Biashara ya Vanilla, Tshs 850,000 kwa kilo; Kuna nini nyuma ya tangazo hili?

Biashara ya Vanilla, Tshs 850,000 kwa kilo; Kuna nini nyuma ya tangazo hili?

Sana tu,
Mi nadhani Kuna rushwa huwa inatembea, au Ni miradi yao ya utakatishaji
Dah!!!,Sasa Mbona kuna wakubwa wanawakeza sasa humo?,kwa hiyo na wao wanaliwa.Mfano kule Kijiji Cha Vanilla akina Prof.Juma Kapuya wamewekeza, Joyce Mhaville mkurugenzi wa ITV na Radio one naye ana plot kule,na wengine.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Utata upo hapa kwanini wakati wanaendelea kulima ili kupunguza cost zaidi wasinunue zilizopo na kuuzia hilo soko lao ? Kama wanao uwezo wa wao kununua kwa milioni moja kwanini wasinunue kwa bei pungufu huko Bukoba wakati wanasubiri ?

Mkuu kwahio ukimuona fulani anafanya kitu wewe utafanya sababu fulani na yeye kafanya ?, Sidhani kama a Sound investment ukiulizwa kwanini umefanya itakuwa na fulani kafanya... Hata kama hao jamaa wana soko leo, Je watakuwa na soko three years down the line ? In short hakuna mtu wa ku-predict bei ya kitu miaka mitatu ijayo with accuracy kufanya hivyo ni speculations
Mkuu inawezekana mkurugenzi wa vanilla village-Njombe ameingia mkataba na wanunuzi,kwa hiyo usiwe mwepesi kuweka prediction.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Issue yangu ndio inakuja hapo..., hivi kweli kwa sasa huko Bukoba n.k. huwezi kupata Vanilla mbichi chini ya 150K? kama ndio unaweza kwanini wakati unasubiri usichukue hizo Vanilla kwa hao wadau na kupeleka huko kwenye soko lako la 150K kwa Kg?

Issue yangu hapa ni pricing, huenda hao wakakupa prices nzuri zaidi kulingana na longterm investment yako n.k. ila sio necessarily bei ya soko ikawa hi

Kwani kuwa soko la hisa ndiyo kufanikiwa? TOL na Precision ziko listed DSE kwa miaka zaidi ya 20 lakini shareholders wake hawajawahi kukinga hata Tsh 100.
LAKINI WAPO DSE, how they perform hiyo ni ya kwao; hivyo usikariri kuwa kwa sababu ya your negativity kwa JATU au hao wengine basi WATASHINDWA, NO!
 
Mbona unatumia nguvu kubwa mno aisee
emoji1.png
Inapokuja kwenye FACTS na UKWELI hamna njia nyingine ya kuwaeleza watu wenye MIOYO MIGUMU na MIZITO kamaH
Hao wawekezaji wako wanatofauti gani na yule Mr. Kuku wa kigamboni?

Maana nae approach yake ilkua Ni hii hii a watu walikuja kulia baadae

Wewe CHIEF MASALAKULANGWA, I bet ni mmoja wapo wa wasanii wa hiyo Vanilla International, si kwa kuumiza kichwa huko kutetea wizi wa mchana
 
LAKINI WAPO DSE, how they perform hiyo ni ya kwao; hivyo usikariri kuwa kwa sababu ya your negativity kwa JATU au hao wengine basi WATASHINDWA, NO!
Kuwapo DSE does not mean people don't cook their books...., ENRON walikuwa Wall Street lakini haikuwazuia to cook their books..

Cha maana ni kuangalia issues on offer if they make economical sense, na watu kuuliza maswali ni katika kuhakikisha if they indeed do make sense...
 
Ujumbe wa DC Njombe kissagwakisakasongwa kuhusu VanillaNjombe

Serikali bado inafanyia kazi maswali mengi yaliyopo katika jamii kutokana na matangazo kwamba Vanilla inalipa na bei ya manunuzi ya Vanilla kwa kilo zinazotajwa kuwa ni kubwa sana. Naomba wananchi tuwe watulivu wakati Serikali Inaendelea kufuatilia jambo hii kwa Kina. Aidha kwa wale ambao tayari wamewekeza waweze kufika kwa RPC wa Mkoa wa Njombe kama ambayo Mheshimiwa RC ameagiza ili kujihakiki majina yao.

