Biashara ya Vifaa vya Ujenzi (Hardware Store): Ushauri wa Mtaji, Uendeshaji, Changamoto na Faida

Ushauri mzuri, Nashukuru sana
 
Safi sana ushauri mzuri sana. Hata mimi natamani kuwa na biashara kama hiyo.
 
Habar wapendwa wa JF

Naomba kujua ABC za biashara ya kuuza tofali hizi za mchanganyiko wa cement na mchanga

Mim naona fursa hii huku kwetu maeneo ya Kilema-moshi-kilimanjaro ila cjafahamu jinsi ya hii biashara inavyoendeshwa

Naomba kufahamishwa chochote kwenye hii biashar;
Huku kwetu mchanga ni 180000 Lorry
Cement 15000 @ bag

Moramu wa kuchanganya ili tofali iwe strong 60000@lorry

Ahsante kwa ushauri wenu
 
Ngoja wadau waje
nikajua nawewe utamoa ushauri kidogo mkuu.....ila biashara ya kuuza tofali inaugumu fulani

kwanza ni ya msimu kuna kipindi mvua zinaoiga kiasi kwamba mzigo hautoki kabisa, pia hali ya uchumi ikiwa ngumu, mzigo pia hutoka kwa hasara au usitoke kwa urahisi

Pia kujuana kwingi sana, kiasi kwamba utahitaji connection, mfano kuna wanaofanya hii biashara kwa mwaka wa 9 au 5, so anakuwa na wateja permanent, changamoto hii namshauri ajitahidi sana kutembea site za ujenzi, anaongea na mafundi kuwa kwa kila mteja atakaeletwa basi fundi anapesa kiasi fulani (ni makubaliano yenu tu).....

Maana fundi anaweza mshauri boss akachukue tofali za fulani maana zinaquality nzuri, sema hii biashara ukiwa na tipa itakufaidisha zaidi maana unatafuta wateja na kupeleka mzigo mwenyewe....
 
Oh ushauri mzuri[emoji1666]
 
Sehemu Nyingine Trip Ya Mchanga Tshs 50000
 
Ahsante mkuu,
Vp kuhusu faida
Yan
Mfuko mmoja wa cement unatoa tofali ngap?
Tipa moja ya mchanga inaweza toa tofali ngap?
Then gharama za kununua mashine hasa ya mkono coz ndio naanza

Kibarua wa kufyatua per bag nimlipe ela nga

I dont expect to have a maximum profit at the lowest risk
 
Mkuu naomba nikuulizie kuhusu hii kitu maana mzee wangu ndo alikuwa anafanya hii biashara, sijajua kama bei ipo sawa ila faida ipo mkuu.....
 
Mkuu naomba nikujibu ninayoyajua, kwanza faida ipo ondoa shaka

Pili9 mfuko mmoja wa cement, inategemea na aina ya tofali ila kwauzoefu wangu, mfuko mmoja hutoa tofali 40 zenye quality nzuri, ila kuna uchakachuaji mwingi kiasi kwamba kuna wengine wanatoa hadi tofali 55 hadi 60 .....

Unaweza chakachua na tofali zako zikawa na quality nzuri kutokana na mchanga (mchanga wa bagamoyo) mzuri sana.....so unaweza tafuta sample yake.....

Tatu, kuhusu tipa ya mchanga inatoa tofali ngapi sina hesabu sahihi mkuu ila kwa mwaka 2019 ilikuwa ni 13000 hadi 13500.....

Nne, Mashine ya mkono zinapatikana kwenye viwanda vya SIDO bei inaanzia laki 4 hadi 350.....pia unahitaji kuwa na vibao ambavyo hivi nashauri uende kwa mafundi (carpenter) wanakutolea vibao vingi....unahitaji kama vibao 400 hadi 500....

Tano, Vibarua hulipwa kutokana na mfuko wa cement, so mfano wapo vibarua 7 basi unawapa 5000 kutokana na mfuko wa cement, (ila hata wakiwa 10 bei ni hiyo hiyo 5000) hii hesabu ni ya 2019 ila ikiongezeka sana inaweza kuwa elfu 6 au 7 ila wewe wakomalie elfu 5.....
 
Mkuu cha msingi ubora wa tofali unazofyatua unategeneana na aina ya mchanga, aina ya cement na maji unayitumia kumwagilia.

Maji yakiwa na kemikali au chumvi sana sio mazuri kwa kufyatulia matofali...., cement bora itabidi uwaulize wauzaji maana ubira wa cement nahisi zimetofautiana kipindi cha karibuni kuna cement nzuri zaidi

Ujitahidi pia kumwagilia maji kwa siku 7 za mwanzo asubuhi na jioni ili kupata quality nzuri na, kuzuia tofali kutoa ufa ambao utafabya uoate hasara ...

Pia inabidi kuwe na mchanganyiko sahihi wa cement na mchanga kutoa tofali bora,.....

Pia kuna suala la usimamizi direct...yani uwepo eneo la tukio mda wote vibarua wanavyofyatua ili wasikuibie cement.....

Vilevile utafute eneo zuri mkuu, eneo ambalo linafikika kwa urahisi, au lenye ujenzi mkubwa unaoendelea...... Uwe na office eneo hilohilo, ili iwe rahisi kuwahudumia wateja kwa haraka, pia daftari la kutunza kumbukumbu muhimu sana,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…