Biashara ya nguo, viatu, mikoba na cosmetics kutoka Uganda

Biashara ya nguo, viatu, mikoba na cosmetics kutoka Uganda

Nairobi kama vya mtumba kama special nenda Kariakoo au Uganda.
Uganda tuseme simpo moja utanunua elfu 75 ya uganda bei ya jumla sawa na 5000 ya TZ. Ambapo vinauzwa sio chini ya
12,000 hadi 15,000 hapa nchini. Ukichukua mzigo mkubwa utapata faida

Unaweza ukatumia Saibaba au Mordern coach kusafilisha mzigo wako kwa bei poua
Nauli 130,000/= kwenda na kurudi. Weka hapo kula kulala. Kuna sehemu panaitwa MUKWANO MALL ndo kariakoo ya Uganda

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante sana kwamaelezo mazuri mkuu. Umetufungua macho wengi. Na km in Nguo za special Kwa kariakoo ni upande gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
....ila naomba kuuliza wadau, hivi kafremu ka biashara ya mitumba as mitumba inakatiwa leseni ya biashara TRA, coz kuna watu wanasema kibanda cha mitumba hakikatiwi wengne wanadai kibanda cha mitumba kinakatiwa leseni, ukwel upo wap? Msaada plz mwenye uelewa juu ya hili.
Ndio unakaiwa uwe na leseni ya biashara hiyo.Kama unafanya kwenye jiji au manispaa(URBAN) kwa mwaka sh 50,000.kama upo ktk Halmashauri za kawaida(RURAL DISTRICTS) ni chini ya 50,000/= TRA utalipia kutokana na mauzo yako.
 
Mamboz!
Siku za nyuma nilipost kama nataka kuanzisha biashara ya lipsticks, naomba ushauri kwa sasa nipo tayari na Mungu akipenda mwanzo wa mwezi wa 10 nitaanza rasmi business......napenda kujua kwa wenye uwezo kama hii biashara itafaa kwa kipindi hiki
Nawasilisha
 
Angalia soko lako mkuu.

Unalenga kuwauzia kina nani, unauza jumla au rejareja au vyote kwa pamoja.

Dar au mpaka mikoani na nchi jirani.

Inategemea bei yako mkuu je ni vunja bei au...?.

Tuanze na hayo kwanza.
 
Angalia soko lako mkuu.

Unalenga kuwauzia kina nani, unauza jumla au rejareja au vyote kwa pamoja.

Dar au mpaka mikoani na nchi jirani.

Inategemea bei yako mkuu je ni vunja bei au...?.

Tuanze na hayo kwanza.
Nataka kuanza kuintroduce kwa marafiki zangu na kwenye whatsapp groups then nitajitangaza rasmi instagram

Nitaangalia na uhitaji wa watu but kwa kuanza nitaanza kuuza rejareja hapo baadae ndo nitauza kwa jumla

Nitaanza na dar coz ndo ninapoishi ila Mungu akisaidia nitapeleka mpaka mikoani

Price itakuwa affordable wala sitaweka bei kubwa
 
upload_2017-9-17_13-12-14.png
upload_2017-9-17_13-12-14.png
 
Nataka kuanza kuintroduce kwa marafiki zangu na kwenye whatsapp groups then nitajitangaza rasmi instagram

Ooh okay, kama ni hivyo pia si mbaya coz uta-minimize baadhi ya costs zisizo na ulazima.

Nitaangalia na uhitaji wa watu but kwa kuanza nitaanza kuuza rejareja hapo baadae ndo nitauza kwa jumla

Yah, coz wanasema usipime kina cha maji kwa miguu miwili, Anza kwanza kiasi, wateja wakiwa wengi utaongeza zaidi.

Nitaanza na dar coz ndo ninapoishi ila Mungu akisaidia nitapeleka mpaka mikoani

Ni kweli MUNGU akisaidia, ila japo upo Dar ila naamini mpaka mikoani utatuma mzigo na tafuta wateja mpaka mikoani coz bei ya perfume kwa Dar sio sawa na mkoani mamii.

Price itakuwa affordable wala sitaweka bei kubwa

Safi.
 
Ooh okay, kama ni hivyo pia si mbaya coz uta-minimize baadhi ya costs zisizo na ulazima.
Yah costs zitapungua

Yah, coz wanasema usipime kina cha maji kwa miguu miwili, Anza kwanza kiasi, wateja wakiwa wengi utaongeza zaidi.
Kweli kabisa ni muhimu kuanza na kidogo kwanza

Ni kweli MUNGU akisaidia, ila japo upo Dar ila naamini mpaka mikoani utatuma mzigo na tafuta wateja mpaka mikoani coz bei ya perfume kwa Dar sio sawa na mkoani mamii.
Ni lipsticks.....unachosema ni ukweli nitafanyia kazi ushauri wako
 
Uganda nguo ni bei nafuu sana kwa sababu nchi za America,Asia na Europe zimefanya uganda kama sehemu ya kupeleke nguo ,begi,viatu etc kutokana na kuwa hawana urasimu wa biashara na kodi ni kidogo sana.Tanzania kuna urasimu na kukandamiza sana wafanyabashara kwa njia za kodi.kule wanasapoti wafanyabiashara kwa vitendo.

