Biashara ya ukahaba imekithiri Sinza na kusababisha wakazi kuhama nyumba zao

Biashara ya ukahaba imekithiri Sinza na kusababisha wakazi kuhama nyumba zao

Dar es Salaam. Biashara ya ukahaba imevamia kwa kasi baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, na kusababisha kero na adha kubwa katika makazi ya watu, hasa eneo la Sinza kiasi cha kuzifanya baadhi ya familia kuhama nyumba, Mwananchi limebaini.

Wazazi na walezi wanasema hali hiyo pamoja na kelele zinazosababishwa na muziki unaopigwa kwenye baa kubwa vimewasababishia ugumu usizoelezeka wa malezi ya watoto.

Uchunguzi wa Mwananchi umebaini biashara hiyo imekithiri katika mitaa mingi ya Sinza, hasa ile inayozunguka kumbi maarufu za starehe na hoteli kubwa.

Hali hiyo inayomulikwa kwa Sinza, ipo pia maeneo mengine kama Tabata, Ubungo, Kindondoni Buguruni na kwingineko, japokuwa ni kwa viwango tofauti.

Kutokana na hali ilivyo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe hivi karibuni alikutana na watendaji na wenyeviti wa mitaa ili kujadili mambo mbalimbali, likiwemo la biashara hiyo huku akiwataka viongozi wa dini kulikemea suala hilo akisema utamaduni huo si wa Tanzania.

Wakazi wa maeneo husika wanasema mbali na kuwaletea changamoto ya malezi, hali hiyo imewalazimisha kubadili mifumo ya maisha ili kuzilinda familia zao.

“Nimelazimika kuhamia Goba kuwakwepa ‘madada poa’ na kelele za usiku kucha. Jirani na nyumba niliyokuwa naishi na familia yangu kuna gesti wanayotumia hao madada poa. Wanavuta bangi usiku kucha na asubuhi tunapotoka tunakuta kondomu zimetapakaa hadi magetini kwetu.

“Wakati mwingine wateja wao wanapaki magari yao kwenye uzio wa nyumba zetu na kuyatumia kufanya mapenzi badala ya kwenda gesti. Tumeripoti sana polisi hatuoni nafuu yoyote,” anasema Ally Mohamed aliyekuwa akiishi katika nyumba moja, nyuma ya baa ya Meeda, maarufu kama Kitambaa Cheupe.

Anaongeza kuwa “changamoto ya kulea watoto kule ilikuwa kubwa kwa kuwa akirudi saa moja usiku anakuta tayari (madada poa) wamejipanga mtaani, wakiona gari wanajiachia uchi, kumbe mtu unakwenda nyumbani akiwa na watoto.”

Mohamed anasema baadhi ya familia, kama ilivyo kwake, zimehama kuepuka kero na adha za ukahaba pamoja na kelele zinazotoka kwenye kumbi za starehe.
Na wa Mwanayamala, Tandika, Kinondoni, keko nao wamehama? ni watoto gani wanakuwa macho na kuranda barabarani nyakati za usiku, sema tu mwandishi alitaka kumpaisha mkuu wa wilaya ili aonekane anafganya kazi, akakague na na kuongea na wakuu wa Tanesco basi.
 
Nilitembelea rufiji hapo ikwiriri hali ni mbaya sana nikabahatika kufika mloka nako mambo ni fire..hakika huduma hii kabambe imewafikia...ni mwendo wa ulipo wapo.

#MaendeleoHayanaChama
Njoo hadi Kisaki hapa uone Malaya walivyo wengi, mshahara tushapata huku bwawa la Nyerere
 
Wanao paswa kukomesha hiyo hali nao ni wateja wa hao makahaba, nawambieni hali hiyo sio dar tu ni kote nchini, kwa sasa kulea watoto imekuwa ni mtihani mzito makahaba kila mahali, hakuna anayejali.
Hapana tatizo ni kuwepo mazingira wezeshi kama kumbi za starehe ndannk ya makazi ya watu
 
Hii biashara ya Sodoma na Gomola imeshaishinda Dunia.

Cha kufanya Serikali iwajengee nyumba flats wasajiliwe wapewe number walipe kodi - ili wateja waende sehemu moja kwa uhuru - watoke huku katika makazi yetu, ni aibu unapita na mama mkwe au na watoto unakutana na kituko kimevaa chupi tu ziwa nje mapema saa moja na nusu ucku.
 
Hii biashara ya Sodoma na Gomola imeshaishinda Dunia.

Cha kufanya Serikali iwajengee nyumba flats wasajiliwe wapewe number walipe kodi - ili wateja waende sehemu moja kwa uhuru - watoke huku katika makazi yetu, ni aibu unapita na mama mkwe au na watoto unakutana na kituko kimevaa chupi tu ziwa nje mapema saa moja na nusu ucku.
Hahahaha Pole sana mkuu. Hama huko
 
Back
Top Bottom