Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Wadau za Leo,

Nataka kufanya biashara ya kuuza nguo za mitumba za aina mbili kama nilivosema hapo juu za watoto na wanawake.

Lakini sina uzoefu kabisa na biashara hii na wala sjui lolote..sema nimeona ndo biashara ninayoweza kuianza na kuimudu.

Mtaji nilionao ni milioni moja na biashara nataka nifanyie maeneo ya Kibaha maili moja au Kibaha kwa Mathias. Kibaha picha ya ndege au eneo lolote karibu na hapo ntakapopata eneo zuri na lenye uelekeo wa biashara hyo?

Sasa naomba walio na uzoefu wanijuze kipi bora. Nianze kwa kununua balo au nianze kwa kununua moja moja minadani?
Kama ni kununua balo ni wapi ntapata mabalo yaliyo mazuri na bei zake zikoje?

Na kama ni kununua moja moja ni mnada upi uko vzri ili nipate faida?
 
Wanataka wafaidike wao tu wabongo kwa nongwa
 
Mkuu,

Mimi pia nitaanza biashara hii wiki ijayo hapa dar es salaam,japokuwa sina uzoefu wowote kuhusu biashara hii isipokuwa imekuwa kichwani muda mrefu na ninaipenda toka moyoni na pia kabla ya kuamua nilipata ABC kuihusu.

Nilipitia maandiko ya wajasiliamali mitandaoni na pia wadau wengine wenye uzoefu wa biashara hii na hata kuomba ushauri kwa wafanyabiashara wenyewe wanaofanya biashara hii pale Kariakoo na kwingineko.

Wengi wanasema biashara ya mitumba kwa ujumla inalipa sana isipokuwa inahitaji umakini katika manunuzi ya mzigo ili utengeneze faida.

Kwa maoni yao wanasema;
~Ukiwa ndo unaanza kufanya biashara hii ni mara mia ukanunue mzigo pale Ilala sokoni has a kwenye ule mnada unaoanza saa 4 aksubuhi kuliko kununua balo kwani wafanyabiashara wa Kariakoo wengi si waaminifu wanaweza kukuuzia balo lenye malonya mengi na hivyo kwa vyovyote mzigo utakukata na kukusababishia hasara.

Wanashauri kwa mfanyabiashara anayeanza ni vema apate uzoefu wa kutosha na connection ya uhakika kabla ya kuamua kwenda kununua balo la nguo pale.

Nyongeza ya hilo,kwa kuwa huna uzoefu wa kutosha,wafanyabiashara wa kariakoo ni rahisi kukuibia kwa kutojua tu grades za mabalo amboyo kimsingi yanatofautiana quality na bei.

Mfano;kuna mabalo yanauzwa kuanzia 150,000-600,000 kwahiyo unaweza hitaji balo let's say la (laki 4) na wao wakakupatia la (laki 1.5),kwa vyovyote hapo itakuwa ngumu kwa wewe kugundua kama umetapeliwa hadi utakapoiona hasara.

Binafsi nakushauri kanunue mzigo wako pale Ilala sokoni,achana na habari za balo katika hatua hizi za awali otherwise uwe na mtu wa kuaminika kwelikweli pale Kariakoo ambaye atakusaidia upate mzigo unaoutarajia japo ni ngumu kidogo ila inawezekana.

Aksante.
 
Wakuu bei za Mitumba nguo za watoto Balo moja inarange kuanzia sh ngapi hadi ngapi? Pia naomba kujulishwa bei ya jumla ya nywele za kinadada Rasta zinauzwajekwa bei ya Jumla Kariakoo?
 
 
 
Balo inategemeana kuna laki 3 na kuendelea.
 
Habari ndugu,

Nilikuwa naomba msaada wa taarifa juu ya upatikanaji wa nguo za mitumba za jumla (bale). Naomba kujua mabeli yanapatikana wapi na bei zake zipoje? Nipo interested zaidi na makoti ya suti za kiume na kike pamoja na mapazia.

Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…