Pia soko ni kubwa kuna watu toka tanzania,Kenya ,rwanda,Congo,Burundi,Eritrea,Ethiopia,China,India etc na hakuna sheria kali za uhamiaji kama tanzania kwa ufupi kule hakuna kufatiliana utaifa ni free kabisa.Twende kwenye maswali yako sasa,

Sehemu ambazo unaweza nunua mzigo ni city centre lakin mitaa ya Ben Kiwanuka,Tax park,Copper complex,Arua park na Owino market na sehemu jiran na Owino market.
Kwa vile unataka mitumba ingia Owino Market uko vitu ni bei rahis sana ila inahitaji ubageini na ni lazima ubageini,viatu ( TimberLand )ambavyo nanunua Tanzania 90,000 tzsh kule nanunua kwa 15,000-18,000 tzsh ila wanakuanzia mbali unaomba upunguziwe.
Uko Owino wafanyabiashara wanajua kiswahili vizuri ila ukiambiwa bei,wewe sema ambayo ni kidogo sana kutegemea na mzigo pia wakat unanunua ndio wakat mzuri wa kujua pia utauza kiasi gani.
Tshirt ya 15,000 tzsh pale unapata kwa 1,500 tzsh tena hiyo bei rejareja kwa wewe ukinunua kwa uwingi bei ni rahis sana.Uganda imefanywa kama dampo la bidhaa hizo na watu wa ulaya,asia na america.

Sehemu ya kulala maeneo ya copper complex kuna guest nzuri moja inaitwa Galaxy Guest house ni nzuri sana,bei zake ni ndogo sana kutegemea na unachukua room gani bei uanzia 15,000 ugsh hadi 30,000 Ugsh ndio bei ya juu kabisa.
room zipo ghorofan chini ni mgahawa,pia ukikuta imejaa jiran na hapo kuna nyingine Boston guest house ni nzuri pia na ata wafanyakaz wa hapo uongea kiswahili .bei zake ni ndogo.na hizo sehemu ni jiran na shoprite pia kutoka hapo hadi owino ni dakika 2 tu kutembea na hizo sehemu ndio kwenye maduka mbalimbali.

Kuhusu kodi,kuna mbinu inafanyika nitaku pm si vizuri nikieleza hapa.Kuna njia mbili za kwenda uko kuna njia ya kupitia Nairobi hadi Kampala na kuna jia ya kati hadi Bukoba kisha unapanda bus za Friends huondoka saa moja asubuh kutoka bukoba kwenda kampala,na saa sita na nusu uko kampala,ukifika hapo chukua bodaboda hadi Galaxy Guest house au Boston zipo maeneo ya copper complex jiran na shoprite ambapo kwa bodaboda haizid 2000 ugsh.

Pia ata maeneo ya Arua park kuna guest za kulala pia. ( hayo maeneo ni kama unavyoona kariakoo majina ninayotaja ni kama mitaa tu mfano msimbazi etc hizo sehemu ziko jiran jirani )

Rate za ubadilisha pesa ni 1.5 hadi 1.6
yani 1,000 Tzsh ni 1550-1600 Ugsh.
wakat ambapo shule zinafunguliwa rate inashuka sababu wanafunz wengi wa kitanzania wanakuja na pesa na wanachange inaweza pungua hadi 1.5 au 1.55.

kuna bus kama Falcon utoka dar kupitia njia ya kati hadi bukoba kisha kampala.
njia ya nai mfano kuna spider utokea dar-nairob-kampala.

ni wewe sasa kuamua,nawajua watu wengi wanawake/wanaume wamefanikiwa sana kimaisha kupitia biashara hii.cha muhimu ukinunua kitu uombe sana kupunguziwa pia usiingiwe tamaa za kununua vitu ambavyo hukupanga kuna vitu vizuri sana kule na cha muhimu kuwa makini ili usiibiwe pesa,uporaji kule hakuna labda mtu achane pochi yake bila wewe kujua.

mkiwa na swali ulizeni
Mkuu,,kwa taarifa nilizonazo ni kuwa mitumba kutoka Kenya ndio iko bomba sana coz ile grade 1 haijachakachuliwa,hukuti matambala yaani yote iko very smart. Kiukweli nipo ktk process za kwenda kenya kufungasha mzigo nilete Tanzania hebu nitosheleze na hili,nikweli mitumba ya kenya ina ubora kuishinda ya Uganda?
 
Back
Top Bottom