Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Wenye ufahamu wa biashara hii watusaidie tujifunze zaidi masoko na changamoto zake
 
Mimi nakupongeza kwa ujasili lau wa kuuliza tuu na ninakutaka usikate tamaa.Kumbuka hiyo biashara inachangamoto zake Naomba hizo changamoto ukabiliane nazo usiteteleke.

Leo embu toka kazunguke maeneo yanayouzwa hizo nguo km Ilala.Tandika Kkoo hata Mwenge najua utakutana na wenzio walioanza hiyo biashara waulize alafu fanya utafiti kisha anza

Sina zaidi nakutakia kila la kheri.

Kumbuka mguu wa kutoka Mtume kaumbea.
 
Nimependa ku share kuhusu biashara ya mitumba kutoka Kampala. Lengo ni kuwapa ufahamu kwa wale wenye interest. Safari yangu ya kwanza kwenda Kampala nilienda kama kutembea na kurudi na haya ndio niliyojifunza:

1. USAFIRI:
Nilipanda bus la friends kutoka Bukoba mpaka Mutukula. Kumbuka lipo pia la kutoka Mwanza to Kampala. Kuna hiace/coaster za Bukoba mpaka Mutukula. Yapo pia mabasi yanayotoka Dar es Salaam to Kampala mfano Falcon, mengine siyajui. Kutoka mwanza pia Kuna mabasi mengine kama J4

2. KIBALI CHA KUSAFIRI DHARURA /Emergency travelers documents:
Wengine sisi tumezoea kuita passport. Hiki hukatwa kwa mwaka mmoja. Taratibu zake ni cheti cha kuzaliwa na malipo ambayo ni elfu kumi kama sijakosea labda kama imepanda maana mimi changu nilikataa last year desemba. Kibali hiki kinakuwezesha kusafiri nchi tano mpaka sasa nazani including South Sudan ila sina uhakika. Unapokwenda Uganda ukipitia Mutukula, mihuri ya katika kibali chako unagongea Ofisi za Immigration za Uganda kwa kuanza na watanzania (exit) then Uganda (enter) and vice-versa kama utatoka Uganda kurudi Tanzania mihuri unagongea immigration ya Tanzania ila sijui kama imebadilika kwani ukisafiri kwa basi kila kitu Safi kwani utauliza kwa wazoefu au bus likifika border utaona tu wazoefu wa naelekea wapi.

3. KUBADILISHA FEDHA: Wapo watu wa ku change pesa from Tz shilingi to Uganda Shilling and vise versa, hapa epuka kubadilisha fedha kwa wale vijana wenye sare ambao wanatembea na pesa. Kuna maduka ya kubadili fedha kibao. Ukiwa mgeni na safari hizi jaribu kupiga mihuri uhamiaji then nenda ka change pesa kwa haraka maana Kuna watu huwa wanaachwa hapo kwa kuzuzuka na Mutukula.

4. KAMPALA:
Ukifika Kampala utagundua tu utofauti wa kwetu Tz na Uganda. Waganda ni wachapakazi sana, biashara every corner of the city. Kuna sehemu nyingi za kufukia. Mimi nitajikita sehemu moja tu, kuna GEST inaitwa KAMPALA GUEST HOUSE iko karibu na Owino market. Bei za vyumba ni 20 mpaka 26. Kuna usalama wa kutosha na pia kwa sisi wazee wa second hand ni Bomba kwani Owino the market iko karibu.

5. MITUMBA YA KAMPALA: Hiki ndio kiini cha uzi huu. Jamani Kampala Kuna mtumba mzuri sana yaani najiuliza wao wanatoa wapi kwani ni mzuri sana, mashati, magauni, mikoba, mabegi, viatu, sweet pants n. K.

6. LUGHA: Hapa ndio kwenye shida sasa. Lugha kuu ni Luganda na Kiingereza katika mawasiliano kibiashara. Shida inakuja pale wanapojua sio wa kwao huwa wanapiga bei mbaya. Bora uwe na mwenyeji au jifunze Luganda katika kutamka pesa yao kama Lukumi (1000) mpaka milioni. Ila hata kiingereza poa cha msingi bei utakayotajiwa linganisha na ya huku nyumbani. Nashauri kwenye kununua marobota ni bora ukawa na mwenyeji muaminifu akusaidie kwani Kuna robota nyingine sio fashoinable yaani ni grade mbovu. Hakikisha unapata robota zuri usije ibiwa.

[HASHTAG]#Njooinbox[/HASHTAG] kwa maelezo zaidi au 0757463047 au 0676463047. Napatikana hewani zaidi ila nisipokuwa hewani simu inakua chaj.
 
Huu ni mwendelezo wa kuhusu biashara ya mtumba kutoka Kampala.

Unapokuwa Owino market jaribu kuuliza sehemu wanazouza kwa bei ya jumla. Sehemu ziko nyingiiiii sana kwani hata baadhi ya maeneo yaliyo mbali kidogo na Owino Kuna maduka ya Second hand whole salers kwa mfano maeneo ya kisenyi bus terminal.

