Biashara ya Usafirishaji kwa Bajaji: Ueandeshaji, Changamoto, Faida na Ushauri

Biashara ya Usafirishaji kwa Bajaji: Ueandeshaji, Changamoto, Faida na Ushauri

biashara nzuri sana mkuu. Nunua Tvs King 7.2M hizi ndo imara na zinadumu weka msimamizi ye ndo atafute madereva atakao wamudu upigee pesaa yakoo mkuu. Uzuri wa bajaji unapiga iwe ni nje ya mji au mjini kati. kwa mwanza hesabu ni Tsh elfu ishirini

Uzuri wa bajaji.
  • Gharama nafuu za uendeshaji
  • Devera anajilipa mwenyewe cha msingi hesabu yako ikamilike
  • Kodi Tsh Laki moja na nusu kwa mwaka
  • Spare bei nafuu

Fanya yafuatayo
Ndgu wadau mimi n mkaz wa jiji la Mwanza ktk hali ya kutaka kujikwamua kiuchumi nimedhamiria kuanza biashara ya kusafirisha abiria kwa usafiri wa bajaji. Kwa hali hiyo kwa wenye uzoefu naomba msaada wa mambo yafuatayo;
1. Naomba kufahamu bei halisi ya kununua bajaji mpya.
2. Tahadhar muhimu za kuchukua/kuzngatia pindi naponunua bajaji mpya
3. Naomba kufahamu taratibu muhimu za kufuata kabla ya kuanza biashara hii.
4. Changamoto za biashara hii.
5. Ushaur juu ya mahali panapolipa zaid kwa wenye uzoefu na mazingira ya jiji la Mwanza
6. Ushaur kuhusu mengineyo.....

Natanguliza shukran zangu kwa wote mtakao amua kutumia muda wenu kunisaidia kimawazo ktk harakat zangu hizi.

Fanya yafuatayo na utaipenda biashara ya bajaji ila mimi nipo Dar

Bei halisi ya bajaji ni 7mil
Insuarence, sumatra na mambo mengine mpaka bajaji inaingia barabarani laki 4

Sasa cha kufanya ni kutafuta dereva mzuri na mwenye mke na mtoto/ watoto ambaye anajua umuhimu wa kazi na familia. Huu ni uangalizo tu, unaweza kupata dereva bachelor na akawa mchapaka kazi

Total hapo juu ni 7.4 mil
Ingia na huyo dereva mkataba unaosema akifikisha mara 2 ya hiyo fedha ambayo ni 14.8 mil, bajaji inakuwa ya kwake. Hutahusika na kitu chochote, awe anakuletea hesabu ya 150,000 kwa wiki

Less na 2 yrs atakuwa keshakuletea hiyo 14.8mil, tena madereva wengine watakuwa wanakuletea zaidi ya hiyo hesabu ili amalize deni mapema.

Ukishafikisha 7.4mil unaenda kununua bajaji nyingine au huyo dereva akimaliza mkataba wake unamnunulia nyingine mkataba unaanza upya, ile bajaji ya zamani anampa dereva wa kwake anakuwa anamletea hesabu dereva wako au option 2 anaiuza anaanza kazi na hiyo mpya.

Dereva akishajua mwisho wa siku chombo kinakuja kuwa chake anakitunza.

Hizi ndio tunavyofanya Dar.
 
Wanajamii wenzangu,nimeoa wazo la kununua bajaj 3 kwa mkupuo nifanye biashara ambayo kwa siku nitakua naingiza kiasi cha shilingi elfu 60.
Tafadhali kabla ya kununua naomba mnipe mawazo yenu je biashara sahihi au nibadilishi biashara?nawekeza kiasi cha milioni 15

Ni sahihi sana cha msingi ni usimamizi uwe mzuri tu........
 
ni wazo zuri , lakini upate kingTVs ndo imara na bei imesimamia 7.1m kama sikosei hyo 15m hatatosha bajaji 3 . pia usimamizi madereva wanatakiwa waaminifu na wenye kujielewa vinginevyo ni tarajia maumivu makali. bado vipuri bajaji ikianza kuchoka baada ya miaka 2 so jipange kwa yote
 
Mr. Unalizungumzia vipi swala la kununua bajaj kwa mtu(second hand) kwa lengo la kufanyia biashara.
Wakuu naomba mwenye jibu la swali hili atusaidie na mimi nataka kununua bajaj used je pesa yangu inaweza kutoka na faida.
 
