biashara nzuri sana mkuu. Nunua Tvs King 7.2M hizi ndo imara na zinadumu weka msimamizi ye ndo atafute madereva atakao wamudu upigee pesaa yakoo mkuu. Uzuri wa bajaji unapiga iwe ni nje ya mji au mjini kati. kwa mwanza hesabu ni Tsh elfu ishirini
Uzuri wa bajaji.
- Gharama nafuu za uendeshaji
- Devera anajilipa mwenyewe cha msingi hesabu yako ikamilike
- Kodi Tsh Laki moja na nusu kwa mwaka
- Spare bei nafuu
Fanya yafuatayo
Ndgu wadau mimi n mkaz wa jiji la Mwanza ktk hali ya kutaka kujikwamua kiuchumi nimedhamiria kuanza biashara ya kusafirisha abiria kwa usafiri wa bajaji. Kwa hali hiyo kwa wenye uzoefu naomba msaada wa mambo yafuatayo;
1. Naomba kufahamu bei halisi ya kununua bajaji mpya.
2. Tahadhar muhimu za kuchukua/kuzngatia pindi naponunua bajaji mpya
3. Naomba kufahamu taratibu muhimu za kufuata kabla ya kuanza biashara hii.
4. Changamoto za biashara hii.
5. Ushaur juu ya mahali panapolipa zaid kwa wenye uzoefu na mazingira ya jiji la Mwanza
6. Ushaur kuhusu mengineyo.....
Natanguliza shukran zangu kwa wote mtakao amua kutumia muda wenu kunisaidia kimawazo ktk harakat zangu hizi.
Fanya yafuatayo na utaipenda biashara ya bajaji ila mimi nipo Dar
Bei halisi ya bajaji ni 7mil
Insuarence, sumatra na mambo mengine mpaka bajaji inaingia barabarani laki 4
Sasa cha kufanya ni kutafuta dereva mzuri na mwenye mke na mtoto/ watoto ambaye anajua umuhimu wa kazi na familia. Huu ni uangalizo tu, unaweza kupata dereva bachelor na akawa mchapaka kazi
Total hapo juu ni 7.4 mil
Ingia na huyo dereva mkataba unaosema akifikisha mara 2 ya hiyo fedha ambayo ni 14.8 mil, bajaji inakuwa ya kwake. Hutahusika na kitu chochote, awe anakuletea hesabu ya 150,000 kwa wiki
Less na 2 yrs atakuwa keshakuletea hiyo 14.8mil, tena madereva wengine watakuwa wanakuletea zaidi ya hiyo hesabu ili amalize deni mapema.
Ukishafikisha 7.4mil unaenda kununua bajaji nyingine au huyo dereva akimaliza mkataba wake unamnunulia nyingine mkataba unaanza upya, ile bajaji ya zamani anampa dereva wa kwake anakuwa anamletea hesabu dereva wako au option 2 anaiuza anaanza kazi na hiyo mpya.
Dereva akishajua mwisho wa siku chombo kinakuja kuwa chake anakitunza.
Hizi ndio tunavyofanya Dar.