charty
JF-Expert Member
- Oct 28, 2013
- 7,460
- 5,992
Jaribu kusearch humu ndani kuna nyuzi nyingi tu hiyo biashara ya mitumba imeelezewa.Mmh ina maana hakuna wataalam wa hii kitu humu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jaribu kusearch humu ndani kuna nyuzi nyingi tu hiyo biashara ya mitumba imeelezewa.Mmh ina maana hakuna wataalam wa hii kitu humu
nimeiona mkuu text yako!
ila biashara ipo hivi:
kila baro inavyotoka nje inakua na mchanganyiko wa nguo zote yaani grade A, B,C na zinginezo na haswa kwa zile mixture kinachosumbua kuna aina fulani ya baro huwa wabongo huzifungua na kuchukua nguo nzuri then huzipack tena
sasa hukikumbana nazo hizo zilizofunguliwa unaweza ukakata mtaji
kuna aina kama tatu hivi za baro ambazo ni nzuri kwa mnada kwani zenyewe ni mixture
aina ya kwanza ambazo zenyewe hutoa nguo nyingi ambazo ni grade one ni Australia ambazo zinapatikana ktika uzito wa kg 100 na bei yake ina range Tsh 450000 hadi 500000,hizi ni nzuri na ndio ninazoziuza Mimi nawe nakushauri uzipate hizo kwani si rahisi kukata pesa yako ,umeanguka sana unarudisha pesa yako
za pili ni baro za kichina nazo ni nzuri na hata bei yake ni affordable kg 100 @ Tsh 370000 hadi Tsh 420000
na za tatu ni za kimarekani maarufa kama SUMMER, zinapatikana katika uzito wa kg 50 na 80 na bei zake Tsh 250000 hadi Tsh280000 kwa za kg 50 na Tsh 320000 hadi Tsh370000
ndio hivyo mkuu jipange kachukue mzigo huo
Balo zipo sehemu nyingi
Changamoto ni iyo uchakachuzi wa mabalo, niliwai kwenda uganda balo hazifunguliwi.
Mara nyingi balo ikiwa na koa, imefungwa na yale mabati inakuwa haijafunguliwa, ila ikiwa na plastic mara nyingi izo ndizo zimefungwa upya, ila c lazima iwe ivo.
Haya ni jibu swali wanalokwepa wengi zinapatikana wap?
Ukifika mnazi mmoja dar, kama unatoka k.koo nyooka moja kwa moja kama unaenda mnara wa saa au stesheni, unapovuka tu makutano ya pili ya mataa, ya mnazi mmoja kuna maduka wanauza sana kanga na vitenge, kuanzia hapo, maduka ya mitumba nikibao, nenda mtaa wa pili kama sikosei unaitwa sofia, maduka kibao hapo mitumba tupu, yani zunguka eneo ilo utapata mitumba kibao.
Pili ukiwa congo, k.koo kituoni mkono wa kulia ukiwa unaelekea mnazi lipo duka moja hapo kwa mhind linapakana na duka la samsung.
Tatu Magomeni, ni eneo jipya hili, ofis za ttcl ukifika hapo upande wa pili utaona mitumba had ya viatu wholesale bales.
Hapa magomeni ni makutano ya mataa pale ukiuliza ofis za ttcl utaoneshwa.
Changamoto ni kupata bales nzuri, kama unaweza mtafute mteja wao mzoefu wanaempaga vitu bora, akuchukulie.
Au washikishe wale jamaa tingo wa dukani kitu kidogo, wambie nipe kitu cha maaana jifanye ni mzoefu ila unabadili duka tu.
Ukijifanya mzoefu usizubae, kwa mfano ukiuliza mixer ya nguo za kike, akikuuliza kg ngap unakuwa shapu kuonesha unajua, sio wanauliza Kg hujui kuwa balo zina kilogram
Au unaulizwa material inayotaka hukui, either cotton, nylon n.k
Nahs nimesema kidogo kitakachowasaidieni