Biashara ya Uchawi Tanzania

Biashara ya Uchawi Tanzania

Vipi kuhusu wachawi wanaofanya watu wa kawaida kuwa invisible? yeye anajiona kawaida kumbe watu wanaomzunguka hawamuoni?

Joyceline, Maelezo jinsi ya kufanya mtu asionekane nimeyaelezea kwenye page 4 #62
 
Majimoto unasema vitu vingi vya kimaendeleo tunavyotumia vinatokana na ujuzi wa kuzimu. na komputa? Kwa hiyo sisi wote tunaotumia ukiwemo na wewe huoni kwamba nia mawakala wa kuzimu hapa dunia?
Vipi kuhusu ushoga kwani sku hizi nchi nying za Ulaya na Marekani wanaupigia kelele. Hauna uhusiano wowote na kuzimu au ushetani?

Jini Munsar ndilo linalosababisha ndoa ya jinsia moja , maelezo yake yako page 4 #78
 
Niko kijijini natayarisha shamba kabla ya mvua za masika.[/QUOTE

Kwa hiyo Majimoto unatuambia tutakumiss na hizi story au ni aje? dondosha vitu adoado baba mpaka kieleweke.

Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
Majimoto unasema kuwa misukule wanakula pumba za mahindi lakini huko vijijini kuna habari kuwa misukule huwa inapelekwa kwenye nyumba za watu hasa usiku kula chakula. Yaani mnakaa kula chakula cha jioni kumbe kuna watu wengine pia wanakula chakula hichohicho bila kuwaona. matokeo yake ni kuwa hata kama chakula kilikuwa kingi mnakimaliza huku hamjashiba maana walaji walikuwa wengi.
 
Sawa kabisa. Mwenye misukule hutuma misukule yake kula chakula cha familia za jirani kikiwa ndani ya sinia. Kitakachoshanga mpikaji ni idadi ya walaji na wingi wa chakula alichopika, lakini watalalamika hawakushiba.
 
Habari yako Mkuu Majimoto! Nimefuatilia kwa makini hii maada na naona unatoa elimu ambayo unatujuza vitu ambavyo tusivyovijua. Ila nina swali ambalo nitashukuru nikipata jibu lake. Ikitokea mtu anayejiusisha na mambo ya Uchawi yuko Tanzania then ikatokea hakaamia nchi za Ulaya mfano Ujerumani. Je anaweza kuhama na Uchawi wake mpaka huko? Kama inawezekana anaweza kuwanga kama alivyokuwa Africa? Pia anaweza kupata washirika wenzake ikiwa maeneo yakaribu ikitokea kuna Mchawi au wachawi mwenzie? Maana kuna msemo unasema Uchawi auvuki bahari.
 
1.Sasa mkuu, kuhusiana na yote hayo, ya ulimwengu usioonekana na sisi binadamu wa kawaida ni vp tuishi ili kuepukana/kuachana na matatizo ambayo yanasabishwa na hao wasionekana?.

2.
Na vipi unaweza kujikwamua iwapo unahisi/umepata uhakika kuwa umetupiwa majini,mapepo ili uweze kuishi maisha yako ya kawaida na uweze kutumia nguvu zako asilia pasipo kuwekewa ugumu?
 
Jamani hii mada ni nzuri maana inahusu maisha haya haya, lakini nashangaa hamumgongei thanks, sio tu kwa sababu jambo ambalo linalongelewa kuhusu uchawi lakini mpeni kwa habari na ufahamu alionao.
Nategemea baadaye atakuja na jinsi ya kuepukana na haya mambo.
 
Niko kijijini natayarisha shamba kabla ya mvua za masika.

Vp majimoto nasikia hata katika mashamba hayo unaweza usifanikiwe kama washirikina wakikuamulia, unaweza lima lakini unawalimia wengine, kweli?
 
majimoto mimi nina maswali haya....

1,je kuchoma ubani ni ushirikina?
waislamu na wakatoliki kanisani wanachoma ubani je ni makosa????????

2.umesema katika maelezo yako kuwa yapo majini kazi yao ni
kukufanya usisikie adhana na kengele ya kanisani....
je kwa nini? adhana ina nini mpaka jini likuzuie kuisikia?

3.waislamu wote ni wachawi?????????
 
Habari yako Mkuu Majimoto! Nimefuatilia kwa makini hii maada na naona unatoa elimu ambayo unatujuza vitu ambavyo tusivyovijua. Ila nina swali ambalo nitashukuru nikipata jibu lake. Ikitokea mtu anayejiusisha na mambo ya Uchawi yuko Tanzania then ikatokea hakaamia nchi za Ulaya mfano Ujerumani. Je anaweza kuhama na Uchawi wake mpaka huko? Kama inawezekana anaweza kuwanga kama alivyokuwa Africa? Pia anaweza kupata washirika wenzake ikiwa maeneo yakaribu ikitokea kuna Mchawi au wachawi mwenzie? Maana kuna msemo unasema Uchawi auvuki bahari.

