.0m per month.
Aliyewekeza 30m kwenye nyumba ya kupangisha ataingiza only 150k per month.
Tafauti ya hizi biashara mbili ni security ya mtaji na usimamizi wa biashara.




Chunya
 
Hela nyingi hiyo tafuta mzoefu akupe mbinu unatobo.
 
Asante sana mkuu
Umemaliza Kila kitu
 
Jikite kwenye fani yako fungua duka la vifaa vya umeme
 
Biashara ya nafaka usifanye kama huna mtaji, milioni 6 kafungue duka la nyakula vya nyumbani. Huko wanaanza na nilioni 100 kuendelea hapo utaona faida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…