Biashara ya nguo, viatu, mikoba na cosmetics kutoka Uganda

mkuu money stunna na wadau wengine je hizo nguo special zinazopatikana huko ni latest kwamba ziko kweny fashion ya kisasa kwa mfano tshirt.,jeans
 

Habari? Unaweza kuni pm manake nilishakusanya mtaji wangu,nataka kwenda kuchukua viatu

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
ngojea ntafute karamu nakaratasi niupeluz uzi vizur

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
ngojea ntafute karamu nakaratasi niupeluz uzi vizur

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Yan Baraka kwa hapa nilipo kwa mujibu wa hii thread nasisimka tuu naona kila kitu sasa nahisi harufu ya utajiri. Yan kwa mchango wa money stunna nashukur sana katufungua kichwa money stunna una mchango mkubwa juu ya kila mtu hapa mana kila nipitapo nkikukuta nakuta umeshusha nondo za ukwel. Daah Jf kweli kisima cha maarifa ngoja nianze kuandaa michakato ya safari sasa mbarikiwe kwa michango yenu yote.
 
Wakuu me nataka kufanya biashara ya nguo but mtaji Wang ni 2m msaada tafadhali
 
Inatosha kabisa. Ukianza anza na zile zinazo uzika sana kwenye soko

Mtaji ninao,knowledge nimepata, vipi kuhusu soko nitalipataje na mie sina fremu?? ...Nipe idea ndio nataka nianze hii biashara sina uelewa wa soko.
 
Yoyote mwenye uelewa wa masoko ya hii biashara ya mavazi tujulishane..
 
Umetoa maelezo mazur sana kwa maana hiyo ukiwa na mtaji wa m5 unaweza pata mzigo mkubwa na mzuri me napenda sana biashara aisee asante sana kwa maelekezo yako..
Dada yangu hebu nisaidie. Je,mtaji wa sh milioni 2 za TZ naweza kuanza?
 
mkuu stunna nakukubali na tusaidie kidogo kuhusu mambo kadhaa.
1: Je utaratibu upi unatumika wakati wa ununuzi? namaanisha wauzaji kule uganda wauza kwa robota au mtu unaweza chagua kidogokidogo haswa ukizingatia mitaji yetu midogo?
2: Je ukitokea moshi arusha nairob then uganda kunaweza usafiri huu umekaaje,? Namaanisha itachukua siku ngapi kufika uganda na njia hii inaweza kuwa na changamoto gani?
3: Je kama nafuata taratibu,itanilazimu kuwa na nini au kufanya nini mpaka mmzigo wangu ufike moshi?
4; Kwa ujumla kuna changamoto gani zingine za hii biashara maana wengine tunahamu na ndoto za kuifanya ila hatujawahi hata kuuza vocha,so tusaidie kujua lolote lingine kwenye hii biashara hasa changamoto za namna ya kununua na kusafirisha mizigo.
Hasante sana mkuu
 

jibu kwa swali la kwanza.Yote yanawezekana ukitaka kununua moja moja au kwa robota,ni utashi wako tu.

jibu la pili,bus zinazoenda kampala kupitia moshi na arusha zinafika moshi kama saa 9 na arusha kama saa 10 jioni kama hazikuchelewa njiani,na nairobi mnafika kuanzia saa 3 usiku kisha mnaanza tena safari saa 4 usiku na bus ilo ilo.Boda (mpakani) mnafika alfajili saa 12 pia kuna boda 2 moja ya Malaba kama mtakuwa mlipitia eldoret au Busia kama mlipitia Kisumu.

Kampala mnafika saa 3 asubuhi.

swali la 3 hakuna utaratibu wowote zaidi ya wewe kuwa na passport na nauli tu.

swali la 4,changamoto kubwa ni namna ya kufahamu wapi ununue mzigo na lazima uombe kupunguziwa bei ata kama utaona bei ndogo.pia kuhusu kusafirisha utaongea na konda kila kitu kitaenda poa.

Cha muhimu ukienda uko nenda kwa kazi uliyoendea kamwe usiingie kwenye starehe
 
Mtaji ninao,knowledge nimepata, vipi kuhusu soko nitalipataje na mie sina fremu?? ...Nipe idea ndio nataka nianze hii biashara sina uelewa wa soko.

Mkuu kwanza ungesema uko wapi na mazingira gani kwa maana ya mjini au nje ya mji.

Unaweza ukaenda kununua mzigo kisha ukawa unatembeza maofisini, make watu wa maofisini wengi huwa hawazunguki madukani kutokana na kutokuwa na nafasi.

Kuna changamoto ya watu kukopa hivyo basi uwe na uhakika na watu unaowauzia, kwa mwanzoni uza kwa cash ama mkopo kwa watu wachache unaowaamini.

Vile vile watu wanaokuzunguka ndio wateja wako!
 

Good Idea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…