Magerezani wapo mamia ya wafungwa, wamefungwa kwa makosa mbalimbali yaliyotendeka sehemu mbalimbali na kujikuta wanakamatwa kwa kushukiwa kuwa wao ndiyo waliofanya uhalifu huo.
Vidhibitisho vya upelelezi vilivyopokelewa na mahakama vinaonyesha pasipo shaka kuwa watu hao, ndio wenyewe waliofanya na kuhusika na vitendo hivyo vya uhalifu.
Ukweli ni kwamba licha ya udhibitisho huo wa kipelelezi usikuwa na shaka hata kidogo, lakini ukweli ni kwamba ,mamia ya watu wamefungwa bila ya kufanya kosa lolote, au wafungwa wengi waliopo magerezani leo siyo wahalifu kabisa.
Mara kadhaa umeshasikia au umeshashuhudia mwenyewe, mtaani kwako wanakuwepo watu wawili wanaofanana sana lakini siyo ndugu, wala hawana uhusiano wowote, watu mara nyingi wanaishia kusema, dunia watu wawiliwawili, kwa maana kuwa kufanana huko ni jambo la kawaida.
Kufanana ni jambo la kawaida sina tatizo nalo, isipokuwa kufanana huko ni pale inapokuwa ni mtego wa kichawi wa kukunasa wewe.
Wachawi wakinua kukumaliza hutengeneza mtu bandia, ambaye anachukua sura yako kama ilivyo, kimsingi mtu huyo ni jini linalobadilishwa umbo na kuvishwa umbo la binadamu. Mtu huyo badia mnakuwa munafanana kwa hali zote, kuazia nywele, macho, urefu, unene, rangi ya ngozi hadi jinsi unavyotembea na sauti.
Wakishalipatia umbile lako, wananunua nguo za aina zote ulizonazo, wananunua viatu kama vya kwako, wingi kama zako ikiwa ni mwanamke hadi aina ya uturi unaotumia unakuwa wa aina hiyo hiyo. Kwa ufupi mtakuwa mnafanana kuliko watoto mapacha.
Hatua inayofuata baada pacha wako kuumbwa, wanamtembeza maeneo yaleyale ambayo huwa unatembelea mara kwa mara, unapotoka nyumbani asubuhi, pacha wako naye huvalishwa nguo za aina ileile ulizo vaa siku ile. Kazi kubwa wanayoifanya hawa wachawi ni kuzuia msikutane uso kwa uso na huyo pacha wako wa kichawi. Wakiona njia anayopita pacha wako mtakutana uso kwa uso, basi pacha wako wa kichawi huzuiwa na kulazimika kurudi nyuma na kupita mtaa mwingine, ilihali tu hakuna siku wewe utakutana uso kwa uso na huyo pacha wako, lakini taarifa za uwepo wa mtu mwingine mnayefanana naye utazipata kwa ndugu na marafiki zako mtaani.
Baadaye mipango ya uhalifu huandaliwa, ama kuteka nyara magari, kuvunja maduka na kuiba au kuvunja benki, kila mtu anayeshuhudia uhalifu huo anashangaa fulani naye kumbe siku hizi ni jambazi, picha za cctv zinakuonyesha kabisa ulivyokuwa ukifanya uhalifu huo, mbaya zaidi uanapokamatwa alama za vidole zinapochukuliwa zinakuwa ni za kwako kabisa.
Unaposikia mtaani yupo unayefanana naye hata nguo unazovaa, chukua tahadhari, huo ni mtego utakaohatarisha maisha yako.