Biashara ya Uchawi Tanzania

Biashara ya Uchawi Tanzania

Mkuu Majimoto,kwenye red napinga

Majini ni moja ya viumbe ambao hawaonekani kwa macho katika ulimwengu unaoonekana kuna aina kuu mbili za majini, yapo majini yaliyovurumishwa kutoka mbinguni baada ya kuasi, na yapo majini yanayotengenezwa kwa kufuata mila za Kiarabu, majini yaliyo vyurumishwa toka mbinguni yanamjua Mungu na siku zote hawasogelei nyumba za ibada, kwani wanaujua moto wake, majini ya kutengeneza hayaelewi chochote na huingia kwenye nyumba za ibada wenyewe kwa kutumwa au wakiwa ndani ya mwili wa mtu. Ndiyo maana yanapokemewa, hupiga kelele za kuunguzwa na moto.

Ili haya majini nayo yaweze kufanya ibada yao, Hutawanyika kwenye maeneo au nyumba zenye kawaida ya ibada na kuwalaza wahusika usingizi mzito, kwani kwenye ulimwengu usioonekana neno la Mungu ni moto makali sana na mara nyingi wamekuwa wakiumizwa vibaya sana. Mara kwa mara wamekuwa wakikosa kufanya ibada kwa kuwa huwa wamejeruhiwa, na ni najisi kufanya ibada ukiwa na majeraha ya damu.
 
Lakini Majimoto,unaposema suala la Maijini,mie naona hilo liko Kiimani zaidi.
Unaposema kuna Majini yamefuikuzwa toka Mbinguni,una Maana gani Majimoto,ina Maana Mungu nafuga Majini Mbinguni kweli,na kama ni kweli,aliyaumba ya kazi gani hayo Mjaini ilhal yanakuja ulimwenguni kukwaza kazi zake hapa Duniani Majimoto
 
Bramo. Lucifier alikuwa malaika mkuu wa sifa Mbinguni, akiwa na malaika wasaidizi, walipotaka kufanya maasi, Mwenyenzi Mungu aliwafukuza na kuwashusha kwenye moyo wa dunia. Kimsingi Lucifier ndiye sasa anajulikana kama shetani na malaika wasaidizi ndio sasa wanajulikana kama majini.
 
Majimoto, una maana wakati Mungu anamuumba Lucifier hakujua kama atakuja kuasi siku moja na kusababisha matatizo yote Majini na Mashetani wanayotuletea balaa hapa Duniani,Mimi siamini katika haya Majimoto,Mungu hana Makusudi kiasi hiko kutuwekea Vikwazo Vya kufika kwake yeye mwenyewe
 
Naomba nichangie nami hapa.
Swali ni moja ya maswali yanayochanganya watu wengi dunia. Na yapo mengi kama kama mungu alijua kuwa tutakula tunda la uzima kwa nini aliliweka? Kwa nini yuda alimsaliti yesu ingali yesu alijua kabisa na hakufanya jitihada za kumzuia kutenda hiyo dhambi ya kusaliti? etc.
Yote yanatokana na utashi wa viumbe na kuonyesha uwepo wa mungu. Kama dunia ingekuwa kawa tulivyoumbwa bila kufa, bila dhambi, nafikiri hapa uwepo wa mungu usigeweza kuonekana sana. Kumbuka yesu alitenda miujiza kama kuponya vipofu, kufufua wafu ili kuonyesha utukufu na uwezo wa mungu.
 
Hata hivyo Majimoto vipi kuhusu nguruwe na majini? Nasikia ukitembea na mfupa wa nguruwe majini hawasogei kabisa. Hii kweli? Kama kweli kwa nini hawasogei?
 
mhmm, majimoto kuhusu milango mikuu ya kuzimu na mambo mengine mingi umeyapatia, lakini kosa lako ni kuchukua ufahamu wako wa dini kuchanganya kwenye uelewa wako wa dunia isioonekana. ubani au oudy ni kinachotumika katika kumvutia mungu asikilize maombi yako, mana hutoa harufu yakupendeza, kwa mfano huwezi ukamwita mtu kwenye kikao chochote hata cha harusi bila ya kumpa kiburudisho ajisikie anatakiwa mahali hapo, na pia kila kizury hutumiwa vibaya, ndio hapo washirikina wanapoingia, na vile vile majini sio kama wote ni wabaya. nikama binadam hukijua kipi kizury na kipi kibaya lakini ni shauri yao kufata wanachokipenda, kuna msemo unasema ''sio lazima mtoto wa sheikh nae awe sheikh''.
 
