Biashara ya Uchawi Tanzania


hii kali. napita tu.
 
Msitu wa Tembo ndo wapi?
 

WARAKA TOKA KUZIMU


THE SAINTS DARKNESS IN THE WORLD
UNDER GROUND DRAGON
SECTION WXXX69

23.05.2011

TO OUR DEAREST SAINTS

TANZANIA; KENYA AND UGANDA

Tunawapa pongezi kwa juhudi zenu juu ya kazi ngumu: tuliyonayo nyakati hizi za mwisho juu ya kuja kwake Adui yetu kulichukua kundi lake.

Tuna Mbinu ambazo kufikia sasa zinaendelea kufaulu nabado zingine zina shida sana upande wetu kuzifanikisha!!

Tungependa kuwaalika rasmi kwenye "kongamano kuu la Africa Mashariki na kati "Mwishoni mwa mwezi 30/07/11.

Jambo hili sio la kawaida kwetu japakuwa itakuwa mwisho wa mwaka. Lakini mambo yetu yanazidi kuharibika kwa upande wetu na baadhi yetu mkashindwa kutekeleza wajibu wenu wengine kukosa nguvu kwa kukawia kutoa sadaka zao.

Kwa usalama wetu acha tukutane nje ya mji katika lango kuu la kuzimu "Mushitara-Dar es Salaam" saa 6.30 usiku hadi saa 9.00 usiku na viti vyetu ni watu; bila kusahau chupa ya lita 5 za damu za watu na mchanga wa kanisani.

Kulingana na lengo letu mambo ambayo tutayazungumzia ni mbinu ambazo tungelifanya ili kuzuia Maombi yao adui zetu na kuvunja amani ya jamii kupitia Migogoro na Migongano ya familia hasa kwa viongozi wakuu wa Makanisa ya Kiroho na kuliwahi kundi lao.

Lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunamwangamiza hasa aliyekuwa Mkuu wetu wa uchawi Africa Mashariki na kati ndiye anayezifahamu siri zetu nyingi sana akawa amechukuliwa na adui yetu na kanisa lake linaenda kwa kasi saana wakiwachukua watu wetu maana amefichwa mno.

Kwa kulifanikisha jambo hili na watakieni nguvu kupitia kwa damu yetu DWS-UD na unasema mara sita; ukiwa umesimama na mara sita umechuchumaa, mara sita ukiwa umelala huku ukiwa uchi (666)

AMRI: sasa nendeni kwao ili kuharibu nguvu zao kwa kutumia sheria No. 999 WD ili kujificha (usionekane) unapozidi kuwasogelea na kuwafunga wanaume, wanawake na watoto wao.

Pia kumbukeni Yule M/kiti wetu wa wachawi Africa Mashariki na Kati aliyechukuliwa na adui yetu alipoanza maombi yake mmerudi nyuma sana. Huenda mambo yetu yakawa Mabaya zaidi ndio maana tunawahitaji mkapokee nguvu.

Pasipo kusahau kuwa yupo yule;
URGENT WETU MSALITI WA 1993.

Maeneo hayo tumempa jukumu kupambana naye ni (Madam-mwanamke) wa No 1-11-11-18 ambaye kufikia sasa anaendelea kutafuta njia ya kumnasa na kumharibia mipango yake mungu wao.

Hata hivyo kuna mbinu mpya tunayotaka kuwaelezea watu wa eneo hilo.

Jaribuni kufanya haraka sana ili kutoa kwa mara nyingine sadaka zenu ili kujiwekea ulinzi.

URGENT 1-14-14-18 amekawia tangu alipomtoa mama yake kafara hata sasa hajatoa mwingine akiulizwa anasema atatoa hivi karibuni. Tunawashukuru sana wale wenzake watatu walioshirikiana na kuleta watu wengi kwa ajali.