Uchawi ni roho hai iliyokamilika, kila mchawi haijalishi yuko duniani, mwezini, ndani ya nyota au popote pale, hizi roho za uchawi hutambuana kwa urahisi sana, na ndiyo maana wanapowanga huwa wanaongea lugha moja kwa makabila yote wakiwa kwenye vikao vyao.
 
1.Sasa mkuu, kuhusiana na yote hayo, ya ulimwengu usioonekana na sisi binadamu wa kawaida ni vp tuishi ili kuepukana/kuachana na matatizo ambayo yanasabishwa na hao wasionekana?.

2.
Na vipi unaweza kujikwamua iwapo unahisi/umepata uhakika kuwa umetupiwa majini,mapepo ili uweze kuishi maisha yako ya kawaida na uweze kutumia nguvu zako asilia pasipo kuwekewa ugumu?

Ipo mamlaka moja tu yenye kukomesha mauzauza yote hayo. Ni YESU pekee
 
Vp majimoto nasikia hata katika mashamba hayo unaweza usifanikiwe kama washirikina wakikuamulia, unaweza lima lakini unawalimia wengine, kweli?

Unapanda mahindi unavuna mabua.

Jirani yangu alikuwa ni mkulima wa mpunga, aliponza kilimo alianza na ekari mia mbili za mpunga, aliajiri wataalamu na mpunga wake ulistawi vizuri, lakini wakati wa kuvuna mpunga, alikuta mpunga wote umeondolewa, na akaachiwa makapi.

Baadaye aliniuzia shamba lake, wachawi wa nchi wameshindwa kuingia, ekari moja ninavuna wastani wa magunia thelathini.
 
majimoto mimi nina maswali haya....

1,je kuchoma ubani ni ushirikina?
waislamu na wakatoliki kanisani wanachoma ubani je ni makosa????????

2.umesema katika maelezo yako kuwa yapo majini kazi yao ni
kukufanya usisikie adhana na kengele ya kanisani....
je kwa nini? adhana ina nini mpaka jini likuzuie kuisikia?

3.waislamu wote ni wachawi?????????

Ubani huendana sana na ibada za kishirikina, kila jini lina ubani wa aina yake ambao ukichomwa na kusoma dua, jini hilo hutokea, na kama unataka kulituma utatakiwa ulimweshe kwanza damu ya kuku, mbuzi, ng'ombe au ya binadamu ndipo ulitume kwenda kudhuru watu. Ndiyo maana unapokwenda kwa mganga wa kishenzi atakutaka ulete kuku kwanza ndiyo afanye uchawi wake.

Majini yanafanya Wakristo walale usingizi mzito wakati wa adhana, kwani wakati huo ndio wakati yanakwenda kwenye ibada, na ibada za Wakristo zinawazuia kutembea. Pia yanawafanya Wakiristo walale usingizi mzito wakati wa mahubiri, ndiyo maana makanisani watu wengi hulala fofofo kabisa.
 
Asante Majimoto kwa kujibu kwa ufasaha kila swali kuhusu ulimwengu uhusiano wa ulimwengu unaoonekana na usioonekana. Leo naomba unijuze vifuatavyo:
1:Vipi kuhusu Vibwego kwa maeneo ya Pwani na masharti yake ambayo huwa wanasema lazima usema hadhari kama atakufanyia shughuli? Haya na majini, misukule au nini?
2:Vipi kuhusu wale watu wanaoomba pesa na kifanyia kazi (hasa coins) ambapo mapato yako yanakuwa yanaelekea kwake? Kuna mtu alinishauri hasa Dar kutokutoa msaada kwa mtu yeyeote coins kwani huweza kuifanyia kazi kwa urahisi. kuna ukweli hapo Majimoto.
 
Ubani huendana sana na ibada za kishirikina, kila jini lina ubani wa aina yake ambao ukichomwa na kusoma dua, jini hilo hutokea, na kama unataka kulituma utatakiwa ulimweshe kwanza damu ya kuku, mbuzi, ng'ombe au ya binadamu ndipo ulitume kwenda kudhuru watu. Ndiyo maana unapokwenda kwa mganga wa kishenzi atakutaka ulete kuku kwanza ndiyo afanye uchawi wake.

Majini yanafanya Wakristo walale usingizi mzito wakati wa adhana, kwani wakati huo ndio wakati yanakwenda kwenye ibada, na ibada za Wakristo zinawazuia kutembea. Pia yanawafanya Wakiristo walale usingizi mzito wakati wa mahubiri, ndiyo maana makanisani watu wengi hulala fofofo kabisa.
Mkuu Majimoto,kwenye red napinga
 
Back
Top Bottom