Sijafanya biashara ya nguo za watoto ila nishafanya biashara ya nguo za mitumba , ni biashara nzuri sana kama utakuwa mtu wa kujituma, na inategemea biashara yako unafanyia sehemu gani, ukiwa unafungua balo la mtumba na nguo zikatoka nzuri basi jua utapata pesa yako mara mbili ya mzigo.
Mfano ukifungua hilo balo moja la nguo za watoto, watakuja walengaji uta wauzia,wateja wa reja reja uta wauzia,wateja wa jumla uta wauzia, inategemea wewe biashara yako unataka kufanya vipi? Mana wengine huwa wanauza kwa kwenda kwa kwenye minada. na bei ya balo inategeme na mzigo unao chukua coz kuna kuwa na lebo, kama za Canada, China na kwingineko.