Samahani mkuu naomba nikuweke sawa hapo..
Dangote Cement anazarisha 6000tone/day, Tanga Cement anazarisha 4000tone/day, Twiga Cement anazarisha zaidi ya 1500/day, Mbeya Cement around 1000tone/day..
Kwa uzarishaji nafikiri tunazarisha nyingi kuliko nchi yeyote East Africa nafikiri tatizo kubwa la kuzingatia kuna mchangiaji hapo juu ameelezea ni Gharama za uzarishaji zinazopelekea bei kuwa juu kuliko imported cement inayotoka pakistani na India. Ni vyema wenye mamlaka na maamuzi wakajaribu kupitia gharama za uendeshaji hivi viwanda ili kuvipunguzia mzigo vizarishe zaidi na kuuza cement kwa bei ya chini, pia tuboreshe hizi reli za mipakani ili kurahisisha cement kufika kwa haraka na nafuu mipakani.. Tuwawezeshe wafanyabiashara wa Kitanzania wafungue madepot ya Cement kwenye nchi kama Uganda, Rwanda, Burundi, Congo DRC, Eritrea, Djibout, Comoro kupitia bahari tuweze kufikisha cement huko kirahisi ili viwanda vyetu viweze kufanya kazi na kuajiri watu wetu maelfu na kulipa kodi nyingi..