Hello wakuu,
Mwenye uzoefu na biashara ya bajaji tupeane uzoefu please.
 
Nina uzoefu wa daladala, Uber, na Boda Boda, Bajaj ni Kidogo kiasi, lakini biashara ya Usafiri inataka kuwa katili saäana. Ni hilo tu.
 
Ukitaka kutoa bajaji kwa dereva kwa mkataba inachukua muda gani mpaka iwe yake na kwa siku analeta sh ngapi?
Nina uzoefu wa daladala, Uber, na Boda Boda, Bajaj ni Kidogo kiasi, lakini biashara ya Usafiri inataka kuwa katili saäana. Ni hilo tu
 
Ukitaka kutoa bajaji kwa dereva kwa mkataba inachukua muda gani mpaka iwe yake na kwa siku analeta sh ngapi?

Tangia anapoanza kuiendesha/drive au kuifanyia kazi...automatically inakuwa ni yake

hadi siku anapomaliza mkataba na kukabidhiwa kadi original ya bajaji yake.!

Muda wa mkataba ni pale anapokamilisha hesabu yote.Yaweza kuwa miezi 6 hadi 8

*na iwe mpyaa
 
Uaminifu mhimu. Uzuri wa mkataba, bili zote kwake ila inabidi alete kwako kila wiki au utakavyoamua. Usipokee pesa. Mpe account yako wewe upate risit itawasaidia wote wawili. Kila wiki akiweka let say 120,000/ ni sawa na anakuletea risit. Akitaka kuweka zaidi poa.

Kama mmepatana millioni nane au saba mtajua wenyewe ila ahakikishe anaweka kwenye account. Usishike pesa ni balaa. Nina uzoefu wa hiyo kitu nilianza na hao wa kuleta kila siku ikawa nongwa ndo nikaingia mkataba. It pays. Kumbuka kuna TRA na maegesho yanahitaji malipo.
 
TRA na maegesho ni kwangu au dereva?natoa ya mkataba

Tra ni kwako sababu bado ipo kwenye jina lako. Maegesho ni kwa dreva. Kama una gate mpe masharti ya kuwa anapark kwako na anaoshea kwako then mnakatana.
 
Thank you
Tra ni kwako sababu bado ipo kwenye jina lako. Maegesho ni kwa dreva. Kama una gate mpe masharti ya kuwa anapark kwako na anaoshea kwako then mnakatana.
 
Na hizo charges za TRA zkoje?amount na kwa mda gani?

Hujaelezea sababu kuu ya kuweka kwenyw account ni nn? Kwann isiwe cash in hand?
 
Na hizo charges za TRA zkoje?amount na kwa mda gani?
[Nikikueleza kwa sasa nakudanganya sababu ya kwangu nilimaliza naye 17 na baada ya hapo nikasema sitaki bajaj kamwe. Bajaj inahitaji mtu aliyetulia. Ukiniambia upo maeneo gani nitakupa contact za watu ninaowaamini. Mimi nipo Masaki hivyo unijulishe upo wapi ili nikwambie contact.
 
Duh huko hata sijui ramani yake. Mimi nipo Masaki Oyster bay na bajaj yangu inapark Africana Dar hivyo tofauti. Lakini umepata idea how to run it. Usifuatilie sana utakuwa kichaa na umpe mtu unayemwamini. Mpe account yako utakachojali ni mrejesho na limit ya muda mliowekeana kumaliza mkataba.
 
Back
Top Bottom