Wachawi wa nchi wanapotoka usiku kwa shughuli za kuwanga, hawaondoki na miili yao ya kibinadamu, kinachofanyika ni kuwa roho au mtu wa ndani ndiye anayechomoka ndani ya mwili, kisha roho la uchawi hubaki na mwili wa mchawi kitandani.

Inapotokea kwamba roho ya mchawi ikiwa kwenye shughuli zao za ulozi, ikapigwa au ikazidiwa nguvu na mamlaka nyingine na akamudu kurudia mwili wake basi kipigo kile alichopigwa sehemu yoyote ya mwili wake kitadhihirika katika mwili wake aliouacha kitandani. Kwa mfano ikiwa roho yake ilikurupushwa sehemu fulani na akavunjwa mguu, basi akirudi nyumbani na kuvaa tena mwili wake mguu wake wa nyama utakuwa nao umevunjika.

Kwa kawaida maisha ya kiroho ya mtu ndio muhimili wa maisha ya kila siku ya binadamu na ndiyo yanakuja kujidhihirisha katika maisha ya kawaida ya binadamu. Wachawi wa nchi wanaweza kabisa kuyaona maisha ya mtu wako wa ndani na kumdhibiti. Ukitaka kujenga nyumba kubwa ya kisasa, ni lazima utafute mchoraji akuchoree ramani ya nyumba unayotaka kujenga, kama ni nyumba ya ghorofa, atachora, kama nyumba itakuwa chini ya ardhi atachora na atakupa michoro yako utafute fundi wa ujenzi kazi ya ujenzi wa nyumba yako ipate kuanza.

Kila binadamu anapozaliwa anakuwa na ramani ya maisha yake nzuri tu iliyoandaliwa na Mwenyenzi Mungu tangu maisha yeke ya utoto, maisha ya shule, maisha ya ndoa, hadi maisha yako ya uzee na inaonyesha kabisa mafanikio yako kuwa utajaliwa kupata watoto wangapi, utakuwa na nyumba ngapi, mashamba, viwanda nk. Wachawi wakiona ramani yako ni ya maendeleo na mafanikio makubwa, huingilia kati kuzuia ujenzi wa maisha yako usiendane na ramani yako. Wachawi wana uwezo kabisa wa kuichukua ramani yako na kuibadilisha na ramani nyingine ya hovyo, isiyokuwa na mafanikio.

Wachawi wanaiuza ramani yako kwa mtu mwingine, kawaida binadamu anakuwa na ramani moja, lakini wachawi wanaweza kumpa mtu zaidi ya ramani moja, zilizochukuliwa kwa watu wengine. Ramani yako kama imechukuliwa inaweza kabisa kurejeshwa, na inaporejeshwa huyo mtu ataeleza kuwa alikuwa nyumbani kwa fulani na atasimulia mambo yote aliyokuwa akifanya, kama ramani yake ilikuwa ni ya uongozi, yule mtu aliyekuwa anaitumia, uwezo wake wa kuongoza hufikia mwisho na atageuka kuwa kama zezeta.
 
Hivi uchawi ndio nini?
Au ni nadharia za chuki tu?
Mbona uchawi hautaji mafanikio kwa wema.
Nikutaja uchawi kwa chuki hata kama mtu amefanikiwa utasikia mchawi huyo!
Mara mwanga huyo!
Mshirikina huyo!
Kama mtu amefanikiwa tatizo liko wapi jaman?
Nipeni ufafanuzi mnanitisha saaaaanaaaa!!!

watu kama nyie lazima mnamiliki fisi na matunguri ndani!!! unajifanya uchawi hujui!!
 
watu kama nyie lazima mnamiliki fisi na matunguri ndani!!! unajifanya uchawi hujui!!

Na watakuwa wamezaliwa na kukulia kwenye uchawi kwani wanafikiria kila mtu anaishi jinsiw anavyoishi wanavyoishi.

