Biashara ya Vanilla, Tshs 850,000 kwa kilo; Kuna nini nyuma ya tangazo hili?

Biashara ya Vanilla, Tshs 850,000 kwa kilo; Kuna nini nyuma ya tangazo hili?

Leo hao JATU wako Soko la Hisa la Dar-es-Salaam (DSE), wewe baki na mawazo yako negative kwenye kila kitu chenye kuzalisha pesa ambayo akili yako imeshindwa kuielewa!
Kuwepo Soko la HISA haimaanishi kitu ni genuine ni jukumu la muwekezaji kufanya duel dillegence..., Hata kina ENRON, walikuwa kwenye Stock Exchange za Ulimwengu achana na DSE; Ila mwisho wa siku they were cooking books...

Na hata wewe ukipata haimaanishi kitu ni sustainable unaweza wewe ukapata wengine wakalia..., cha maana kwa mwekezaji ni kujua inside out ya kitu kabla hajawekeza..., na kwa muuliza maswali kuuliza ndio njia ya kujua ukweli..., na kwa mwenye Kampuni dawa ni kujibu maswali yote pasipo shaka wala sio kukasirika
 
Leo hao JATU wako Soko la Hisa la Dar-es-Salaam (DSE), wewe baki na mawazo yako negative kwenye kila kitu chenye kuzalisha pesa ambayo akili yako imeshindwa kuielewa!
Kwani kuwa soko la hisa ndiyo kufanikiwa? TOL na Precision ziko listed DSE kwa miaka zaidi ya 20 lakini shareholders wake hawajawahi kukinga hata Tsh 100.
 
Issue yangu ndio inakuja hapo..., hivi kweli kwa sasa huko Bukoba n.k. huwezi kupata Vanilla mbichi chini ya 150K? kama ndio unaweza kwanini wakati unasubiri usichukue hizo Vanilla kwa hao wadau na kupeleka huko kwenye soko lako la 150K kwa Kg?

Issue yangu hapa ni pricing, huenda hao wakakupa prices nzuri zaidi kulingana na longterm investment yako n.k. ila sio necessarily bei ya soko ikawa hio
Akikujibu hili unishtue
 
inachukua miaka mitatu kuanza kutoa matunda, ikivunwa kuanika Ni kila siku kwa muda wa miezi sita[emoji706][emoji706]
Ha ha ......
Hiki Ni kilimo kichaa.
JamiiForums-152468582.jpg
 
Bei ya Vanilla iliyokaushwa sio hiyo ni zaidi ya Milioni moja, wakati Vanilla mbichi ni Laki moja kwa kilo.Mimi nimefika hadi kwenye hicho Kijiji Cha Vanilla.Ishu ilivyo ni kwamba wale jamaa wao wanadai kuwa Wana Soko la kuuzia Vanilla lkn hawana Uwezo wa kifedha kuzalisha vanilla ya kukidhi mahitaji ya Soko.Km una mtaji nakushauri nenda kachukue ploti kule utakuja kunishukuru.Mimi nimeenda nikawahoji maswali yote niliyokuwa nayo akilini mwangu wakanijibu bila shida.Kule kuna plot za Akina Joyce Mhaville mkurugenzi wa ITV na Radio one,Prof.Juma Athuman Kapuya,na wengineo.
Usipotoshe wana jf
 
Sawa huo unaitwa ULANGUZI au UDALALI na kwenye biashara inaruhusiwa ILA inategemea na SOKO LAKO! Masoko mengine wanataka aidha ORGANIC or NON - ORGANIC products or produces na kwa wingi fulani na kwa muda fulani. Katika hali hiyo na masharti hayo, kwa nini, kama unaweza usiingie shambani tu, ukalima kwa njia yoyote ile ikiwa ni pamoja na hiyo ya kukaribisha "wana hisa au wawekezaji binafsi" kwa masharti ya WIN-WIN SCENARIO? Inaonekan huu ni utaratibu mpya wa uwekezaji unao ingia sasa nchini mwetu, in fact mchana huu nilkuwa nazungumza na wafuga samaki kwenye vizimba huko Mwanza nao wanatumia utaratibu huu, na hii ni baada ya kumuona Mzee Mecki Sadiki (former RC wetu hapa Dar-es-Salaam) akilielezea hili kwenye TV moja na likanivutia sana.

