komamgo
JF-Expert Member
- Sep 14, 2012
- 1,757
- 1,483
SafiSio kweli mkuu, npo kwnye hyo industry vipo viwanda vinatoa tan 2000 mpk 3000 kwa siku
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
SafiSio kweli mkuu, npo kwnye hyo industry vipo viwanda vinatoa tan 2000 mpk 3000 kwa siku
Hata isipoingia nchini, Nchi nyingine inaingia, je tunaweza kushindana nayo sokoni?kweli kabisa ni shida, saruji ya pakistani inauzwa bei gani hapa nchini hata hivyo sidhani kama itakuwa inaruhusiwa kuingia
20,000 kama inavyouzwa Bukoba.
Yaa.Kama hakuna cement nyingine watanunua.
Hata isipoingia nchini, Nchi nyingine inaingia, je tunaweza kushindana nayo sokoni?
Mod hii lugha gani aiseeOfuruke Ogye Dar. Negurwa 13,500.
Wewe mi sio kama wewe mwongo mi ni mkweli asilimia mia ila wew ni mfanya biashara ndio unataka kutudandanyaWewe ni muongo unafanya kazi kwenye viwanda vya Simenti kwenye keyboard za computer tu usidanganye watu sie kila siku tupo kwenye hii biashara sema tukuambie , tusafirisha simenti kupeleka Kongo Burundi na watoto wanaenda choo acha upotoshaji.
Ekitakukwet'okileke!!!Mod hii lugha gani aisee
Mkuu dangote sina uhakika kama anazalisha hiyo tani unazo sema
Kwenye makaratasi huwa mandishi tofaut na vitendo
Mbeya cement wakijitahidi huwa wanafikisha tani 600 hapo wanatumia mill mbili
Nyati wao wakijitahidi sana wanaenda mpaka 800
Twigs kidogo wanasogea 900
Kwenye makratasi watambia tofauti ila kwa sisi tulio wahi kufanya kazi kwenye hivi viwanda tunajua
Mijadala yenye ushahidi kama hii inapendeza.Haha, et niwe mkweli,, ok kuna Dangote, Lake cement wazalishaj wa Nyati cement, Twiga cement huyu anapga zaid ya tani laki 1 kwa mwezi.
Ukihitaji mzigo karibu.
Lakini 'installed capacity' yao ni kubwa zaidi kuliko hizo namba ulizotoa au sio?Mkuu dangote sina uhakika kama anazalisha hiyo tani unazo sema
Kwenye makaratasi huwa mandishi tofaut na vitendo
Mbeya cement wakijitahidi huwa wanafikisha tani 600 hapo wanatumia mill mbili
Nyati wao wakijitahidi sana wanaenda mpaka 800
Twigs kidogo wanasogea 900
Kwenye makratasi watambia tofauti ila kwa sisi tulio wahi kufanya kazi kwenye hivi viwanda tunajua
Pinga pinga kaziniGharama za uzalishaji saruji ni kubwa mno kuliko Nchi za jirani ie Kenya
esther mashiker ni mbinu gani utaitumia ili Mrundi anunue simenti ya Tanzania akaacha ya Pakistan?
esther mashiker umetumwa na unatumika, ondoa akili zako kwenye rasta, zirudishe kwenye ubongo
Mkuu uzalishaji chini ya kiwango kunatokana na aina ya mitambo yao ya kuzalishia cement kwa mfano mtambo ulio zinduliwa na raisi ulikujengwa kwa mategemeo ya kuzalisha tani 100 kwa saa lakini unazalisha tani 55 mpaka 60 kwa SAALakini 'installed capacity' yao ni kubwa zaidi kuliko hizo namba ulizotoa au sio?
Maana yake ni kuwa kama wanazalisha chini ya kiwango cha uwezo wao, kuna sababu zinazopelekea kufanya hivyo; mojawapo ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa soko, au.... Sasa soko kama linapatikana DRC si watazidisha uzalishaji huo hadi kufikia uwezo wao wa uzalishaji?
Labda ungeeleza sababu zinazosababisha wazalishe chini ya kiwango, hapo hoja yako ingeeleweka.
Kuelewa ni ngumu kama unasoma kwenye makaratasi na hauko kiwandanisikuelewi unajua, wewe mwenyewe unasema hakuna kiwanda kinachozalisha tani 1000 kwa siku, hapohapo unakubali Twiga inazalisha mpk 900 kwa siku na unajua Tanga Cement ndie alikuwa mzalishaji mkubwa wa cement kabla ya kuingia kwa DANGOTE... jee alikua anazalisha chini ya 1,000??
