Biashara ya Vifaa vya Ujenzi (Hardware Store): Ushauri wa Mtaji, Uendeshaji, Changamoto na Faida

Biashara ya Vifaa vya Ujenzi (Hardware Store): Ushauri wa Mtaji, Uendeshaji, Changamoto na Faida

Ntakupa maelezo mazuri sana kama ukiwa serious yatakusaidia.

Mimi naishi dubai huu ni mwaka wa 6 sasa, siku moja nikiwa likizo Tz niliona maduka mengi yakiwa na cement toka arabuni na pakistan. Wale watu wanapata faida kubwa sana. Mfuko mmoja wa kiwango cha juu kuununua na kuutuma mpaka port Dar itakugharimu kama Tsh 3500, sasa tatizo ni kwenye kuutoa.

Kipindi kile ufisadi bandarini ulikuwa mkubwa wakanisumbua sana japo nilikuwa na mifuko 100 tu kwa ajiri ya kibanda changu. Pia TBS watachukua mfuko mmoja ili kupima ubora na gharama ilikuwa TSH 20,000. Ilikuwa mwaka jana, sijuhi kwa sasa. Homework unayotakiwa kuifanya ni kutafuta agent mzuri mwenye ofisi na umwulize process ya utoaji ilivyo.

Navyojua chaji za TRA si kubwa sana ila bandarini walinisumbua. Nina hakika kuna faida kubwa sana kama ukijua utoaji bandarini ulivyo na utapata faida kubwa zaidi kama utanunua mzigo mkubwa.

Nakutakia kila la kheri gharama za ujenzi kwa wenzetu huku ni ndogo sana ila wana tatizo la plots za kujengea. Sisi tatizo ni gharama za vifaa vya ujenzi wakati maeneo tunayo.

Karibu sana najisikia vizuri nionapo mtu anatafuta maisha.

Thanks for the useful info mkuu ubarikiwe
Nina swali dogo inawezekana kununua vifaa kidogo vya ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba binafsi kwa mfano nikitaka kufanya roofing naweza kuagiza vigae/bati huko nika coload na mtu mwingine gharama yake itakuwaje? naweza kusave kitu hapo? au ni bora kununua huku huku tu?
 
Vifaa vya ujenzi kama tiles,milango na vitasa na vifaa vingine vingi sana vya ujenzi vipo chini sana na havina ushuru mkubwa ndio maana walioshtukia deal mapema wanapiga pesa sana..mfano floor tiles zilizo 15 kqenye box wawezanunua kwa tsh 5000 na ndio maana wenye pesa wakitaka kufanya finishing ya nyumba wanafanya ahopping kubwa huku.

Kusafirisha container zima la fiti 20 ni kama $1700 humo wawezajaza chochote utakacho..mlango mzuri ni tsh 70000 ambao ukiukita dukani Tz watakupiga 300000/jaribu kaka
 
Lucky sabasaba, asante kwa taarifa hii. Nina swali kuhusu hivyo vifaa vya ujenzi kama tiles, marble, milango, kitchen cabinets, madirisha. Je hao wauzaji (maduka) wana online website, ili wateja wa mbali kama huku TZ waweze kuona hizo bidhaa/ vifaa. Au ni mpaka mtu atie mguu huko huko Dubai?
 
Habari za leo JF..

Watu wengi wanasema wana mitaji lakini hawajui wafanye nini. Mimi naishi Dubai ila sitaki kufanya biz na mtu maana najua watakuja watu na comments kwamba wanataka kuibiwa..

Kuna hii biz ya vifaa vya ujenzi, napenda kuwaambia kuwa hivi vifaa vinauzwa bei rahisi kuliko bidhaa zote hapa Dubai. Mfano mfuko mmoja wa cement wa kiwango cha juu kuununua na kuutuma mpaka Dar unakugharimu tsh 4500 ndio maana unaona mifuko ya cement toka arabuni ni mingi Tz, kiufupi inawalipa sana wafanya biashara.

