Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
MajiMoto anajitungia yeye Mwenyewe tu Tanzania haiwezi kuishinda Nigeria kwa UchawiIna maana Tanzania inaizidi Nigeria kwa uchawi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MajiMoto anajitungia yeye Mwenyewe tu Tanzania haiwezi kuishinda Nigeria kwa UchawiIna maana Tanzania inaizidi Nigeria kwa uchawi?
Shetani ndiye mtawala wa dunia, ametapakaa kila kona ya dunia, angani yupo, nchi kavu yupo, ndani ya bahari na maziwani yupo. Kila mahali shetani yupo. Shetani kama mtawala wa dunia, anao wasaidizi wake na ana vikosi vya majeshi ya kupigana vita. Madhalani shetani anamtegemea sana shetani anayemiliki anga, huyu ni mwanamke anayejulikana kama malkia wa anga, ni mbaya na katili kwelikweli kuliko wasaidizi wote wa shetani. Malkia wa anga huwa hakai sehemu mmoja huwa anasafiri kuzungukiwa anga yote ya ulimwengu kuanzia dunia yetu sayari zote, nyota zote, hadi mwezini. Huyu malkia ana njia zake kabisa angani anazopita na anatembea kwa kuteleza kwenye ulimwengu usioonekana, huteleza kama wanamichezo wanavyoteleza kwenye michezo ya barafu.
Majanga yote makubwa yanayoikumba dunia husababishwa na malikia wa anga, kama vimbunga, matetemeko ya ardhi n.k.
Shetani anao wasaidizi wengine kama majini na mapepo, na yote yametapakaa dunia yote. Majini yanatumiwa sana na ulimwengu wa Kiaarabu, mapepo nayo yapo kwa wingi sana, kiasi kwamba hapo ulipo sasa hivi umezungukwa na mapepo kati ya 500 hadi 1000 au zaidi kutegemea na hali ya eneo, kama eneo hilo wanateketezwa kwa wingi wa sala ndivyo idadi kubwa ya mapepo hutumwa eneo hilo, kuzuia maombi na sala.
Hao ni baadhi ya wasaidizi wa shetani ambao wako katika ulimwengu usioonekana, kwenye ulimwengu unaoonekana shetani anawatumia wanadamu ndio hawa tunaowaida wachawi au waganga wa kienyeji. Hawa wachawi hutofautiana sana kutoka eneo moja hadi eneo lingine la ulimwengu wetu, tofauti yenyewe hutokea haswa kutokana na maendeleo na kiwango cha elimu ya eneo husika. Kwa mfano mchawi wa Tanzania wengi elimu hawana au ni ndogo sana, mchawi huyu ataloga kila kitu, hataki mtu ajenge nyumba ya bati, ataloga mkorosho, mbuzi, watoto wako yeye uchawi ni kuzuia maendeleo.
Wachawi wa uropa na marekani siyo rahisi kuwatambua, wamesoma na wana nafasi nzuri za biashara na utawala, wengi sasa hivi utawakuta wamening'iniza flash disk shingoni kumbe ni ungo wa kusafiria.
Yapo maeneo ambayo uchawi ni sehemu ya maisha ya kila siku ya watu wa eneo hilo, maeneo yanayoongoza duniani kwa uchawi ni:
a) Bara lote la Asia, Japan ikiwemo
b) Nchi zote za Kiarabu, Iran ikiongoza
c) Bara lote la Afrika, Tanzania ikiongoza
d) Marekani ya Kusini
e) Nchi za Uropa
Mkuu maji moto, nina maswali mawili.
1. Kwa mujibu mwa maelezo yako kuna tofauti gani kati ya msukuleni na kuzimu.
2. Je, mtu akichukuliwa msukule, anaweza kurudishwa kwenye ulimwengu unaoonekana? Na kama ndiyo anakuwa kama zamani? Na lile kanisa la Kawe ( zamani ilikuwa Ubungo maji), huduma zake zina association na mambo haya? Na hao wachawi/waganga wa kichawi wanaweza kurudisha maisha ya zamani?
Majimoto Tanzania inaongoza kwa uchawi Africa ni kweli au umekosea mimi nadhani ni Nigeria?! Tuambie vyema hapa
MajiMoto anajitungia yeye Mwenyewe tu Tanzania haiwezi kuishinda Nigeria kwa Uchawi
JE UNAJUA MSUKULE NI NINI?
Msukule ni mtu ambaye anahesabiwa amekufa, lakini ukweli ni kuwa mtu huyo huwa amechukuliwa na Mchawi ili amtumie katika kazi zake maalum au amtumie katika mambo yake mengine anayoyataka.
MSUKULE
Mchawi humfanya mtu huyo awe maiti au kama kitu kinachojiendesha chenyewe kikiwa kimekufa lakini hakijaoza wala hakiozi.
Mchawi kabla ya kumchukua mtu Msukule hufanya Mkataba Maalum na Jini anayeitwa "BAKAS" ili amsaidie katika kazi hiyo, na kuna Sadaka maalum ambayo hutoa kumlipa Jini huyo kama malipo ya kazi yake. Huyu Bakas ni Jini anayetawala siku ya Jumamosi.
Baada ya kukubaliana na Jini Bakas Mchawi huchagua mtu ambaye anataka kumchukua na akishampata huenda nyumbani kwa mtu huyo kinyume nyume mpaka anafika mlango wa mbele.
Anapofika mlangoni hunyonya roho ya mtu anayemtaka kwa kupitia tundu ya ufunguo na kama tundu hiyo haipo hutoboa tundu ndogo ambayo huiziba akimaliza kazi yake.