Ndani ya Owino market ni mwendo wa kutoa mguu niweke mguu maana ni watu wengi na kelele za wachuuzi za kukaribisha wateja wa retail. Ukitaka kununua kwa rejareja poa tu kwani ukiamka asubuhi saa moja, ukiwa na speed mpaka saa tano unaeza kuwa umenunua mzigo wa kutosha.

Kampala Kuna masharti ya mtumba mazuri sana. Mi huwa hata ofisini wanakubali na hata wale wa masharti ya shop special nawatoa knock out. Bei za masharti mazuri ni elfu kumi mpaka 20 ya kiganda. Ila kwa hapa nazunhumzia kwa wale ambao wanaotafuta ya kuvaa wao na sio ya biashara.

Kuna magauni na tops, pia blouse za kina dada nzuri sana yaani ukiingia Owino for the first time unaeza changanyikiwa.
Ukiwa Owino jaribu kukalili njia za kutoka maana unaeza jikuta unachanganya uliingilia wapi.

Kuna nguo za watoto nzuri sana. Unaeza nunua kwa issue binafsi au unaenda uza na kupata faida Kubwa
Karibu Owino sio kibiashara tu hata wale wapenda bling bling just go to Kampala for vacation and do shopping utaniambia mtumba ule hakunaga.

Kuna mikoba na mabegi ya mtumba mazuri sana. Hapa ngoja nikazie.


BIASHARA YA MTUMBA ILIYOPEWA KISOGO NA WENGI

Hapa naomba kuzungumzia second hand bags (mabegi, mikoba na pochi za mtumba).Wengi tumekuwa tukiangalia nguo na viatu tu na kusahau biashara moja ya bags. Napenda hapa nijikite na bags from Kampala (mivumba).Kampala Kuna bags nzuri sana, kuna mikoba, mabegi na pochi amazing. Unajua wanafunzi wanapenda begi nzuri na ngumu yaani kwa Kampala ni noma.

Vipi kuhusu mama zetu na dada zetu kwenye mikoba ;wanawake wa mji wanapenda kuwa na vitu unique bhana, Leo msibani ana pochi hii, kesho sokoni ana mkoba huu, keshokutwa saloon au jumatatu mpaka ijumaa kazini ana change mikoba tu sio anarudia mkoba mpaka unapauka kwa Jua.

Unajua Akina dada wakikutana kwenye shughuli zao hupenda kuwa wamependeza from toe to head, sasa mkoba muhimu au pochi. Kuna Luis Vuitton, Anna Sui, Gucci, Prada etc za mtumba.

Mabegi ya shule pia yapo mazuri sana na ukiwa mjini yapo unauza hata 40 kulingana na uzuri na ugumu wake.
Jaribu kufanya hii biashara kwani ukichukua mzigo the mtaji flani mkubwa hautajuutia aisee kwani biashara hii inaihitaji iwe na mzigo wa kutosha.

Kwa mfano umechukua mzigo wa milioni mbili za kibongo ukapata mzigo wenye items 600, ukaamua kila item uuze elfu 10000 utapata ngapi? Na hapa umepigia kwa bei flatlet, kumbuka Kuna mikoba ipo ya mpaka 20,, 30 na zaidi kulingana na eneo ulipo, sio uwe Chato au Buseresere afu utegemee uuze kwa bei kubwa utajikuta biashara yako unasubiri mwisho wa mwezi tu salary itoke ndio uuze.

[HASHTAG]#karibu[/HASHTAG] tuunge umoja kibiashara yaani kufanya safari za kibiashara Kampala tupige hela kabla mtumba hujapigwa stop 2018
Wale wa Mwanza, Dodoma,Geita Musoma n. K nafasi ni hii sio lazima tuende Dar. Afu mtumba wetu unachachuliwa sana.
 
Kwel kabisa mkuu,kampala vitu vya mtumba vipo vya kutosha na vizuri pia sio kubwa sana,kama mimi nlienda kuchukua viatu vya kike na vya kiume,kwa viatu vya kike nlinunua kwa 10000UGX ambayo ni kama 7000TZS na viatu viko bomba sana.
 
Kwel kabisa mkuu, Kampala vitu vya mtumba vipo vya kutosha na vizuri pia sio kubwa sana,kama mimi nlienda kuchukua viatu vya kike na vya kiume, kwa viatu vya kike nlinunua kwa 10000UGX ambayo ni kama 7000TZS na viatu viko bomba sana.
Unaenda lini tena mkuu tufungue kijiwe chetu?
 
Elezea transport cost na disturbances za border kupitisha mzigo....
Suala la transport cost sina uzoefu sanaa ila kwa kupitia conductors wa mabasi ni rahisi. Last time i heard from somebody kuwa waweza lipia 40000 up to 60000 for robota
 
Back
Top Bottom