Biashara ya ndege haiwezi kuleta faida kabla pay back period haijafika

Report ya Cag ina utata mwingi sana mfano kama hasara ni bil 60 mbona hajasema nani awajibishwe na hasara lkn bil 3 mtu kachukuliwa hatua iwe wazi kama msomi hapa kachemka sana
Yeye kazi yake ni kukagua na kutoa info wapi penye uozo, hilo swala la nani awajibishwe lipo nje ya majukumu yake.

Nyinyi mlijifanya mnaipa promo serikali ya magufuli kua ipo secured kiasi hakuna ufujaji wa pesa now the thruth has been revealed mnaanza kutafuta huruma
 
Kwaiyo kipind tunasubr ayo unayosema ,CAG aseme kuna faida au aseme bado kwanza au asikague ,nazan anasema anachokiona ukifika muda wa faida itaonekana pia atasema
 
CASE 1.
Ili faida iwe kubwa (au iwepo) ,ni Lazima Mapato(mauzo ya huduma na bidhaa) yazidi Matumizi,Tofauti ya Mapato na matumizi itakuwa Chanya (positive),tutasema tunajiendesha kwa faida.

CASE 2.
Kinyume chake,Matumizi(Gharama za uendeshaji n.k),zikizidi Mapato,Tofauti ya Mapato na Matumizi itakuwa hasi (negative).Kwa Muktadha huu tutasema Shirika linajiendesha kwa hasara

Case 2,hautawahi kufikia Payback period
 
Nimekuelewa mkuu ila huyu mleta mada naona anataka kutulisha viaz pori kulingana na report ya CAG shirika la ATCL achilia mbali kuzalisha faida lakini hata gharama za kujiendesha bado zinaghalamiwa na serikali atlest tungeambiwa kwamba shirika linajiendesha lenyewe lakin bado halijaanza kuzalisha faida correct me if am wrong!!!
 
Hiki ndio nacho kitafuta mkuu, sasa kama ni hivyo kumbe ndege hazina makosa, sasa hapo ndege zina makosa gani. Wenye makosa waendeshaji wa shirika, kuanzia mkurugenzi hao ndio wenye makosa.
 
Payback period inakuja baada ya prediction ya mapato kwa biashara/investment husika.
Mfano:
Umewekeza TSH 10,000/= then kwa mwaka biashara inakungizia TSH 5,000/=. Hapo payback period itakuwa baada ya 2 years.
After 2 years utaanza kuingiza faida kama kila kitu kitakuwa kama ulivyo panga.

HASARA KABLA YA PAYBACK PERIOD

Mfano:
Umewekeza TSH 10,000/= then kwa mwaka biashara inakungizia TSH 5,000/=. Hapo payback period itakuwa baada ya 2 years.

But....Kuna mda mambo yanaenda mrama, badala ya kuingiza Tsh 5,000/= unakuta unapata Tsh -6,000/= kwa mwaka kutokana na sababu mbalimbali hapo payback period ya 2 yrs inaweza ruka to 3,4,....n.

So, usishangae ATCL kutangaza hasara, sababu yaweza kuwa wanacho kipata kwa mwaka sio walicho kitarajia.
Unafika wakati hata pesa ya mafuta, salary wana omba serikali kuu. Hapo lazima watangaze hasara kwasababu matumizi yamezidi kipato.
 
Plz naomba link /pdf ya annual reports za ATCL.
 
Na kama utataka kutumia kanuni ya Pay back period kwa kuingiza mtaji wa zile ndege za Magufuli kuwa sehemu ya mtaji wa ATCL, kiuchumi huenda itachukua labda zaidi ya karne moja (zaidi ya miaka 100) ili wao kuanza kuhesabu faida. Projection ikiwa watakuwa na trend ya kupata at least 30bilion kwa mwaka kutoka kwenye biashara (Revenue-Operation cost).

It is too complicated for ATCL to run into profit.
 
Mkuu hiyo hasara ya 60B IPO kwenye operating cost maana take imejiendesha kwa hasara kwa mwaka mzima.

Kwa simple language ni kwamba hizo 6O B sio mapato yatokanayo na biashara Bali ni fedha zilizovhukuliwa kwenye mfuko wa Serikali zikapelekwe ATCL Ku cover matumzi ya shirika.

