MAOMBI YA KUSHINDANA by Senior Pastor Josephat Gwajima.
Sijapata kuona kitabu chenye nguvu za ajabu kama hiki kitabu, nilikuwa Dodoma mwaka juzi nikakutana na Mapadre wakikisoma wakawa wanashuhudia nguvu za hiki kitabu, bahati mbaya nilishindwa kukipata pale Dodoma, nikaangizwa kuwa kinapatikana Kawe katika Kanisa la Ufufuo na Uzima kwenye duka lao la vitabu.
Ndugu kama umepanga nyumba, na mwenye nyumba ni kikagula anza kutafuta chumba kama unataka kukisoma kitabu hiki, kwani ni hakika asubuhi yake atakufukuza ndani ya nyumba yake. Siku nilipoanza kusoma kitabu hiki, nyumba yangu ilipata mitikisiko ya ajabu, kipo chumba sehemu ya dari ilidondoka chini, mtaani alikuwepo mganga wa kienyeji alihama mtaa. Nilishangaa mambo yalivyobadilika mtaani, baadhi ya watu tuliozoeana sana wakawa wananikwepa hata ninapowasalamia hawajibu salamu.
Hiki kitabu huwasha moto wa ajabu kwenye ulimwengu wa Kiroho, ambao wachawi na mashetani wanaumiliki, sasa hivi yale matatizo ya watu wanatembea juu ya paa la nyumba usiku, unakaliwa na wachawi usiku unaamka umechoka vibaya sana asubuhi, magonjwa ya ajabu ajabu yasiyoisha, sasa hivi ni historia nyumbani kwangu.
Hakika MUNGU ni Neno, na neno ni MUNGU.