NOTE: Tumieni mbinu hizi ili kulizuia hili kanisa alilonalo huyu

FORMER URGENT 0-15-15-666

Maana yake anaanza kupanda juu kila kukicha hivi anasikilizwa na ataendelea kusikilizwa kuwaimalisha waliokuwa hawana nguvu amepanga kuwaimarisha kinyume na mambo yetu. Jina la kanisa alipo ni M.D.S Kimekuwa kituo cha uponyaji cha adui yetu akimtumikia.

YAH; NJIA ZA KUWANASA:

Tumieni hii hata kwa makanisa mengine na hata mbali na hilo ili kuweza kufanikiwa:-

  1. Kuzusha magombano baina ya waombezi ili kuwavunja wasiendelee kumtafuta mungu wao.
  2. Sababisheni hadithi kwa wingi wanapoingia ndani ya makanisa yao wakati wa kuja kumwomba mungu wao.
  3. Msiwaruhusu kuomba wakati wa kulala kwao (Janatus) maana hamuwezi kuwaona wakifunikwa na nguvu za mungu wao.
  4. Msiwape nguvu au nafasi ya kusoma Biblia; badala yake wapeni wakati mwingi wa kusoma magazeti, kuangalia Television zao.
  5. Sababisheni ufukara; mateso na pesa zao kupotea bila wao kujua ili wasimtolee mungu wao na walio na pesa roho ya ubahiri ya kutokutoa.
  6. Inueni nguvu za kuzini makanisani kwao baina ya viongozi na washirika wao na vijana kwa wasichana ili kupata nafasi y kuzima nguvu zao.
  7. Ibada zao ziwe baridi kabisa ili Roho wa mungu wao asipate nafasi ya kuongea na kusikia kutoka kwake.
  8. Tumieni ajali maana damu yao tutaitumia katika vikao vyetu.
  9. Akina mama wajawazito wazalishwe kwa operesheni ili kupata damu.
  10. Tumieni ukimwi wa kutengeneza kama pigo kwao ili kuwamaliza na kuwaletea aibu katika vifo vyao.
  11. Vurugeni umoja wa nyumba zao kati ya mke na mume, wazazi na watoto wao ili maombi yasipatikane.
ONYO KALI;
TAFADHALI MUWE NA UANGALIFU SAANA YA KWAMBA MAMBO HAYA YASIJULIKANE NA WAO. MBINU ZINGINE ZA KANISA MTAKUJA KUELEKEZWA KATIKA KIKAO KITAKACHOFANYIKA TAREHE 30/07/2011 "MU"D"

SENIOR URGENT: KUTOKA MAKAO MAKUU:

DW-SU: 13-1-3-18-9-1

Tafadhali tumieni usafiri aina tatu tu! (a) Ungo (b) Kijiko na (c) Kioo

Pia vaeni mapazia rasmi mnapokuja katika mkutano ili kuhifadhi heshima yenu kwa wageni wetu kutoka (hapa kuna maandishi ya kiarabu). UNDERGROUNE

Dugion Canada na ufilipino wakifundisha mbinu mpya za kukabiliana na makanisa pamoja na jamii zao. (Japokuwa: FORMER URGENT 0-15-15-666) anazifahamu!!
 
1.Tafadhali watanzania tutumie akili na uwezo wa kufikiri aliotupa Mungu kuchanganua yale yote tunayosoma au kusikia
2.La msingi sana IMANI kwa Yesu Kristo ni jambo kuu, na niseme sio kuamini tu kwamba Yesu ni Mwokozi bali kuishi maisha matakatifu, kusali na kuomba Kupitia jina la YESU katika kila kitu unachotaka kufanya.

HAKUNA KUBWA ZAIDI YA UPENDO, soma Biblia Upendo hushinda yote, haujivuni, hautakabali, haubagui,.........n.k.Wahubiri wa siku hizi hasa wa makanisa mapya hutawasikia wakitilia mkazo UPENDO na hawahubiri kabisa NENO hili. Kama unafuatilia kwa makini utagundua ni kwanini.