Hawa wa samaki, kama wa Vanilla, nao wanakaribisha "wawekezaji/wana hisa"; wanakujengea kizimba chenye ukubwa wa aidha mita tano kwa mita tano (5m by 5m) au mita sita kwa sita kwa shilingi MILIONI NNE (4milioni)! Hapa ndio penye utata, pesa ndio taabu na ndio msingi wa watu kuanza kusema DECI HAO! Milioni nne si hela fupi ILA wao wanafanya kila kitu, namaanisha KILA KITU! Ikiwa ni pamoja na kukuwekea samaki au mbegu 10,000, hawa wakikua na ukivuna utapata kilo 5000 na kwa bei ya sasa hapo Mwanza ni shilingi 5000/= kwa kilo na kwa Dar-es-Salaam ni shilingi 8000/= hadi 10000/= kwa kilo! Piga hesabu hiyo ya kuzidisha na kisha ULIE NA KUPAYUKA DECI hao!
Mbona unatumia nguvu kubwa mno aisee[emoji1]
 
Bei ya Vanilla iliyokaushwa sio hiyo ni zaidi ya Milioni moja, wakati Vanilla mbichi ni Laki moja kwa kilo.Mimi nimefika hadi kwenye hicho Kijiji Cha Vanilla.Ishu ilivyo ni kwamba wale jamaa wao wanadai kuwa Wana Soko la kuuzia Vanilla lkn hawana Uwezo wa kifedha kuzalisha vanilla ya kukidhi mahitaji ya Soko.
Utata upo hapa kwanini wakati wanaendelea kulima ili kupunguza cost zaidi wasinunue zilizopo na kuuzia hilo soko lao ? Kama wanao uwezo wa wao kununua kwa milioni moja kwanini wasinunue kwa bei pungufu huko Bukoba wakati wanasubiri ?
Km una mtaji nakushauri nenda kachukue ploti kule utakuja kunishukuru.Mimi nimeenda nikawahoji maswali yote niliyokuwa nayo akilini mwangu wakanijibu bila shida.Kule kuna plot za Akina Joyce Mhaville mkurugenzi wa ITV na Radio one,Prof.Juma Athuman Kapuya,na wengineo.
Mkuu kwahio ukimuona fulani anafanya kitu wewe utafanya sababu fulani na yeye kafanya ?, Sidhani kama a Sound investment ukiulizwa kwanini umefanya itakuwa na fulani kafanya... Hata kama hao jamaa wana soko leo, Je watakuwa na soko three years down the line ? In short hakuna mtu wa ku-predict bei ya kitu miaka mitatu ijayo with accuracy kufanya hivyo ni speculations
 
Tatizo ni lile lile tu, watu wanaogopa kuchukua risks kwanza kwa vile ni utaratibu mpya wa biashara na uwekezaji (tukikubaliana kuuita hivyo) na pili ni kwa sababu ya kiasi "kikubwa" cha fedha za kuwekeza na tatu ni juu ya "mapesa meeeengi" unayo ambiwa utapata baada ya "mavuno" aidha ya vanilla au mahindi au samaki! Akili ya non risk taker haielewi wala haikubaliani na the concept na matokeo yake. Hili ndio tatizo na chanzo cha wasiwasi na kuishia kwenye name - calling. Yote haya yanasindikizwa na umaskini wa kipato kwa jamii yetu kiasi cha kufanya haya yote - uwekezaji huu na matokeo yake - kuwa njozi na ndoto za mchana kama siyo za Alinacha! Na kuishia kutoa majibu mepesi ya DECI au Matapeli!
Hao wawekezaji wako wanatofauti gani na yule Mr. Kuku wa kigamboni?

Maana nae approach yake ilkua Ni hii hii a watu walikuja kulia baadae
 
Hakuna kuchoshana hapa kwani hakuna aliyeitwa au kulazimishwa kuchangia kwenye hili, ila ni suala la kujaribu kuangalia facts kama zilivyo kwenye suala hili. Kama kuna watu kule Songea walilizwa na huyu Simon Mkondya then hilo ni tatizo lao na wanao wajibu wakujipambania aidha kisheria au kivingine ili wapate haki yao. Suala la kupata mkopo Benki ni hoja nyingine ambayo hapa siyo mahali pake kwa sasa ila hilo nalo siyo rahisi kama usemavyo, mbona wenye viwanda wana tafuta wana hisa, kwa kuuza hisa huko DSE, kwa nini wasiandke hizo proposals na wakope Benki?
Kwanini na nyie msiende huko DSE mkakusanye mitaji?

Mnapaogopa nini huko?
 
Back
Top Bottom