Biashara ya viatu nyoko sana mi nilinunua kiatu kwa chinga alianzia elfu 25 nilikua sitaki tu kununha ila ningekua na hela ningempa...akanikazia nikaishia kumpa elfu 10 nikaona nimempiga.Siku nimeenda karume kwa ishu zingine nikakuta wanafungua mabelo kucheki mzee vinauzwa elfu tatu hadi elfu tano top.
Na kiatu hichohicho ukienda makumbusho wanauza elfu 30 kudadadeki msiwadharau machinga watembeza viatu wanapiga hela mazee imagine elfu 10 mtaji pair 3 na ukiuza kwa haraka ndo unalamba elfu 30 , japo vingi wanaanzia bei ya juu akiuza elfu 10 unaona umempiga.
Sijui graduates tunafeli wapi mitaji inaishia kwenye simu na bundle insta afu tunasubiria ajira for f**ng 5 years in vain