Kila uchwao wao wanahubiri namna ya kupata utajiri. Nakubaliana na Majimoto kwamba kuna uwakala wa shetani kati ya manabii, wachungaji, mitume na wanaojiita wenye upako, angalia kama utasikia kwa mwaka mzima wakihubiri Upendo, wako kimya kabia. Kwa namna hii msitegemee jamii ya kitanzania ikawa nzuri kimaadili.
3.usijali sana hizi details zinazotolewa hapa siju lango la kuzumu, n.k. yawezekano yapo lakini pengine yasisimua tu kusikia hivyo lakini weka imani yako kwa Muumba wako kila kitu kitakuwa poa tu
4.Mengine yawezekana kabisa ni kuweka utamu tu katika hadithi, au maelezo yaliyotolewa kwenye vitabu fulani lakini hatari ni kwamba baada ya kuaminishwa sana na mwandishi wa thread unaweza kujikuta ukiamini kila kitu(kama ilivyo kwa wengi hapa) na hivyo ni rahisi kwa mwandishi kuingiza yale anayotaka kusema hata ya kutunga tu
5.hadithi za uchawi zinasisimua lakini nyingi zinakosa authenticity (uhalisia)

Hiyo barua ya kuzimu yawezekana tu imeandikwa na mwandishi wa thread hii kwa kufuata yaliyotokea hivi karibuni kati ya viongozi wa makanisa ya kilokole na wengi wanaweza kuamini kirahisi hasa waliokwisha kuzama kwenye utamu na wasiochambua vitu kwa umakini mkubwa

6. Kuna logic fulani katika yale ambayo Majimoto anayosema, ulimwengu wa giza nakubali bila shaka kabisa upo na ulimwengu wa mwanga hakuna wasiwasi.
7. watu wasistushwe hata kidogo na mambo ambayo shetani anaweza kufanya. Ukiwa na Mungu wa kweli ndani yako utakuwa unasikia adithi tu na kamwe huwezi kudhurika na haya mambo, ni madhaifu mno mbele za Mungu! Nimeona katika maisha yangu na ninawatiisha hawa viumbe kwa nguvu za Mungu na hawana lolote! lakini ukiwa chini ya mbawa za YESU la sivyo utaipata.

Hata hivyo bwana Majimoto endelea kutupatia mambo haya lakini hakikisha kuchakachui kitu manake Mungu aona yote

SIFA NA UTUKUFU KWA MUNGU BABA YETU KATIKA JINA LA KRISTO YESU, AMINA!
 

Haya maneno kama vile yanatoka kinywani mwa mtu ambaye ni mchawi tayari! BWANA YESU akutembelee ili uachane na hiyo kazi ya shetani.
 
Mpendwa Fazili, ninakushauri tafuta gazeti la Msema kweli toleo 722 ujisomee mwenyewe kile Maji moto amebandika kwenye post yake.
 
Wachawi ni majenti wa shetani, kusudi lao ni kuangamiza maisha ya wanadamu, hukumu yao ni kifo wakipatikana wakiwanga, wakipiga bao au kutabiri kwa kutumia nyota.
 
Magerezani wapo mamia ya wafungwa, wamefungwa kwa makosa mbalimbali yaliyotendeka sehemu mbalimbali na kujikuta wanakamatwa kwa kushukiwa kuwa wao ndiyo waliofanya uhalifu huo.

Vidhibitisho vya upelelezi vilivyopokelewa na mahakama vinaonyesha pasipo shaka kuwa watu hao, ndio wenyewe waliofanya na kuhusika na vitendo hivyo vya uhalifu.

Ukweli ni kwamba licha ya udhibitisho huo wa kipelelezi usikuwa na shaka hata kidogo, lakini ukweli ni kwamba ,mamia ya watu wamefungwa bila ya kufanya kosa lolote, au wafungwa wengi waliopo magerezani leo siyo wahalifu kabisa.