Kwa hali kama hiyo ni wazi shirika haliwezi hata kurudisha hela za kununulia ndege.

Kwa Tanzania issue sio kununua ndege kwa cash au kwa mkopo,issue kubwa ni vipato vya watu watu Milo 3 tu shida hiyo wa kulanda ndege watatoka wapi??

Nchi yeye shirika lolote la ndege customers wa kwanza wanatakiwa wawe wananchi wako na robot ndio wageni,sasa kwa Tanzania hii watu hela Hanna.
 
Wakati wanakujibu watutajie shirika gani la ndege hapa Africa lililoingiza faida katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita
 
Hayo maelezo aliyoyatoa ndio ambayo yalitakiwa sasa yaelezwe ili mtanzania aelewe, kwa mantiki hiyo tatizo halipo kwenye ndege tatizo lipo kwenye uongozi wa shirika, hapo ndio kwenye tatizo.
 
Ninachojua mtanzania mwanasiasa hawezi fanya biashara yoyote akapa faida labda awe anakwepa kodi. Halipi gharama za operating cost, tumeona hata kwenye benki. Hebu hilo shirika mpeni Charse Kimei mwone kama halitaingiza faida.
 
Wakati wanakujibu watutajie shirika gani la ndege hapa Africa lililoingiza faida katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita
Information is power na kama una informations zozote leta hapa tufanye sharing, for the information that i have Ethiopian airline bado ipo vizuri on sky achilia mbali mashirika mengine ambayo yapo hoi bin taabani kama kq, sa, rwandan air. Acha kutuaminisha kwamba mashirika yote yanafanya vibaya kiasi cha kuifikia ATCL stop joking!!!!!
 
Pay back period ndo nn?
Internal Rate of Return (IRR).
Unanunua kitu x kwa kiasi fulani unakitumia kuzalisha faida ya kiasi fulani ili baada ya muda y upate rejesho z lenye faida ama kwa kubakia na kitu hicho au uendelee upate faida.
Hesabu za namna hii zinajumuisha
1.gharama za uendeshaji
2.matengenezo
Hata hivyo kama matengenezo ni makubwa kuliko uzalishaji matokeo yake si mazuri katika return kwani yqnaongeza gharama za uendeshaji katika kulipa mishahara n.k
 
Plz naomba link /pdf ya annual report ya ATCL.
Kwa mujibubwa CAG leo...ile ripoti ni mpaka ipelekwe bungeni kuwa tabled ndipo inakuwa public document.

Nadhani bado haijafikishwa kwenye kikao cha bunge ili iwe released to the general public.
 
Tatizo la wasomo wa kitanzania ni ujinga wa kutokuja na solution katika kila tatizo wanaloligundua.

Kama kwa miaka mitano yote ATCL imekuwa ikipata hasara ni kupitia maeneo gani hasara hiyo imetokea?

Au pia ni hatua zipio zilichukuliwa na ACG kushauri njia za kuepuka hasara hizo na ni nini matokeo ya njia hizo kutumika?

ATCL huko nyuma imekuwa ikiingiza hasara ya mpaka bilioni 200 tofauti na hii bilioni 60 ya sasa ambayo inaonyesha kwamba kuna dalili za madeni kupungua.

Mashirika mengi ya ndege ikiwemo ATCL pia hutakiwa kulipa ada ya maegesho na ile landing fees na naamini bado ATCL inadaiwa na viwanja vya ndege kama Heathrow.

Je, katika taarifa zake ACG amewahi kuzungumzia hizi tozo za viwanja vya kimataifa na kwamba hadi sasa serikali inaendelea kulipa madeni hayo na ni kiasi gani gani sasa?

Tufike wakati sisi watanzania tuwe tunatumia akili zetu kupambanua masuala kama haya ambayo hayahitaji kutumia nguvu nyingi.
 
Hapo umemaliza kila kitu.
Hichi ndicho ambacho CAG alikuwa akikimaanisha. ATCL bado haijaweza kufikia kujiendesha kwa faida kwa kipindi chote cha miaka mitano mfululizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…