Suzy huwezi kujua upo katika msitu mnene kama upo ndani ya msitu kwani miti iliyokaribu nawe inakuzuii kuona mbali, toka nje ya msitu na uuangalie jinsi msitu ulivyo mnene.

Uchawi unasumbua watu sanaaaaaaa katika dunia hii hasa wenye imani haba.
 
Mikoa saba nchini Tanzania ndiyo tishio kwa kuwa na nguvu kubwa za uchawi
1. Tanga ndio kinara
2. Lindi unafuatilia
3. Dar es Salaam
4. Mtwara
5. Tabora
6. Kigoma
7. Mwanza

Mikoa yenye wachawi wengi, kwa maana kwamba karibu kila kaya kuna mchawi
1. Sumbawanga (Rukwa) ndio kinara
2. Ruvuma inafuatialia
3. Mbeya
4. Singida

Mikoa ambayo wananchi wake ndio wateja wakuu wa wachawi
1. Kilimanjaro inaongoza
2. Morogoro inafuatilia
3. Kagera

Wateja wengine wa wachawi
1. Wafanyabiashara
2. Wasanii
3. Kina mama wa nyumbani
4. Wanafunzi wa shule za sekondari hasa wa kidato cha pili.

Kwa watu wenye mawzo yaliokaa kushoto kama yako "kichawi chawi.. kamwe nchi haitoendelea" nafkiri watu kama nyinyi mkiona wale wazee wenye macho ya rangi ya njano mnawashutumu wachawi kumbe ni jaundice maskini... AMKA DUDE!
 
Kwani kuna uongo hapo?
 
LANGO LA KUZIMU LA TABORA

Mji wa Tabora ni moja ya miji ya zamani sana, mji huu ulianzishwa na wafanya biashara wa Kiarabu, na ulikuwa ni kiungo muhimu cha biashara ya watumwa, waliokuwa wanakamatwa kutoka mikoa ya ziwa, Kongo, Burundi na Rwanda, kabila ya kusafirishwa hadi Bagamoyo kisha kuingizwa kwenye majahazi na kusafirishwa hadi soko kuu la watumwa la Zanzibar.

Lango la kuzimu la Tabora liko ndani kabisa ya soko kuu, Mkuu wa lango hili anajulikana kwa jina la Swaheral, akisaidiwa na majini yafuatayo:-

1) Alibadiri ni jini katili sana, likitumwa linaua kifo cha aina yoyote lililotumwa kufanya kwa muda mfupi na kwa usahihi.

2) Anzula ni jini linalowaingia sana vijana wa kike na wa kiume, linawazuia vijana kuoa au kuolewa. Usiku wanaota wanafanya tendo la ndoa na msichana mzuri sana, na huwa wanamaliza hamu wenyewe. Raha anayopata ni zaidi ya anayopata akifanya mapenzi na msichana/mvulana.

3) Maimuna ni jini ambalo huwakamata kina baba wenye ndoa zao, usiku anaota anafanya mapenzi na msichana mzuri sana, kumbe anafanya tendo la ndoa na hili jini, baba anakuwa hana hamu kabisa na mke wake wa ndoa, hali inayosababisha ndoa kuvunjika na kuachana.

4) Makata (Simba au leo) hili jini linawaingia sana wanawake, usiku anaota ndoto anafanya mapenzi na huwa anapata raha kuliko anayoipata akifanya mapenzi na mume wake.

5) Kafurani ni jini linalofanya watu wawe bubu, utakuta mtu alizaliwa mzima kabisa lakini kwenye ujana wake anaanza kupoteza uwezo wa kuongea.

Jini hili pia ndilo linalosababisha watu kupooza, pia linasababisha au linaharibu kabisa nguvu za kiume za akina baba, na kuondoa uwezo wao wa kufanya tendo la ndoa.

6) Kabru jini hili likiingia kwenye ukoo wenu, linaua watu wasiopungua wawili kila mwaka, na vifo vinatokea miezi inayofanana kila mwaka. Kama limeanza kuuwa mwezi wa April basi kila mwaka mwezi huo ukifika ni lazima atakufa mtu.