Mara kadhaa umeshasikia au umeshashuhudia mwenyewe, mtaani kwako wanakuwepo watu wawili wanaofanana sana lakini siyo ndugu, wala hawana uhusiano wowote, watu mara nyingi wanaishia kusema, dunia watu wawiliwawili, kwa maana kuwa kufanana huko ni jambo la kawaida.

Kufanana ni jambo la kawaida sina tatizo nalo, isipokuwa kufanana huko ni pale inapokuwa ni mtego wa kichawi wa kukunasa wewe.

Wachawi wakinua kukumaliza hutengeneza mtu bandia, ambaye anachukua sura yako kama ilivyo, kimsingi mtu huyo ni jini linalobadilishwa umbo na kuvishwa umbo la binadamu. Mtu huyo badia mnakuwa munafanana kwa hali zote, kuazia nywele, macho, urefu, unene, rangi ya ngozi hadi jinsi unavyotembea na sauti.

Wakishalipatia umbile lako, wananunua nguo za aina zote ulizonazo, wananunua viatu kama vya kwako, wingi kama zako ikiwa ni mwanamke hadi aina ya uturi unaotumia unakuwa wa aina hiyo hiyo. Kwa ufupi mtakuwa mnafanana kuliko watoto mapacha.

Hatua inayofuata baada pacha wako kuumbwa, wanamtembeza maeneo yaleyale ambayo huwa unatembelea mara kwa mara, unapotoka nyumbani asubuhi, pacha wako naye huvalishwa nguo za aina ileile ulizo vaa siku ile. Kazi kubwa wanayoifanya hawa wachawi ni kuzuia msikutane uso kwa uso na huyo pacha wako wa kichawi. Wakiona njia anayopita pacha wako mtakutana uso kwa uso, basi pacha wako wa kichawi huzuiwa na kulazimika kurudi nyuma na kupita mtaa mwingine, ilihali tu hakuna siku wewe utakutana uso kwa uso na huyo pacha wako, lakini taarifa za uwepo wa mtu mwingine mnayefanana naye utazipata kwa ndugu na marafiki zako mtaani.

Baadaye mipango ya uhalifu huandaliwa, ama kuteka nyara magari, kuvunja maduka na kuiba au kuvunja benki, kila mtu anayeshuhudia uhalifu huo anashangaa fulani naye kumbe siku hizi ni jambazi, picha za cctv zinakuonyesha kabisa ulivyokuwa ukifanya uhalifu huo, mbaya zaidi uanapokamatwa alama za vidole zinapochukuliwa zinakuwa ni za kwako kabisa.

Unaposikia mtaani yupo unayefanana naye hata nguo unazovaa, chukua tahadhari, huo ni mtego utakaohatarisha maisha yako.
 
Lol! Majimoto hii sasa balaa! Na lengo la hawa wachawi kukupeleka wewe kwenye uhalifu ni nini?
 


mkuu mbona naona watu kibao wanafanana na watu naowajua lakini hakuna kitu kinatokea?
 
mkuu mbona naona watu kibao wanafanana na watu naowajua lakini hakuna kitu kinatokea?

director 1. Kufanana siyo tatizo, tatizo ni pale unapokuwa ni mtego wa kichawi.

Zimepita kama wiki mbili hivi, alifika dada mmoja nyumbani, hali yake ilikuwa ya simazi na alionekana kanyong'onyea kwenye lindi la mawazo, kiasi kwamba mara kadhaa, alishindwa kumbeba mwanaye vizuri hadi kuanguka naye.