Mkuu njoo tukutembeze kwe viwanda ujue uzalishaji ulivyo na si kuingizwa vichaka kama unavyo aminishwa hapaMijadala yenye ushahidi kama hii inapendeza.
Huyo jamaa uliyemjibu alitaka kutuingiza kwenye kichaka bila ya wewe kufyeka kichaka chake. Na wapo wengi wa namna hiyo humu JF.
Saruji inayozalishwa na viwanda vya ndani ni nyingi kuliko mahitaji ya ndani mkuuDuuuh umenikumbusha kitu viwanda vya Tanzania havina uwezo wa kusambaza hiyo saruji nchi jirani kwa kiwango hicho
Mpaka sasa hakuna kiwanda kinacho zalisha tani elf moja kwa siku sasa unajiuliza tu kwa mahitaji ya ndani tu haitoshi sasa huko nje tutapeleka nini
Unajua sio kwanba uzalishaji unazidi watumiaji ila garama za kununua ziko juu zaidiSaruji inayozalishwa na viwanda vya ndani ni nyingi kuliko mahitaji ya ndani mkuu
Mkuu hakuna barabara yoyote inayojengwa kutoka Namanyere kwenda kasanga na wala sababu na huo mpango haipo ila kuna barabara iko hatua za mwisho kutoka sumbawanga/Matai kwenda kasangaView attachment 1129614
Ni baada ya upanuzi wa gati la kisasa kukamilika, katika bandari ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa.
BIASHARA ya saruji kwenda nchi za Demokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi, inatarajiwa kushika kasi na kukuza uchumi wa Taifa, baada ya upanuzi wa gati la kisasa kukamilika, katika bandari ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa.
Kwa sasa bandari hiyo ina gati lenye urefu wa mita 20 lenye uwezo wa kupokea meli moja na mpango Mamlaka ya Bandari (TPA) ni kuongeza gati lenye urefu wa mita 100 na kufika mita 120 litakalowezesha kupokea meli tatu za mizigo na abiria. Meneja wa bandari ya Kigoma anayesimamia bandari zote za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese, akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea bandari hiyo juzi, amesema bandari hiyo inategemewa kwa kusafirisha saruji kutoka Mbeya kulekea nchi za Congo na Burundi.
Amesema upanuzi wa bandari hiyo utakaogharimu Sh. bilioni 4.7 utawezesha shehena kubwa ya saruji kusafirishwa kwenda nchi hizo kutoka tani 20,000 kwa mwaka hadi tani 100,000 kwa mwaka. "Kuboreshwa kwa bandari hii ya kimkakati inayotegemewa na mikoa ya Katavi, Mbeya, Songwe na Rukwa utawezesha kukuza uchumi wa Taifa. Bidhaa kubwa inayosafishwa kwenda nchi za Congo na Burundi ni saruji ambayo inazalishwa na kiwanda cha Safuri cha Mbeya Cement.
Hivyo tunatarajia mizigo itakayosafirishwa inaongezeka mara tano zaidi," amesema Msese
Amesema mapato ya bandari hiyo kwa mwaka ni Sh. bilioni moja hivyo wanatarajia yataongezeka mara dufu baada ya kukamilika mradi huo. Adha, amesema bandari hiyo ambayo ipo Kusini mwa Ziwa Tanganyika, ina ghala la kuhifadhi tani 2,000 za saruji na ghala lingine la nje lenye uwezo kuhifadhi tani 2,000 ya makaa ya mawe.
"Upanuzi wa bandari pia utasaidia shughuli za bandari kufanyika kwa wakati na kuondoa msongamano wa meli zinazosafirisha mizigo kukaa bandarini kwa muda mrefu kwa sababu zote zitafanya kazi kwa wakati mmoja," amesema kiongozi huyo. Amesema zaidi kuwa, upanuzi wa gati hilo utaenda sambamba na ujenzi wa sakafu ngumu, ujenzi wa nyumba za wafanyakazi, ghala kubwa la kuhifadhia shehena ya mizigo na ofisi za taasisi za umma zinazofanya kazi na bandari.
Adha, amesema kuelekea katika bandari hiyo kulikuwa na changamoto ya barabara ya kutoka Namanyele kuelekea Kisanga ambayo kwa sasa imeanza kujengwa na Wakala wa Barabara (Tanrods) ili kuongeza ufanisi wa bandari.