Nitoe wito kwa wananchi ambao wanakusudia kuwekeza kusubiri kwanza kuendelea na uwekezaji huu uliopo hadi pale serikali itakapojiridhisha ili kuepusha migogoro au sintofahamu ya aina yoyote inayoweza kujitokeza kwa wananchi.

Kazi inaendelea
Picha zinaelezea ziara ya leo nilipoongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwenda kufanya ukaguzi wa eneo maarufu lililowekezwa Vanilla wilayani
 
Nisiwachoshe bure nitaandika kifupi sana. Kuna tangazo limepata airtime kubwa kwenye ITV kuhusu Vanilla International inayo promote kilimo cha vanilla wilayani Njombe. Bottom line ni bei ya soko ya kilo moja kuwa ni Tsh 850,000.

Wasiwasi wangu:
1. Kama faida ni kubwa hivyo kwa nini wasilime wenyewe kwa vile wanajuwa soko lilipo?

2. Ile methali ya kizuri chajiuza, na kibaya chajitembeza, je ina apply hapa?

3. Kuna watu wanalima vanilla Mkoa wa Kagera wanadai kuwa hata mteja wa kumuuzia kilo moja kwa Tsh 50,000 hawampati.

4. Kwa nini wanatangaza "faida" tu mfano bei nzuri na hawatangazi "changamoto" zinazoendana na biashara hii?

5. Naiona kama DESI watu wanaweza kupigwa hela hapa.

Wajuzi tufahamisheni
Tumekuwa hodari kuandika bila kutafiti,cha kushangaza hata hapa naona siasa,mi siko njombe hila najua vanilla inalipa,nenda tu ZANZIBAR mwezi may mpaka june soko la viungo utakutana na wageni toka Ulaya wakinunua vanilla kavu kilo moja mpka laki 8 mpaka 9,Acha hiyo google soko la vanilla Duniani ujue bei yake utakuja kubadirisha mada.Mwisho Tanzania tuna shida ya utafiti kila kitu tunahisi kuibiwa hata hii teknolojia ya mtandao tumeshindwa kujielumisha tukajua,Kilimo kwetu ni mamamkwe NDO maana chinga ni mamilioni ya watu.TUBADILIKE

Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app
 
Bukoba kuna watu wamelima vanilla hawana hata mtu wa kumuuzia Tsh 50,000 kwa kilo.

Ila Arista naomba unijibu swali hili; Kama vanilla Ina faida kubwa hivyo, kwa nini hao wenyewe akina Mkondya wasilime?

Yaani upate mgodi wa dhahabu halafu utangaze redioni?
 
Ukiona zao linatangazwa sana kwa bei ya manunuzi na materials zote wanatoa wao basi ogopa kama ukoma

Watu walifugishwa kwale kwamba mayai yake watanunua kwa pesa ndefu, watu kwa gharama kubwa sana
Kuanzia vifaranga
Chakula
Madawa
Mabanda nk

Kwale walipo anza kutaga jamaa wakasepa zao
 
Sijui nani anatakiwa kusikia hili lakini hichi ndicho ninachojua juu ya soko la zao la vanilla.

Bado bei ya zao hili ni ndogo sana kulingana na watu wanavyolipaisha; japo ni zao moja wapo lenye bei nzuri kulingana na mazao mengine nchini.

Watu huchanganya bei za zao(fresh vanilla beans) na bei ya ule mchuzi wa vanilla baada ya kuchakatwa. Bei za vanilla beans ni za chini sana huku bei za mchuzi wa vanilla zikiwa juu sana.

Vanilla beans huwa na grades tofauti lakini kiwango kizuri ni kile chenye urefu wa +16cm sasa hapa kwa kg 1 inategemea na bei za nchi husika pamoja na hali ya uchumi. Ukikuta ina harufu nzuri(aroma) bei huongezeka zaidi. Wakulima wengi wanashindwa kuilea mimea ya vanilla hivyo hupata viwango vya kawaida hususani Tanzania na Uganda pia.

Hayo ni baadhi niyajuayo kuhusiana na zao hili. Natamani niandike yote ila mpaka hapo baadae karibu kwa nyongeza.
 
Hawa jamaa wa Njombe Vanilla International, hawaongei kama unavyofafanua wewe. Wala hawajagusa changamoto hata moja inayohusiana na kilimo hiki. Ndiyo maana tunahisi ni MATAPELI
 
Back
Top Bottom