lucky sabasaba
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 1,656
- 1,204
Habari za leo JF..Watu wengi wanasema wana mitaji lakini hawajuhi wafanye nini,mimi naishi dubai ila sitaki kufanya biz na mtu maana najua watakuja watu na comments kwamba wanataka kuibiwa..kuna hii biz ya vifaa vya ujenzi,napenda kuwaambia kuwa hivi vifaa vinauzwa bei rahisi kuliko bidhaa zote hapa dubai,mfano mfuko mmoja wa cement wa kiwango cha juu kuununua na kuutuma mpaka dar unakugharimu tsh 4500 ndio maana unaona mifuko ya cement toka arabuni ni mingi Tz kiufupi inawalipa sana wafanya biashara,mbali na cement vifaa vingine kama tiles..vitasa..milango..sinks..vyoo..nk ni bei ndogo sana milango mizuri ambayo wahindi wanatuuzia laki 4 hapa inauzwa elfu 85..zaidi ya hapo vifaa vyote vya ujenzi mbali ya cement uwa vina ushuru mdogo sana bandarini...utumaji pia si ghari wawezatumia container kama una mzigo mkubwa,ambalo litakuwa $1700 lenye futi 20 ambalo wawezajaza vitu vyovyote utakavyo...lakini kabda hujafanya hivi mtafute agent yoyote mwenye ofisi ili akupe maelezo ya jinsi ya kuvitoa bandarini..hii si kwa wafanyabiashara tu ata kama unatakajenga nyumba yako wawezanunua kwa kiasi utakacho..suala la cement kuna wazoefu wa biz hiyo mimi nilinunua mwaka jana kwa ajiri ya matumizi binafsi mifuko 150 utoaji bandarini haukua bei kubwa lakini walinisumbua sana..hivyo kama una mtaji wawezajaribu hii..kuna sehemu kubwa zaidi ya kariakoo ambayo imetengwa maalumu kwa ajiri ya vifaa vya ujenzi...so kama umeipenda ijaribu hii..nawasilisha
Hivi Tanzania sisi ni lini tuta Export? Ni sawa kuimport kutoka huko kwa sababu ya Bei yake ila tutambue kwamba tua kuza uchumi wa Dubai na si Tanzania ni kama ilivyo China, Huwa najiuliza kama hadi Milango tunaagiza nje ni huzuni sana wakati tuna mbao na hata Milango inayo tengenezwa na Wabongo ni Bora zaidi ya hiyo ya Kutoka Nje,
Mimi nazani imefika wakati tupende vya kwetu hata kama ni vibaya kiasi gani, China walivyo anza Kujitegemea walikuwa wakitengeneza Bidhaa mbaya na walikuwa wakichekwa sana na Nchi za Ulaya, Ila jamaa hawakukata Tamaa, kuna ile Tiper yao ambayo Ulaya waliidhihaki sana,
Ila leo hii zile Nchi zote zilizo kuwa zinaicheka China ziko mahututi na imebakia Moja tu nayo ni Ujerumani ambayo nayo itapitwa muda si mrefu,
Nataka kufungua biashara ya duka la vifaa vya ujenzi naomba ushauri ni mtaji wa kiasi gani ni nzuri kuanzia na eneo gani ni zuri kibiashara.
Habari zenyu wanaharakati naomba ushauri kuhusiana na biashara hii nampango wa kuanza nayo.
Kama huna 60 milions sahau kuhusu hardware
mkuu acha kumkatisha tamaa anaweza kuanza na mtaji mdogo lkn akiwa makin nao atatoka
Ushauri wako job k ni mzuri, pia kumbukeni Unaposema Hardware ni pana sana hasa kwenye miji mikubwa inaweza gawanyika zaidi ya mara tatu, mfano Kariakoo Dar yapo maduka ya (Gypsum products board,powder, Hardboard, Belts, chip boards,marine boards,chokaa Rangi zote, tiles n.k) group la pili (bati,bomba maji, mabomba yote,flat bars sq pipies nondo,steel sheets, Glasses, wire mesh, hardboards,misumari, tiles,) tatu (patasi,nyundo,misumari,kufuli, gundi mbao, dawa mbao, pvc sheet,bawaba tape maji) huo ni mfano tu unaweza tofautisha hardware ndg ndg na pia hardware kubwa kubwa wapo watu wanauza aina zote za cement na chokaa tuuuu kwa hardware ndg ndg mtaji hata wa 5 mln unatosha sana hasa ukiwa karibu na mafundi wa vitu hivyo lakini kama ni kubwa mfano ya cement roli moja tu mikoani 10 mln na zaidi kwa hiyo wote muko sawa wa 60 mln na pia 7 mln
Mkuu kama ni HARDWARE kubwa tuwasiliane nitakupa data zote niko kwenye hiyo zaidi ya miaka 20, naijua vema ndogo hapana siijui
CONSULT nami pia napenda kuwasiliana nawe. xsadala@gmail.comUshauri wako job k ni mzuri, pia kumbukeni Unaposema Hardware ni pana sana hasa kwenye miji mikubwa inaweza gawanyika zaidi ya mara tatu, mfano Kariakoo Dar yapo maduka ya (Gypsum products board,powder, Hardboard, Belts, chip boards,marine boards,chokaa Rangi zote, tiles n.k) group la pili (bati,bomba maji, mabomba yote,flat bars sq pipies nondo,steel sheets, Glasses, wire mesh, hardboards,misumari, tiles,) tatu (patasi,nyundo,misumari,kufuli, gundi mbao, dawa mbao, pvc sheet,bawaba tape maji) huo ni mfano tu unaweza tofautisha hardware ndg ndg na pia hardware kubwa kubwa wapo watu wanauza aina zote za cement na chokaa tuuuu kwa hardware ndg ndg mtaji hata wa 5 mln unatosha sana hasa ukiwa karibu na mafundi wa vitu hivyo lakini kama ni kubwa mfano ya cement roli moja tu mikoani 10 mln na zaidi kwa hiyo wote muko sawa wa 60 mln na pia 7 mln
Mkuu kama ni HARDWARE kubwa tuwasiliane nitakupa data zote niko kwenye hiyo zaidi ya miaka 20, naijua vema ndogo hapana siijui