Baada ya kuipata roho anayoitaka huitia ndani ya chupa na kuziba chupa hiyo na kuondoka. Kazi hiyo hufanyika usiku wa manane kati ya saa nane na saa tisa usiku.
Siku inayofuata yule aliyechukuliwa roho yake huanza kuugua na hufa ghafla.
Baada ya Mazishi yule Mchawi huenda kaburini akiongozana na yule Jini Bakas ambaye hujigeuza kama babu kizee mwenye ndevu nyingi nyeupe ili kuuchukua ule mwili wa Marehemu.
Wanapofika makaburini yule Jini hukaa upande wa kichwani kwa maiti na mchawi hukaa upande wa miguuni na kila mmoja wao akifanya uchawi wake lakini kazi kubwa ya kumtoa maiti ndani ya kaburi kufanya na Jini.
Jini huomba kwa bidii na kunuiza Uchawi na husema maneno ya kichawi huku akimwaga juu ya kaburi majani ya Mkakaya (Acacia)
Mchawi yeye kwa upande wake husema maneno haya yafuatayo akirudia rudia "Mortoo tombo Mivi" maana yake ni kwamba "aliye ndani ya kaburi ni wangu"
Kwa nguvu za Uchawi mwili hutoka kaburini bila ya kaburi kuchimbwa na kusimama mbele yao na yule mchawi hukabidhiwa maiti huyo.
Baada ya kukabidhiwa kitu cha kwanza ambacho hufanya ni kwenda nyumbani na kumuonesha huyo ndugu zake kuona kama atawakumbuka.
Maiti huyo asipozinduka na kuwagundua ndugu zake au kutambua nyumbani kwao basi Mchawi hujua kwamba kazi imekuwa nzuri na hupelekwa nyumbani kwa mchawi.
Wakifika nyumbani Mchawi humrudishia yule Maiti roho ambayo aliiweka ndani ya chupa na kumnywesha dawa kali ambayo itamfanya asahau kabisa maisha yake yote ya nyuma yaliyopita na baada ya hapo maiti huyo atazinduka na kuwa Msukule.
Msukule ni binaadamu anayeishi lakini hana uhuru na anatumiwa kama mtumwa huku ndugu zake au jamaa zake wakijua kwamba amekufa.
Uchawi huu wa kuchukua Msukule ulianza miaka 500 na 1500 A.D. huko nchini Congo na Haiti na kuenea sehemu nyingi za Dunia
Vuta subira mkuu, serikali ipo kwenye mchakato
MziziMkavu, asante kwa maelezo yako, naongezea kidogo hapo kwenye rangi nyekundu.
Kwa kawaida mwili wa mtu bila roho hauwezi kuishi, wachawi wanapochukua roho ya mtu ndani ya mwili wake, hupulizia jini ndani ya mwili wa huyo mtu, jini hilo likishaingia ndani ya mwili huanza matatizo ya kuumwa magonjwa ya ajabu ajabu, ndugu zake wanapompeleka hospitali vipimo vinakuwa havionyeshi tatizo lolote kwa mtu huyo. Madaktari hujaribu vipimo vya kila aina na vya bei kubwa. Kawaida mtu wa aina hiyo ni lazima afe ndani ya siku saba, lakini wachawi wanaweza kuongeza muda wa kifo chake hadi wiki mbili au tatu ili ndugu zake wapoteze pesa zao nyingi wakilitibu jini. Mtu huyo anapokufa anatakiwa azikwe siku hiyo hiyo, kama kafa jioni hutokea pilikapilika za ajabu ambazo ndugu wanatoa uamuzi wa kumzika ndugu yao usiku huo huo.
Aina ya pili ni roho ya mtu kuchukuliwa kichawi, kisha wachawi kupulizia jini ndani ya huo mwili, mtu huyo ataendelea kuishi maisha ya kawaida wakati roho yake ilishachukuliwa na wachawi. Maisha ya mtu huyo yanakuwa ni ya kupoteza kumbukumbu na wakati mwingine jini lililoko ndani yake linakuwa na tabia ya kuibua magonjwa ya mara kwa mara ya aina moja kama kifafa au kisukari. Roho ya mtu huyo hutumiwa na wachawi kwenye shughuli zao za ulozi, au huziuza kwa watu wenye kuhitaji wafanyakazi kama ilivyo sasa hivi mashamba na viwanda vingi sana vinanunua roho za hawa watu, hutumikishwa kazi ngumu sana kila siku chakula chao kikiwa ni uji wa makapi ya nafaka.
Aina hii ya pili ndiyo maarufu sana hapa nchi Tanzania, kiasi kwamba sasa hivi kiasi cha asilimia 75% ya Watanzania hawapo au ni misukule lakini wapo barabarani wanatembea na kazini wanaenda. Mbaya zaidi ziko familia yote baba, mama na watoto wote roho zao zimechukuliwa, kurudisha roho hizi zilizochukuliwa kichawi zirudi na kuivaa miili yao inawezekana, tena ni rahisi sana.
Majimoto utafanyaje ili roho hizo zirudi na kuivaa miili yao? Naomba unielimishe. Ni vipi pia unaweza kuzuia haya yasitokee?
Hapo anataka umpigie goti Majimoto ndo atoe jibu. Majimoto bwana! hahaaaaaaaaaaaaa
maji moto
je wachungaji wa makanisa kama kakobe,mwingira na mama rwakatare na lusekelo
je wote ni wachungaji kweli?
kwa nini hawapatani?
maji moto
je wachungaji wa makanisa kama kakobe,mwingira na mama rwakatare na lusekelo
je wote ni wachungaji kweli?
kwa nini hawapatani?
Mchakato huu haukubaliki kwa Jina la Yesu