Huyu dada alianza kusimulia mikasa inayomwandama yeye na mtoto wake. Anasema, amepanga chumba na nyumba yenyewe wapo wapangaji wengine sita. Mtoto wake bado hajatembea, ndiyo kwanza anatambaa, anasema huyu dada kuwa mara zote anapotoka na mwanaye kwenda hospitali, sokoni au mjini, huko nyumbani hutokea mtoto mwingine anayefanana sana na mtoto wake hadi nguo anazoonekana nazo ni sawasawa kabisa na nguo alizomvisha mwanae kabla ya kuondoka. Huyo mtoto wa kichawi anaingia kwenye vyumba vya wapangaji wenzake, anachofanya huyu mtoto ni kuharibu kila kitu anachokiona mbele yake.

Akikuta tv anaisukuma na kuiangusha, vyombo anavisukuma na kuanguka chini na kuvujika, kila siku amekuwa akiletewa mashitaka ya uharibifu unaofanywa na mtoto wa kichawi. Anaporudi anakutana na madai kutoka kwa wapangaji wenzake, huyu dada anapojaribu kuwaeleza kuwa siyo mwanaye alifanya hivyo, wapangaji wanashindwa kuelewa kwani mtoto wa huyo dada anafanana sana na huyo mtoto wa kichawi.

Tulimsaidia huyu dada kwa maombi ya nguvu na huyo mtoto wa kichawi alipotea kabisa.

Wachawi huwa wanafurahia sana wanapoona binaadamu anavyoadhirika kwa magonjwa, ndoa kuvunjika, watu kupoteza ajira n.k. Ipo siku fulani tulikuwa tunasafiri kwenda Arusha, bahati mbaya gari letu lilipofika Wami darajani basi letu lilipata hitilafu ambayo ingechukuwa muda mrefu kuirekebisha. Tukiwa maeneo yale tuliteremka bondeni karibu na mto wami, tukamkuta kijana mmoja akatusimamisha, akawa anatuambia angalieni upande wa pili wa mto kuna kijana (utingo) alikuwa na ndoo yake anataka kuchota maji, huyu kijana aliyetusimamisha akatuambia eneo hilo lina mamba wengi, akatuambia angalieni mamba watakavyomkata yule kijana utigo atakapoinama kuchota maji.

Kile kitendo cha kusema mamba watamkata yule kijana, bila kujuwa kila mmoja wetu alipiga kelele za nguvu kumuonya yule kijana asichote maji. Utaona basi wapo wanadamu siku zote wapo wakifurahia maumivu na misiba ya wenzao.
 
Kama hauna IMANI hakika umeumia! Hawana mamlaka kwa yeyote yule mwenye tumaini kwa Bwana wetu aliyekufa na akafufuka na siyo mwingine ni YESU KIRSTO ALIYEKUFA NA KUFUFUKA kwa sababu ya mimi na wewe majimoto. Shindwa pepo shindwa kwa jina la YESU!!
 
Bwana fazili unachokisema ni kweli kabisa nimehudhuria mahubiri kadhaa hasa makanisa ya kilokole mara nyingi mahubiri yao hutawaliwa na vitisho mara utasikia siku ya mwisho yaja ole wenu,mara hapa kuna wachawi na mengine mengi, sio vibaya kusema mambo hayo lakini tatizo ni kwamba vitu hivyo kuchukua 95% ya mahubiri madala ya kuhubiri vitu vya msingi kama upendo miongoni mwetu,unyenyeku,uadilifu na mengine kama hayo.walaka kama hizo zinaweza kutungwa ili kucapture watu fulani.mimi binafsi siamini kama kama kuna kitu kama hicho, ni janja tu ya wanaojiita watumishi wa mungu kunasa watu waende kwenye makanisa yao.kama wana nia njema na waendelee kufanya hivyo!
 
Wewe utakuwa "Mkatoliki wa msingi imara"! Mara nyingi Ukatoliki huko hukosi mahubiri ya UPENDO, UNYENYEKEVU, UADILIFU, NIDHAMU na mengine yafananayo! Big up KRISTO YESU BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YETU! AMEEEEN!
 
imani potofu, mrudieni Mungu na hayo yote (mema) mtazidishiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…