Biashara ya Night Club Dar imekufa?

Band zimepauka mbaya. Yaan huruma. Na mchezo wa Karaoke nao umefika tamati.
Ama kweli kila zama na kitabu chake...naona sahivi Twanga pepeta inajikakamua kwenye kupiga bend ila sio kama zamani zikipiga Mango garden

Karioke nayo naozo naona zimeanza kuchoka

Sijui wadau wa bar za usiku wanataka nini nowadays
 
Hii inaitwa transformation...to the level where you can drink and play in a open zone.Ila ile biashara ya kufungiana ndani hakuna
 
Un
aonekana unapenda sana kubambia dadeki..siku hizi watu wanaangalia maokoto, bar zinawapa pesa nyingi..tofauti na zama zile ambazo vibaka walikuwa wakiingia night clubs kwa ajili ya kwenda kuwaibia watu.

Bar huwezi kukaa saa nzima hujaagiza hata kinywaji...lazima waje kukuuliza
 
Miaka ya 90' tunatoka home usiku tushapiga msosi wa maana , tunakwenda kudance bills mfukoni una pesa ya kiingilio na nauli ya kukurudisha home. Full kubambia milupo...watoto wa siku hizi hawezi kujua hizi mambo....nostalgia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…