Biashara ya Night Club Dar imekufa?

Biashara ya Night Club Dar imekufa?

Habari wakuu,

Naona siku hizi zile Night Clubs ndani ya jiji la Dar es salaam hazipo tena zimefunikwa/replaced na Bar kubwa kubwa.

Mfano hapo nyuma palikuwa na club za mziki mbalimbali mfano Billcanas, Maisha basement, Ambiance n.k Lakini siku hizi zile Nights club zimevunjwa na kugeuzwa Lounge,Casinos au bar.

Siku hizi hata ukitaka kuingia club kwa ajili ya kucheza mziki, utahangaika sana tofauti za hapo nyuma kidogo badala yake utaishia kukaa kwenye bar, lounge kubwa kubwa kama vibez lounge, BM Lounge n.k ambazo si club bali ni bar zenye open space kwa ajili ya kukaa na kunywa pekee mziki upo lakini hauna privacy kama club.
Siasa za Awamu ya Tano na RC wa zamani.....nani angeenda Night Club?

Pia kulikuwa na wimbi la wasiojulikana ambao hadi leo hawajajulikana ilihatarisha usalama wa wala bata usiku.
 
ELEMENT masaki, WARE HOUSE masaki, SAMAKI SAMAKI masaki, 124 masaki, wavuvi camp kidimbwi nk
Nafikiri zote ulizotaja zipo tofauti na anazomaanisha, kwa mfano samaki samaki au element ni yofauti na bilcanas au club maisha jinsi zinavyo operate, hazina dance floor, hazina music special wa ku dance badala yake kuna music .changanyiko hasa wa kusikiliza huku wahudhuliaji karibia wote wakiwa wamekaa na kunywa badala ya ku dance.
 
Tembea mkubwa night club choice dar tu ziko nyingi saaaana. Yaani night club ni biashara ya pesa kuliko hizo open bar zenu za kitambaa.
Sasa sijajua umeangalia wingi kwa level ipi. Maana bar hizo ni chache sana zinazo perform kushinda night clubs.
Pitia masaki ujifunze.
Mbona hutaji majina ya hizo night clubs?
 
Nyakati zinaenda mbio..

Sehem nyingi hawajui kupiga MZIKI mzuri..

Sehem nyingi zina watu wanyasa wanyasa (Ukipiga nyimbo nzuri hawana vibe nazo maana hawazijui).

Mie napenda mziki mzuri.. ndio starehe yangu.

Nimeamua kutengeneza Mini-Bar hapa kwangu seblen kwa pembeni kdg, nikiw Off kazini basi nakaa ktk ki-bar changu nafungulia mziki taratiib napunguza chupa.. bila bughza na mtoto wa mtu..

Nikitaka NYAMA naingia Telegram napoint minofu yangu nakuja kujilia ndani.
 
Mkuu wewe ni kama mimi. Nilijitengenezea utaratibu wa kwenda kusikiliza miziki mizuri kila ijumaa ila kwa sik hizi imekuwa changamoto.
Enzi za Kikwete tuli enjoy sana
 
Attachments

  • Putin.jpg
    Putin.jpg
    3.4 KB · Views: 5
Mkuu wewe ni kama mimi. Nilijitengenezea utaratibu wa kwenda kusikiliza miziki mizuri kila ijumaa ila kwa sik hizi imekuwa changamoto.
Enzi za Kikwete tuli enjoy sana
Siku hizi hakuna wapigaji wa mziki mzr kingine wale host/Dj's almost wote hapa TZ wanaigana Kuongea.. hakuna ubunifu.

Ni vyema ukajifungia ndani na Non-stop music Playlist yako safiii.. ukaepusha mengi.
 
Na ndicho kilichonikimbiza mimi. Yaani kuingia tu mashoga kibao halafu wanachukuliana poa tu na masharobaro wa mule plus wahuni. Sasa mimi hata nilivyovaa nikaona hapa nimepotea njia, nikanywa safari 2 nikatembea.

Kino na mashoga ndio kwao mimi ndio maana Kino na Mwananyamala zimekaa kushoto kwangu.
 
Back
Top Bottom