Mbali na cement vifaa vingine kama tiles..vitasa..milango..sinks..vyoo..nk ni bei ndogo sana milango mizuri ambayo wahindi wanatuuzia laki 4 hapa inauzwa elfu 85..

Zaidi ya hapo vifaa vyote vya ujenzi mbali ya cement huwa vina ushuru mdogo sana bandarini... Utumaji pia si ghari waweza tumia container kama una mzigo mkubwa, ambalo litakuwa $1700 lenye futi 20 ambalo waweza jaza vitu vyovyote utakavyo.. .lakini kabda hujafanya hivi mtafute agent yoyote mwenye ofisi ili akupe maelezo ya jinsi ya kuvitoa bandarini..

Hii si kwa wafanyabiashara tu, hata kama unataka jenga nyumba yako waweza nunua kwa kiasi utakacho.. Suala la cement kuna wazoefu wa biz hiyo mimi nilinunua mwaka jana kwa ajili ya matumizi binafsi mifuko 150 utoaji bandarini haukua bei kubwa lakini walinisumbua sana..

Hivyo kama una mtaji waweza jaribu hii..

Kuna sehemu kubwa zaidi ya Kariakoo ambayo imetengwa maalumu kwa ajiri ya vifaa vya ujenzi...so kama umeipenda ijaribu hii..

Nawasilisha.
 
Mkuu Kilo Saba saba, naomba muongozo wa bei elekezi za vifaa vya aina mbalimbali vyote, vya ICT hapo Dubai
 
Ninahitaji vitasa na tiles nitapita hapo siku tatu zijazo itakuwa ni usiku na kwa masaa kama kumi hivi ,utanisaidiaje kupita shopping fasta,ni pm tafadhali
 
Safi sana mkuu kwa moyo wako mkunjufu usio na roho ya why? Binafsi napenda kufanya buz za namna hiyo.

By the way ntakutafuta by PM unipe contact nur yako mkuu. But utakua huko kwa muda gani? Coz ningependa kuanza biashara hiyo mwezi nov.

Na Vp vifaa vya umeme? Is it cheap also?
 
Hivi Tanzania sisi ni lini tuta Export? Ni sawa kuimport kutoka huko kwa sababu ya Bei yake ila tutambue kwamba tua kuza uchumi wa Dubai na si Tanzania ni kama ilivyo China, Huwa najiuliza kama hadi Milango tunaagiza nje ni huzuni sana wakati tuna mbao na hata Milango inayo tengenezwa na Wabongo ni Bora zaidi ya hiyo ya Kutoka Nje,

Mimi nazani imefika wakati tupende vya kwetu hata kama ni vibaya kiasi gani, China walivyo anza Kujitegemea walikuwa wakitengeneza Bidhaa mbaya na walikuwa wakichekwa sana na Nchi za Ulaya, Ila jamaa hawakukata Tamaa, kuna ile Tiper yao ambayo Ulaya waliidhihaki sana,

Ila leo hii zile Nchi zote zilizo kuwa zinaicheka China ziko mahututi na imebakia Moja tu nayo ni Ujerumani ambayo nayo itapitwa muda si mrefu,
 
Wewe ulikuwa unadhani Wabongo hawapendi kupanda ndege? ona Fastjet walivyotoa offer ya shilling 32,000/= ticket zinavyogombewa. Na wewe kama ni mzalendo kweli shusha bei ya hizo bei ziwe chini ya bei za Dubai uone kama kuna mtu ataagiza bidhaa nje.
 
