Biashara ya Vifaa vya Ujenzi (Hardware Store): Ushauri wa Mtaji, Uendeshaji, Changamoto na Faida

Biashara ya Vifaa vya Ujenzi (Hardware Store): Ushauri wa Mtaji, Uendeshaji, Changamoto na Faida

Umenena vyema mkuu ndugu CHASHA lakini si kwamba hatupendi vya kwetu bali kwetu kuna urasimu na uhuni mwingi, serikali inatoza kodi kubwa kupindukia. Nitakupa mfno hai. Mwishoni mwa 12 mwaka 2018, nilienda kununua cement mfuko mmoja niliuziwa shilingi elf TZ,19500/=hapa kwetu TZ lakini nikajongea nchi jirani ya Uganda nikakuta mfuko huo huo wa cementi unauzwa shilingi elf za Kitanzania 15,500/= sasa hapa nauli ya kutoka hapo hadi nilipo hitaji kuipeleka cement ni shilingi elf 1000 kwa kila mfuko sawa na jumla ya 16,500/=( rejareja) Je, utanunua Mali ya Tz au utanunua Mali Ya UG. Nikaenda kwenye vitenge vya JAVa na Wax, the same product lakini nchi jirani kuna unafuu sana kulinganisha na TZ. Nikaenda kwenye suruali za kiume (KADETI) huku kwetu nilikuta ni kati ya elfu 21/22 the same product nchi jirani ni shilingi elf 15/16 rejareja. Serikali imekosa weredi katika kubalance ushuru ndiyo maana kununua vya nje hakuwezi kuisha si kwamba hatupendi vya kwetu.
 
Bora Dubai tu manina zao kama mtu ana kitanda chake katoka nacho LUPEMBE NJOMBE anaenda kuanza maisha Dar halafu anaambiwa kishushwe ndani ya basi hakina vibali sasa maanake nini.Si bora niagize Dubai nilalie kitu cha DANUBE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi cement huwa hazina expire date(haziharibiki)? Kama zinaharibika,basi heri mtu uwe wakala ili zikiharibika wabebe mizigo yao other wise hasara atabeba muuzaji
Zikikaa mda mrefu huwa zinapungua nguvu
 
1129614


Ni baada ya upanuzi wa gati la kisasa kukamilika, katika bandari ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa.

BIASHARA ya saruji kwenda nchi za Demokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi, inatarajiwa kushika kasi na kukuza uchumi wa Taifa, baada ya upanuzi wa gati la kisasa kukamilika, katika bandari ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa.

Kwa sasa bandari hiyo ina gati lenye urefu wa mita 20 lenye uwezo wa kupokea meli moja na mpango Mamlaka ya Bandari (TPA) ni kuongeza gati lenye urefu wa mita 100 na kufika mita 120 litakalowezesha kupokea meli tatu za mizigo na abiria. Meneja wa bandari ya Kigoma anayesimamia bandari zote za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese, akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea bandari hiyo juzi, amesema bandari hiyo inategemewa kwa kusafirisha saruji kutoka Mbeya kulekea nchi za Congo na Burundi.

Amesema upanuzi wa bandari hiyo utakaogharimu Sh. bilioni 4.7 utawezesha shehena kubwa ya saruji kusafirishwa kwenda nchi hizo kutoka tani 20,000 kwa mwaka hadi tani 100,000 kwa mwaka. "Kuboreshwa kwa bandari hii ya kimkakati inayotegemewa na mikoa ya Katavi, Mbeya, Songwe na Rukwa utawezesha kukuza uchumi wa Taifa. Bidhaa kubwa inayosafishwa kwenda nchi za Congo na Burundi ni saruji ambayo inazalishwa na kiwanda cha Safuri cha Mbeya Cement.

Hivyo tunatarajia mizigo itakayosafirishwa inaongezeka mara tano zaidi," amesema Msese
Amesema mapato ya bandari hiyo kwa mwaka ni Sh. bilioni moja hivyo wanatarajia yataongezeka mara dufu baada ya kukamilika mradi huo. Adha, amesema bandari hiyo ambayo ipo Kusini mwa Ziwa Tanganyika, ina ghala la kuhifadhi tani 2,000 za saruji na ghala lingine la nje lenye uwezo kuhifadhi tani 2,000 ya makaa ya mawe.

"Upanuzi wa bandari pia utasaidia shughuli za bandari kufanyika kwa wakati na kuondoa msongamano wa meli zinazosafirisha mizigo kukaa bandarini kwa muda mrefu kwa sababu zote zitafanya kazi kwa wakati mmoja," amesema kiongozi huyo. Amesema zaidi kuwa, upanuzi wa gati hilo utaenda sambamba na ujenzi wa sakafu ngumu, ujenzi wa nyumba za wafanyakazi, ghala kubwa la kuhifadhia shehena ya mizigo na ofisi za taasisi za umma zinazofanya kazi na bandari.

Adha, amesema kuelekea katika bandari hiyo kulikuwa na changamoto ya barabara ya kutoka Namanyele kuelekea Kisanga ambayo kwa sasa imeanza kujengwa na Wakala wa Barabara (Tanrods) ili kuongeza ufanisi wa bandari.
 
Gharama za uzalishaji saruji ni kubwa mno kuliko Nchi za jirani ie Kenya
esther mashiker ni mbinu gani utaitumia ili Mrundi anunue simenti ya Tanzania akaacha ya Pakistan?
esther mashiker umetumwa na unatumika, ondoa akili zako kwenye rasta, zirudishe kwenye ubongo
Duuuh umenikumbusha kitu viwanda vya Tanzania havina uwezo wa kusambaza hiyo saruji nchi jirani kwa kiwango hicho

Mpaka sasa hakuna kiwanda kinacho zalisha tani elf moja kwa siku sasa unajiuliza tu kwa mahitaji ya ndani tu haitoshi sasa huko nje tutapeleka nini
 
Duuuh umenikumbusha kitu viwanda vya Tanzania havina uwezo wa kusambaza hiyo saruji nchi jirani kwa kiwango hicho

Mpaka sasa hakuna kiwanda kinacho zalisha tani elf moja kwa siku sasa unajiuliza tu kwa mahitaji ya ndani tu haitoshi sasa huko nje tutapeleka nini
esther mashiker kawaambie walio kudanganya kuwa Watanzania sio mbumbummbu tena.
Tena ukiwa muungwana esther mashiker utuombe radhi
 
Mbona unachukia kusikia mema ya nchi?
Mema au ujinga? Mema tunayajua lakini sio hili la simenti, msitulazimishe tuamini uwongo wenu.
Unafahamu factors which are determining price?
Hebu tupe hizo factor halafu utuambie je mzalishaji Mdogo anawezaje kushindana na mzalishaji Mkubwa anaye enjoy economies of scale?
 
Sio kweli mkuu, npo kwnye hyo industry vipo viwanda vinatoa tan 2000 mpk 3000 kwa siku
Duuuh umenikumbusha kitu viwanda vya Tanzania havina uwezo wa kusambaza hiyo saruji nchi jirani kwa kiwango hicho

Mpaka sasa hakuna kiwanda kinacho zalisha tani elf moja kwa siku sasa unajiuliza tu kwa mahitaji ya ndani tu haitoshi sasa huko nje tutapeleka nini
 
Back
Top Bottom