Biashara ya nguo, viatu, mikoba na cosmetics kutoka Uganda

mambo vp mkuu kama umenipa mwanga upo hewani kwa no gani nicheki pm tuweze kushea mawili matatu biashara ya uganda
 
wise boy nakuomba pm ndugu yang nahitaji msaada wako kuhusu hii ishu maana next weak nitakuwa na trip uganda so nahitaji muongozo wa kina
 
Habari za usiku huu mabibi na mabwana..
Mimi ni miongoni ya waliokosa ajira mpaka sasa, kutokana na hali hiyo nimejidunduliza na kupata M1. Kipindi nasoma chuo nilikua nafanya biashara ndogondogo nikiwa naishi hapo hapo hostel. Pia nilikua nazunguka hostel nyingine kike mbalimbali jijini Dsm nyakati za jioni, kuwauzia nguo za mitumba,nguo za ndani na chochote kile atakachoniagiza mteja naenda kujumua namletea kama pafyumu, belt au saa.
Naomba nisiwachoshe sana nina mtaji wa Milion 1 tu nataka niende Uganda kununua vitu kule nije kuuza huku kwetu. Nimejaribu kupitia uzi mbalimbali za miaka ya nyuma za biashara hiyo, nimepata mawili matatu.
Sasa kutokana na miaka kwenda naombeni maoni au ushauri kwa watu wanaofanya biashara hii hivi sasa.
Asanteni
 
Hiyo pesa ni ndogo kusafiri mpaka Uganda kuchukua mzigo, utajikuta umekata tsh 200000 kwa ajili ya usafiri tu, kwanini usianze kwanza kuchukua mzigo hapo ulipo kabla ya kuanza kwenda nje, wenye biashara hiyo faida yao kwa robota 1 huwa ni 50,000/= tu, lakini pia fikria mitumba ya Kenya maana wao huchukua Kenya na hawachakachui kabisa na mitumba yao ni kutoka China na Korea ambao miili tunaendana.
 
Lakini pia kulingana na hali mbaya ya uchumi watu hawanunui nguo sana, fanya kuuza chakula kwa pesa uliyo nayo unaweza kununua gunia kadhaa za maharage au mchele, nenda kwenye maduka ya reja reja, mamantilie ukichukua order, sambaza mzigo wako nina uhakika kwa siku utauza maharage au mchele gunia kadhaa na faida utaiona, kila siku watu wanakula ila hawavai nguo mpya.
 
Hiyo pesa ni mtaji tu wa kununulia mzigo pesa ya nauli na hotel nimetenga lak 3 pembeni, pia nataka nichukue nguo za duka sio mtumba tena na nguo za ndani pichu na sidiria.
 
Nina uzoefu wa hii biashara na wateja wangu wakuu ni wanafunzi wa vyuon nadhani unajua wanafunzi jinsi walivyo, wanapenda kwenda na wakat.
 
Hiyo pesa ni mtaji tu wa kununulia mzigo pesa ya nauli na hotel nimetenga lak 3 pembeni, pia nataka nichukue nguo za duka sio mtumba tena na nguo za ndani pichu na sidiria.
Si uchukue hizo nguo kariakoo ?
 
Si uchukue hizo nguo kariakoo ?
Ni bei sanaaa gauni ndefu nzuri bei ya jumla ni elf 22 had 25...jinsi kali 15 had 18. Chupi nzuri za cotton ni elf 36. Kwa uchunguzi mdogo niliofanya k.koo vitu ni bei sana kuliko ug.
 
Ni bei sanaaa gauni ndefu nzuri bei ya jumla ni elf 22 had 25...jinsi kali 15 had 18. Chupi nzuri za cotton ni elf 36. Kwa uchunguzi mdogo niliofanya k.koo vitu ni bei sana kuliko ug.
Hujaingia machimbo

Kariakoo kuna maduka ya jumla na rejareja unahitaji uchambuzi yakinifu siyo mdogo.

Kwa mfano chupi kuna maduka wanauza kuanzia dozeni kumi kwa 90,000
Hapo hapo kuna anayechukua kwa huyo wa jumla na anauza kwa hiyo 36000
 
Ni chimbo gani unalosema sijaingia hilo..? Nimezunguka k.koo nzima. Na hyo bei chupi ni zile chupi za kawaida sana hakuna mtu anayeuza chupi za cotton kwa elf 9 hakuna.
 
Ni chimbo gani unalosema sijaingia hilo..? Nimezunguka k.koo nzima. Na hyo bei chupi ni zile chupi za kawaida sana hakuna mtu anayeuza chupi za cotton kwa elf 9 hakuna.
Ok all the best.
 
Wazo zuri, Uganda ni cheaper sana nguo
Ni kweli dada, kama kuna jambo lolote unalifahamu au hata maeneo ya kupatikana mzigo kwa bei nafuu zaid huko Ug naomba uniambie mkuu.
 
Hebu angalia jinsi ya kuchukua Mchuzi wa Zabibu au Mvinyo kuupeleka Uganda na kule ukachukua nguo kuleta Tz.
Asante sana mkuu naomba unielekeze jinsi ya kufanya hiyo biashara.
 
Hebu angalia jinsi ya kuchukua Mchuzi wa Zabibu au Mvinyo kuupeleka Uganda na kule ukachukua nguo kuleta Tz.
Tufungue mamcho kwa mapana juu ya hili mkuu.

Umeandika kwa kifupi sana, huenda ukamsadia sana mleta uzi, lakini hata sisi pia...
 
Asante sana mkuu naomba unielekeze jinsi ya kufanya hiyo biashara.
Kwa ujumla unakwenda kwenye viwanda vinavyochakata zabibu ambavyo vipo Dodoma (Hombolo, Bihawana, au Mpunguzi) utakuta wahusika na watakufamisha meeengi yanayohusu Zabibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…