Biashara ya Vifaa vya Ujenzi (Hardware Store): Ushauri wa Mtaji, Uendeshaji, Changamoto na Faida

Biashara ya Vifaa vya Ujenzi (Hardware Store): Ushauri wa Mtaji, Uendeshaji, Changamoto na Faida

Wewe ni muongo unafanya kazi kwenye viwanda vya Simenti kwenye keyboard za computer tu usidanganye watu sie kila siku tupo kwenye hii biashara sema tukuambie , tusafirisha simenti kupeleka Kongo Burundi na watoto wanaenda choo acha upotoshaji.
Wewe mi sio kama wewe mwongo mi ni mkweli asilimia mia ila wew ni mfanya biashara ndio unataka kutudandanya

Tatizo unafikiri wote tunakaa kwaajili ya kudanganya watu
 
Mkuu dangote sina uhakika kama anazalisha hiyo tani unazo sema

Kwenye makaratasi huwa mandishi tofaut na vitendo

Mbeya cement wakijitahidi huwa wanafikisha tani 600 hapo wanatumia mill mbili

Nyati wao wakijitahidi sana wanaenda mpaka 800

Twigs kidogo wanasogea 900

Kwenye makratasi watambia tofauti ila kwa sisi tulio wahi kufanya kazi kwenye hivi viwanda tunajua

sikuelewi unajua, wewe mwenyewe unasema hakuna kiwanda kinachozalisha tani 1000 kwa siku, hapohapo unakubali Twiga inazalisha mpk 900 kwa siku na unajua Tanga Cement ndie alikuwa mzalishaji mkubwa wa cement kabla ya kuingia kwa DANGOTE... jee alikua anazalisha chini ya 1,000??
 
Haha, et niwe mkweli,, ok kuna Dangote, Lake cement wazalishaj wa Nyati cement, Twiga cement huyu anapga zaid ya tani laki 1 kwa mwezi.

Ukihitaji mzigo karibu.
Mijadala yenye ushahidi kama hii inapendeza.
Huyo jamaa uliyemjibu alitaka kutuingiza kwenye kichaka bila ya wewe kufyeka kichaka chake. Na wapo wengi wa namna hiyo humu JF.
 
Mkuu dangote sina uhakika kama anazalisha hiyo tani unazo sema

Kwenye makaratasi huwa mandishi tofaut na vitendo

Mbeya cement wakijitahidi huwa wanafikisha tani 600 hapo wanatumia mill mbili

Nyati wao wakijitahidi sana wanaenda mpaka 800

Twigs kidogo wanasogea 900

Kwenye makratasi watambia tofauti ila kwa sisi tulio wahi kufanya kazi kwenye hivi viwanda tunajua
Lakini 'installed capacity' yao ni kubwa zaidi kuliko hizo namba ulizotoa au sio?
Maana yake ni kuwa kama wanazalisha chini ya kiwango cha uwezo wao, kuna sababu zinazopelekea kufanya hivyo; mojawapo ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa soko, au.... Sasa soko kama linapatikana DRC si watazidisha uzalishaji huo hadi kufikia uwezo wao wa uzalishaji?

Labda ungeeleza sababu zinazosababisha wazalishe chini ya kiwango, hapo hoja yako ingeeleweka.
 
Gharama za uzalishaji saruji ni kubwa mno kuliko Nchi za jirani ie Kenya
esther mashiker ni mbinu gani utaitumia ili Mrundi anunue simenti ya Tanzania akaacha ya Pakistan?
esther mashiker umetumwa na unatumika, ondoa akili zako kwenye rasta, zirudishe kwenye ubongo
Pinga pinga kazini
Saruji itoke pakistan mpaka ifike kalemie ni bora kununua ya Tanzania
Hujui kwamba export price ipo chini brother?
 
Lakini 'installed capacity' yao ni kubwa zaidi kuliko hizo namba ulizotoa au sio?
Maana yake ni kuwa kama wanazalisha chini ya kiwango cha uwezo wao, kuna sababu zinazopelekea kufanya hivyo; mojawapo ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa soko, au.... Sasa soko kama linapatikana DRC si watazidisha uzalishaji huo hadi kufikia uwezo wao wa uzalishaji?

Labda ungeeleza sababu zinazosababisha wazalishe chini ya kiwango, hapo hoja yako ingeeleweka.
Mkuu uzalishaji chini ya kiwango kunatokana na aina ya mitambo yao ya kuzalishia cement kwa mfano mtambo ulio zinduliwa na raisi ulikujengwa kwa mategemeo ya kuzalisha tani 100 kwa saa lakini unazalisha tani 55 mpaka 60 kwa SAA

Manake ni kuwa ukipiga hesabu ni kuwa uwezo wa kuzalisha tani 1000 kwa siku ni ngumu
 
sikuelewi unajua, wewe mwenyewe unasema hakuna kiwanda kinachozalisha tani 1000 kwa siku, hapohapo unakubali Twiga inazalisha mpk 900 kwa siku na unajua Tanga Cement ndie alikuwa mzalishaji mkubwa wa cement kabla ya kuingia kwa DANGOTE... jee alikua anazalisha chini ya 1,000??
Kuelewa ni ngumu kama unasoma kwenye makaratasi na hauko kiwandani
 
Mijadala yenye ushahidi kama hii inapendeza.
Huyo jamaa uliyemjibu alitaka kutuingiza kwenye kichaka bila ya wewe kufyeka kichaka chake. Na wapo wengi wa namna hiyo humu JF.
Mkuu njoo tukutembeze kwe viwanda ujue uzalishaji ulivyo na si kuingizwa vichaka kama unavyo aminishwa hapa
 
