Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Habari zenu wandugu;

Kwa wenye utaalamu wa biashara ya mitumba nahitaji elimu yenu. Wapi nitapata mabalo ya mitumba 1st grade? Ambapo hakuna kupigwa famba? Au jinsi ya kutambua grade nzuri?

Natanguliza shukrani!
 
Ingia Nairobery kwenye soko moja laitwa Gikomba.
 
Msenyele,

Kaka mi hata kuanzia biashara sijaanza na gather info kutoka kwa watu wenye ujuzi kidogo. Kwahiyo siwezi hata kuahidi mkopo Mzee. Ila ntakapokuwa tayari ntatoa taarifa hapa then tutaongea bei.
 
BADILI TABIA
Unaishi wapi?Kama ni Dar nakushauri uende mwenyewe pale Karume...Jaribu kupeleleza na kufanya karisechi kwa kuwauliza wale vijana..Jenga kiurafiki na ikiwezekana uende hata na soda..bila shaka utapata mengi pamoja na masoko na other challenges.

Utanilipa kiasi gani nikupeleke kwenye mizigo yenyewe hadi kukagua ruksa au ukitaka kuagiza nje upokee kontena bandarini ww tu.
 
Last edited by a moderator:
Ushauri wangu, lete hiyo mitumba tz 70% iwe ya kiume na 60% ya kike! na kwakua unaanza lete grade 1, ili ujenge good will na wateja! wahindi wanacho kifanya wanaleta grade tofauti kisha wanachanganya ili kupata super profit! Uzuri mmoja ni kuwa, ukileta mali nzuri. Mteja mmoja akifungua na kuona ni mzuri, huwaambia wenzake na wote huja kwako.

Kizuri kingine ni kuwa, kuna watu wana hela zao chini..Wao wanasubiri wasikie fulani kafungua mali nzuri na inakimbia, yeye anakufuata, kisha anakupa hela ya belo zote ulizonazo store kisha yeye anauza rejareja kama wewe ila anakuwa kaongeza elfu kumi au ishirini kwa belo! kwenye hii biashara, umakini mkubwa ni ubora wa hizo nguo na jinzi sio jinzi tu ziwe za kisasa, sio chupa (juu pana, chini inabana, hutouza)! nilishwahi kuingiza nguo frm tz zamani from usa via charlestone port via s.carolina, zilinikata kwa kweli.

Hakikisha kwenye huo mtumba, hakuna sox wala chupi. TBS watakupa shida bandarini.

Kama unaweza, mkuu badala ya nguo za mitumba weka mitumba ya viatu vya kiume, au changanya nguo za mtumba na viatu vya mtumba ili upime biashara! open shoes, canvas, mukasin, sendoz raba n.k! Kikweli biashara ya viatu vya mtumba inakimbia kupita maelezo.

Huna haja ya kuwa na duka au stoo kariakoo...wewe ukitangaza tu una viatu vya mtumba hasa vya kiume na kama utaweka kidogo vya kike visiwe kokoko, watu wananunua mali yote kwa siku moja! Ukiwa mvivu, utawauzia kontena lote, faida utaiona lakini ni kidogo sana ukilinganisha na watakachoenda kupata wao.

Kila siku asubuhi saa kumi uwe ushafika kariaokoo (mchikichini) na baloo tatu au nne hivi na kuhakikishia mpaka inafika kwenye saa moja asubuhi, unakuwa umemaliza mali yoote na unarudi home na furushi la kimango! Kule unakodisha meza kwa huo muda ni shilingi 5,000/- na vijana waaminifu wapo wa kukusaidia kulinda na kupiga debe, wewe kazi yako ni kupokea hela!

Kinachofanyika ni kuwa a day before upeleke hizo balo za viatu kariaokoo, unaita vijana wanatenganisha viatu vya kushoto na kulia, kwahiyo ukifika mchikichini asbuh unamwaga eiza vya kulia unabaki na vya kushoto and vice vser! Akikipenda kiatu unamtajia bei, bkoz kila kiatu kina bei yake, anakupa hela huku ameshika kimoja alicholipia! wakati wakufunga biashara, unampa mguu uliobakia.

Ofkoz, hadi mida hiyo lazima kuna pea kadhaa zinakuwa hazijapata wanunuzi, good news ni kuwa pembeni kuna watu kibao wanasubiri muhesabiane in a flat rate vyote vilivyobaki...ana ku'cash wewe unarudi na hela home saa moja asbh, na kuandaa mazingira ya kesho!

You can send mtu wako pale mchikichini, mida hiyo asbuhi akathibitishe nilio kwambia!
 
BADILI TABIA
Unaishi wapi?Kama ni Dar nakushauri uende mwenyewe pale Karume. Jaribu kupeleleza na kufanya karisechi kwa kuwauliza wale vijana. Jenga kiurafiki na ikiwezekana uende hata na soda..bila shaka utapata mengi pamoja na masoko na other challenges.

Thanx my dear.
 
Last edited by a moderator:
Yup China kuna mitumba mpendwa tena sagula sagula
Ukienda Guangzhou, kuna soko kubwa linaitwa Canan "jianan"...huko kuna mtumba na nguo mpya pia.

Nataka kwenda Canan "jianan" utansindikiza.
 
Back
Top Bottom