Mkuu kinachouzwa na kinachofanyika sicho kinachosemwa..., Huu mfumo ulikuwepo kwenye Sungura kuuziwa mbegu, mabanda na chakula cha Sungura ili wakizaliwa utafutiwe soko kwa Tshs elfu 30 kila sungura...
Kwa mwenye mfumo business model yake ni kuuza chakula, mabanda na hizo mbegu za Sungura with Zero Risk hata akinunua kwa elfu 30 anakuwa ame-offset , cost nyingine zote with zero risk... Sababu kama product (Sungura) wangekuwa na soko kweli la elfu 30 kwa kilo, asingekataa watu wa vijijini ambao wangeweza kupata na kuwauzia Sungura hao kwa elfu 10...
Kwa hao wa Kuku na Samaki pia hio ndio business model yao, ingawa hao sidhani kama watakataa mtu ambaye hawakumuuzia mbegu kuwauzia hao kuku na samaki kama bei ipo accordingly, watu wakianza kuchagua wanunuzi hapo jiulize kwamba huenda the soko sio kubwa kama wanavyodai..
Sasa hawa wa Vanilla wanauza nini ? Kununua Kilo Moja ya Vanilla Miaka kadhaa ijayo kwa Bei waliyosema ?, Kama ndio basi hapa biashara sio Vanilla per se.., bali ni pesa wanazopata leo kwa ku-offset kwamba miaka kadhaa ijayo hata wakinunua kwa hio Bei huenda bado waka-break even (At Best) at worse ni everything kwenda Pear Shaped na wao na wanahisa wote kwenda belly up (sisemi watu wafanye au wasifanye, bali ni Busara kujua the ins and outs ya kipi mtu anaingia)..., Sababu kama wangekuwa na masoko ya kutosha kwa bei hio ya sasa, hakuna cha kuwazuia kununua kwa watu na kuuza