7) Eziruni hili jini linatumwa kwa njia ya ujumbe. Linaweza kutumwa ndani ya barua na unapoifungua barua jini hili hukuingia na kukumaliza, au hujilaza barabarani eneo unalopita, ukilikanyanga, matatizo yanaanza kwenye mguu na kuenea mwili mzima.

8) Subha hili ni jini la kujiinua na kujiona sana, kuwa hakuna mwingine zaidi yako, pia linafanya mtu anakuwa kichaa au linamfanya mtu ananuka sana, kiasi kuwa unatumia kila aina marashi lakini hayasaidii.

9) Al-Maul hili jini linamfanya mtu anakuwa omba omba sana, kila siku yeye kazi hafanyi ni kuzunguka zunguka kila sehemu akiomba, na kila siku anakuwa ni mtu mwenye matatizo yasiyoisha.

10) Zuhura au Zohar ni jini la fujo, mtu wa namna hiyo ukimkosea yeye anachojua ni kupigana tu kitu kinachoitwa samahani kwake ni mwiko.

11) Araba jini hili linapenda sana harufu ya udi (ubani), unapochomwa ni lazima jini hili lifike eneo la tukio, na linapenda sana kutafuna tafuna vitu, hivyo hutafuna kitu chochote kitakachokuwa nyumbani kwako.
 
Kwani kuna uongo hapo?

i believe in modern science sio uchawi... inamaana wale wazee macho yanayobadilika rangi wewe unafikiri ni wachawi..?!! kwa hali ya umaskini TZ kwa wazee ni rahisi sana Liver kupata defect na kutokufanya kazi vizuri.. matokeo ni jaundice!.... siamini na pinga mauaji ya vikongwe!
 
Ubani huendana sana na ibada za kishirikina, kila jini lina ubani wa aina yake ambao ukichomwa na kusoma dua, jini hilo hutokea, na kama unataka kulituma utatakiwa ulimweshe kwanza damu ya kuku, mbuzi, ng'ombe au ya binadamu ndipo ulitume kwenda kudhuru watu. Ndiyo maana unapokwenda kwa mganga wa kishenzi atakutaka ulete kuku kwanza ndiyo afanye uchawi wake.

Majini yanafanya Wakristo walale usingizi mzito wakati wa adhana, kwani wakati huo ndio wakati yanakwenda kwenye ibada, na ibada za Wakristo zinawazuia kutembea. Pia yanawafanya Wakiristo walale usingizi mzito wakati wa mahubiri, ndiyo maana makanisani watu wengi hulala fofofo kabisa.

mbona hujibu vizuri????

wakatoliki ni washirikina?
kwa sababu kanisani wanachoma ubani...

na majini yanapowazuia watu kusikia kengele ya kanisani je?????
 
i believe in modern science sio uchawi... inamaana wale wazee macho yanayobadilika rangi wewe unafikiri ni wachawi..?!! kwa hali ya umaskini TZ kwa wazee ni rahisi sana Liver kupata defect na kutokufanya kazi vizuri.. matokeo ni jaundice!.... siamini na pinga mauaji ya vikongwe!

Nimeeleza vizuri sana huko juu kuhusu jinsi ilivyo vigumu kumtambua mchawi, mke/mume anaweza kuwa ni mchawi wa kukata na shoka lakini usijue kabisa, jamii inaishia kuwahukumu watu wengine kwa kuangalia umri wa mtu, mabadiliko ya viungo vya mwili kutokana na uzee, ugonjwa au kutoka na mazingira anayoishi.

Je unawezaje kumtambua mchawi unayeishi naye ndani ya nyumba au mfanyakazi mwenzako?
 
i believe in modern science sio uchawi... inamaana wale wazee macho yanayobadilika rangi wewe unafikiri ni wachawi..?!! kwa hali ya umaskini TZ kwa wazee ni rahisi sana Liver kupata defect na kutokufanya kazi vizuri.. matokeo ni jaundice!.... siamini na pinga mauaji ya vikongwe!
Ni kweli kabisa si kweli kuwa watu wenye macho mekundu au defect ya aina yoyote ni wachawi. Lakini katika jamii yetu uchawi upo na wachawi upo, tatizo ni namna gani tunaweza kuwatambua??
 
Back
Top Bottom