Biashara ya viatu inaweza kukutajirisha

Biashara ya viatu inaweza kukutajirisha

Wakuu habarini? nimefikiria kufanya biashara ya sandals, kwawenye uzoefu nabiashara hii naombeni ushauri juu yamtaji ninaoweza kuanzanao pia kwakuchukulia bidhaa na range yabeizake mimi nipo lindi.... Natanguliza shukran.
 
Dah, nimesoma comments zote kuanzia mwanzo hadi mwisho na kujikuta nakuwa inspired na biashara ya viatu. Kuanzia wiki ijayo nitaanza kufanya research kuanzia wanakonunua viatu hadi kwenye soko (pa kuuzia) ili nione nafanyeje. Asante sana innocentkirumbuyo kwa kuanzisha uzi huu...
Pamoja sana chief nakutakia mamuzi mema kwenye safari yako ya mafanikio
 
Wakuu habarini? nimefikiria kufanya biashara ya sandals, kwawenye uzoefu nabiashara hii naombeni ushauri juu yamtaji ninaoweza kuanzanao pia kwakuchukulia bidhaa na range yabeizake mimi nipo lindi.... Natanguliza shukran.
Unataka kuuza sandals gani boss mtumba au shop
 
Zaduka mkuu, tatizo nimeshindwa ku upload picha
Ok sasa sandals za duka zipo aina tatu kuna quality kuna ya kati na yakawaida tu


viatuvyakiumebeipoa_20200728_093438_0.jpg
 
Ukitaka upate pesa ata kwa mtaji mdogo chukua hizo aina mbili za hapo chini
 
Hello

Natumaini mnaendelea vyema na harakati za kutafuta maisha nimeona leo niwaibie siri jinsi hii biashara ya sandals na viatu inaweza kukutajirisha kwa haraka.

Historia
Mimi kwa majina ya kuzaliwa naitwa Innocent kirumbuyo nimezaliwa Kilimanjaro katika hospital marubeneti miaka mingi iliyopita huko nyuma.

Mwaka 2012 nilimaliza elimu yangu ya sekondari katika shule ya sekondari Siha

Baada ya kumaliza elimu yangu ya sekondari nilingia mtaani kutafuta maisha ndipo nilipo jisogeza paka kwenye jiji la miamba Mwanza alimaarufu rock City

Nilipofika tu Mwanza nilianza na biashara ya kuuza viatu vya kike simple zile bei ndogo nilifanya ile biashara kwa kipindi cha miezi miwili tu.

Nikabadili biashara na kuanza kuuza simu za mkononi nilifanya biashara ya simu kwa mwaka moja tu

Kwa mara nyingine tena nikabadili tena biashara nakuanza kuuza viatu na sandals biashara ya viatu na sandals ndio ninafanya paka muda huu ni biashara nzuri sana ambayo ukiwa nayo makini unaweza kutajirika na kusahau umasikini kabisa

Unajua kwanini nakuambia hivyo hii biashara nimeifanya kwa miaka 7 ni biashara nzuri sana naitambua vizuri

Inachangamoto ila siyo kubwa sana kama za biashara nyingine ambazo nimefanya.

Uzuri hii biashara cha kwanza kuna faida kubwa sana na inamzunguko mkubwa sana

Unaweza kupata paka 60 elfu kwa katoni moja tu ata zaidi na hii katoni moja unaweza kuuza kwa siku au wiki inategemea sana mzunguko wako.

Karibu kwenye biashara ya viatu.

Tunakaribisha maswali maoni nipo hapa kutolea kila kitu ufafanuzi kwa kadiri navyoelewa.

View attachment 1582249View attachment 1582304View attachment 1582302View attachment 1582303

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Merry Bennety sio merubenet. Sambarai moja hiyo.
 
Nipe muongozo wa mtaji wa 100K kariakoo.
Kwa mtaji wa laki moja nakushauri uwekeze kwenye viatu vya mtumba huko ndio rahisi kupata faida ni vinatumia mtaji mdogo nenda karume kaperembe buti zako kali kisha piga maji kinachobaki ni wewe kutega tu kumbuka location bora ya kuuzia ni muhimu sana
 
Back
Top Bottom