tinkanyarwele
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 2,016
- 1,946
Umenena vyema mkuu ndugu CHASHA lakini si kwamba hatupendi vya kwetu bali kwetu kuna urasimu na uhuni mwingi, serikali inatoza kodi kubwa kupindukia. Nitakupa mfno hai. Mwishoni mwa 12 mwaka 2018, nilienda kununua cement mfuko mmoja niliuziwa shilingi elf TZ,19500/=hapa kwetu TZ lakini nikajongea nchi jirani ya Uganda nikakuta mfuko huo huo wa cementi unauzwa shilingi elf za Kitanzania 15,500/= sasa hapa nauli ya kutoka hapo hadi nilipo hitaji kuipeleka cement ni shilingi elf 1000 kwa kila mfuko sawa na jumla ya 16,500/=( rejareja) Je, utanunua Mali ya Tz au utanunua Mali Ya UG. Nikaenda kwenye vitenge vya JAVa na Wax, the same product lakini nchi jirani kuna unafuu sana kulinganisha na TZ. Nikaenda kwenye suruali za kiume (KADETI) huku kwetu nilikuta ni kati ya elfu 21/22 the same product nchi jirani ni shilingi elf 15/16 rejareja. Serikali imekosa weredi katika kubalance ushuru ndiyo maana kununua vya nje hakuwezi kuisha si kwamba hatupendi vya kwetu.