Asante mkuu wadau wamenipa msaada wa kutosha kabisa. nishindwe mimi tu.Nipo Mkubwa nimefuatlia michango nadhani wadau washakupa majibu jinsi ya upatikanaji wa Samaki,thanks
kwanini usitumia coldbox kama hili.unapanga fish wako wengi kuliko kutumia ndoo?.unaweka na seal hapo.Ok tuanzie hapa ndoo moja samaki wanasafirisha sh ngapi??
Ile ya 20 lts au wanatumia kipimo gani kusafirisha samaki kwa ndege??
kwanini usitumia coldbox kama hili.unapanga fish wako wengi kuliko kutumia ndoo?.unaweka na seal hapo.
Bei sidhani kama ni kubwa sana,itakua wanalipa kwa kg.
Tafuta contact na mtu aliye mwanza anakua anakutumia kwa ndege kila siku.
Kwa ndege hatopata faida nzuri coz n bucha,kuna magar special yanatransfer samaki kwa bei rahisi
hayo magari hupatikana wapi?contact?.Kwa ndege hatopata faida nzuri coz n bucha,kuna magar special yanatransfer samaki kwa bei rahisi
ndoo inabeba samaki wangapi kwa wastani?ndo kubwa inasafrishwa kwa elfu.20..ukchkua nyngi unafanyiwa discount kwa uku mwanza..na wanaosafrsha samak kwa ndege ni swis port..
Pamoja na maelezo mhimu ya King, na kwakuwa nipo kwenye mchakato wa kuanzisha hii biashara naomba niongezee kidogo. Mimi nategemea kuifanya katika kwa kiwango cha kati na hivyo wateja wangu wakuu nitategemea mahotel na watu wa kipato cha kati na siyo mama lishe. Mambo makuu ninayoyafikiria ni haya
- Jina la kampuni linalofanana fanana na chakula-nitakuwa na matawi mikoa mitatu (Dodoma, Arusha, Dar)
- Location ya biashara-nafikiria iwe kwenye junction kama mwenge kwa Dar
- Means of Transportation-Nitakuwa na gari kubwa ya freezer kwaajiri ya kusafirishia kutoka Lake zone na kupeleka Arusha, Dar then Dodoma kabla haijageuza kurudi Lake Zone.
- Nitakuwa na Gari ndogo kila centre kwaajili ya kusambaza kwa wateja wa kudumu kama wenye hotel na mashule.n.k
- Nitakuwa na Deep freezer kwa kila kituo.
- Nitakuwa na standby Generator kukabiliana na changamoto za TANESCO kwa kila kituo
- Nitatengeneza machinjio ya kisasa-hii ni plan ya baadae baada ya kupata shamba la kutunzia mifugo
- Nitakuwa na shamba la mifugo ambayo ndiyo malighafi yangu
- Nitakuwa na kituo cha kukusanyia samaki hapo Mwanza-Natafuta mtaalam wa kutengeneza Coldroom
- Bidhaa nitakazoanza nazo ni-Nyama ya Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo. Kuku wa kisasa na kienyeji, Samaki aina ya Sato na Sangara, Lakini pia nitakuja na mchele kwa Arusha na Dodoma......tayari nina 100bags za kuanzia na nipo nafunga mshine ya kisasa ya kukoboa na kubangua mchele na kufunga 5, 10. 15, 20kg
- Project to start in June 2014.
Tafadhali mawazo yenu. Nipo tayari kulipa gharama za Busness Plan ila kwa mtu mwenye input ya maana.
Salamu wana JF.
Nimepata mchongo, kuna mtu toka nchi za northern Africa anataka nifanye
nae biashara ya samaki. Yaani namtumia samaki toka huku TZ kwa ndege.
Swali langu ni je, kama unataka ku-export samaki ni vibali gani
vinatakiwa? Je unaweza ku-export kama individual bila kuwa na kampuni
hasa kwa kuanzia?
Kama kuna mzoefu naomba anisaidie.
Pia kama kuna mtu anazo samaki toka lake victoria tunaweza kuongea jinsi
ya kufanya hii biashara.
Asanteni sana
Mkuu wee upo mkoa gani? me samaki naweza kupata so kama vp 2wasiliane tufanye biashara mkuu.
Nenda quality assurance offices za upande wa uvuvi watakusaidia then utatakiwa uwe na leseni au kibali cha kusafirisha hao samaki au products zote zinazotokana na samaki hicho utakipata huko huko ofisi za uvuvi.