Duuuh umenikumbusha kitu viwanda vya Tanzania havina uwezo wa kusambaza hiyo saruji nchi jirani kwa kiwango hicho

Mpaka sasa hakuna kiwanda kinacho zalisha tani elf moja kwa siku sasa unajiuliza tu kwa mahitaji ya ndani tu haitoshi sasa huko nje tutapeleka nini
Saruji inayozalishwa na viwanda vya ndani ni nyingi kuliko mahitaji ya ndani mkuu
 
Saruji inayozalishwa na viwanda vya ndani ni nyingi kuliko mahitaji ya ndani mkuu
Unajua sio kwanba uzalishaji unazidi watumiaji ila garama za kununua ziko juu zaidi

Kwa mfano ukiwa mbeya cement yao inauzwa 14500 kwa 15500

Wakati huo ukifika Iringa inauzwa 13500 mpaka 14500 wakipunguza Bei Haita tosha na kwa cement inayo pelekwa nje inauzwa Bei ya chini kuliko bei tunayo uziwa huku kwetu
 
View attachment 1129614

Ni baada ya upanuzi wa gati la kisasa kukamilika, katika bandari ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa.

BIASHARA ya saruji kwenda nchi za Demokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi, inatarajiwa kushika kasi na kukuza uchumi wa Taifa, baada ya upanuzi wa gati la kisasa kukamilika, katika bandari ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa.

Kwa sasa bandari hiyo ina gati lenye urefu wa mita 20 lenye uwezo wa kupokea meli moja na mpango Mamlaka ya Bandari (TPA) ni kuongeza gati lenye urefu wa mita 100 na kufika mita 120 litakalowezesha kupokea meli tatu za mizigo na abiria. Meneja wa bandari ya Kigoma anayesimamia bandari zote za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese, akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea bandari hiyo juzi, amesema bandari hiyo inategemewa kwa kusafirisha saruji kutoka Mbeya kulekea nchi za Congo na Burundi.

Amesema upanuzi wa bandari hiyo utakaogharimu Sh. bilioni 4.7 utawezesha shehena kubwa ya saruji kusafirishwa kwenda nchi hizo kutoka tani 20,000 kwa mwaka hadi tani 100,000 kwa mwaka. "Kuboreshwa kwa bandari hii ya kimkakati inayotegemewa na mikoa ya Katavi, Mbeya, Songwe na Rukwa utawezesha kukuza uchumi wa Taifa. Bidhaa kubwa inayosafishwa kwenda nchi za Congo na Burundi ni saruji ambayo inazalishwa na kiwanda cha Safuri cha Mbeya Cement.

Hivyo tunatarajia mizigo itakayosafirishwa inaongezeka mara tano zaidi," amesema Msese
Amesema mapato ya bandari hiyo kwa mwaka ni Sh. bilioni moja hivyo wanatarajia yataongezeka mara dufu baada ya kukamilika mradi huo. Adha, amesema bandari hiyo ambayo ipo Kusini mwa Ziwa Tanganyika, ina ghala la kuhifadhi tani 2,000 za saruji na ghala lingine la nje lenye uwezo kuhifadhi tani 2,000 ya makaa ya mawe.

"Upanuzi wa bandari pia utasaidia shughuli za bandari kufanyika kwa wakati na kuondoa msongamano wa meli zinazosafirisha mizigo kukaa bandarini kwa muda mrefu kwa sababu zote zitafanya kazi kwa wakati mmoja," amesema kiongozi huyo. Amesema zaidi kuwa, upanuzi wa gati hilo utaenda sambamba na ujenzi wa sakafu ngumu, ujenzi wa nyumba za wafanyakazi, ghala kubwa la kuhifadhia shehena ya mizigo na ofisi za taasisi za umma zinazofanya kazi na bandari.

Adha, amesema kuelekea katika bandari hiyo kulikuwa na changamoto ya barabara ya kutoka Namanyele kuelekea Kisanga ambayo kwa sasa imeanza kujengwa na Wakala wa Barabara (Tanrods) ili kuongeza ufanisi wa bandari.
Mkuu hakuna barabara yoyote inayojengwa kutoka Namanyere kwenda kasanga na wala sababu na huo mpango haipo ila kuna barabara iko hatua za mwisho kutoka sumbawanga/Matai kwenda kasanga
Pili kuna zaidi ya bandari ndogo 28 plus bandari kuu ya Kigoma kwenye mwambao wa ziwa Rukwa ambazo zinapatikana kwa kila mkoa mfano bandari ya Kabwe na New Kipili port zinajengwa huko Nkasi na serikali iko katika hatua za upembuzi yakinifu ili kuziunganisha na barabara za lami
Kwa Katavi kuna bandari ya karema nayo itapanuliwa mwaka huu wa fedha na mchakato wa kuiunganisha kwa lami kutoka mpanda mjini unaendelea
Mwisho ni kwamba ni bahati mbaya sana upande wa pili wa DRC hakuna miji mikubwa wala rasilimali za madini au nyinginezo za kuchochea biashara tofauti na kusini huko Lubumbashi na kaskazini jimbo la Bukavu thus why muingiliano wa biashara kati ya Tzn na drc mwambao mwa ziwa Tangangika ni kiduchu sana labda siku za baadae sana
 
Back
Top Bottom