Wewe akili yako ni ndogo kama puwa yako. wewe ulikuwa unadhani Wabongo hawapendi kupanda ndege? ona Fastjet walivyotoa offer ya shilling 32,000/= ticket zinavyogombewa. Na wewe kama ni mzalendo kweli shusha bei ya hizo bei ziwe chini ya bei za Dubai uone kama kuna mtu ataagiza bidhaa nje.

wewe ndo kuku kabisa na hakuna unacho jua, na ndo wale wl wanao apply CIVICS kwenye maswala ya Uchumi wa Nchi, kwani wao waliaanzia wapi? au unazani na nwao walianza kwa kushusha bei? China yenyewe bidhaa zake zamani zilkuwa ni ghali tu kama za Ulaya, tatizo unatumia Masaburi tu,

Ishu kama Milando au thamani za Ndani, Mbona za Kitanzania ni Bora kabisa kimataifa, ulisha wahi ona Thamani zinazo tengenezwa na Jeshi la Magereza? Ni bora kimataifa, Ila wabongo bora tukanunua zile za maghumashi kutoka Dubai,

Kumbe inawezekana Mfuko wa Simenti kuuzwa kwa shs.5,000! (dr.slaa: Tanzania Election Campaign:2010)
 
Mkuu 77 hiyo nimeipenda, inaweza kuwa nzuri kama utapata mwongozo wa kutosha jinsi ya kuanza na gharama kwa ujumla ambazo utakuwa nazo hadi mzigo ufike stoo kwako.

Tafadhali hebu nipe gharama halizi za ununuzi kwa huko, usafiri mapaka dar port, ushuru wa bandari pamoja na gharama za ziada kama zipo kwa mzigo hadi niumiliki stoo kwangu, kwa aina zote za HARDWARE unazozifahamu.

Mimi always ni OPPORTUNIST, mtaji naweza kopa bank, japo wa kuanzia.

Nitafurahi kama utani PM
 
wewe ndo kuku kabisa na hakuna unacho jua, na ndo wale wl wanao apply CIVICS kwenye maswala ya Uchumi wa Nchi, kwani wao waliaanzia wapi? au unazani na nwao walianza kwa kushusha bei? China yenyewe bidhaa zake zamani zilkuwa ni ghali tu kama za Ulaya, tatizo unatumia Masaburi tu,

Ishu kama Milando au thamani za Ndani, Mbona za Kitanzania ni Bora kabisa kimataifa, ulisha wahi ona Thamani zinazo tengenezwa na Jeshi la Magereza? Ni bora kimataifa, Ila wabongo bora tukanunua zile za maghumashi kutoka Dubai,

mkuu vuta pumzi halafu angalia unachoandika kama ndiyo unachotarajia......hebu angalia hapo kwenye blue
 
Tatizo kodi iko juu sana that's why watu wanashindwa kumudu bei za vitu hapa tanzania kama kweli serikali inataka kupromoti vya nyumbani basi vipunguziwe kodi ili watu waweze kuvimudu kununua

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
wewe ndo kuku kabisa na hakuna unacho jua, na ndo wale wl wanao apply CIVICS kwenye maswala ya Uchumi wa Nchi, kwani wao waliaanzia wapi? au unazani na nwao walianza kwa kushusha bei? China yenyewe bidhaa zake zamani zilkuwa ni ghali tu kama za Ulaya, tatizo unatumia Masaburi tu,

Ishu kama Milando au thamani za Ndani, Mbona za Kitanzania ni Bora kabisa kimataifa, ulisha wahi ona Thamani zinazo tengenezwa na Jeshi la Magereza? Ni bora kimataifa, Ila wabongo bora tukanunua zile za maghumashi kutoka Dubai,

Mwenzio anaongelea mambo ya bei na mfumo m-bovu wa kuendesha uchumi wa nchi hasa utitiri wa kodi. Mbao inatoka hapo Muheza maushuru njiani kibao hapo bado haijafika Dar kukung'utwa VAT. Mpaka magereza waipate na kuifanyia kazi ya kochi au mlango bei ishafika mara tano ya ile ya mbao na hapo bado tena kuchajiwa Vat ya pili kama mlango safi au kiti kwenye shoo room. Dubai wanaipata mbao yetu kwa robo tu ya makodi na maushuru ya kushibisha matumbo ya mafisadi utakayopambana nayo hapa bongo.
 
Hivi Tanzania sisi ni lini tuta Export? Ni sawa kuimport kutoka huko kwa sababu ya Bei yake ila tutambue kwamba tua kuza uchumi wa Dubai na si Tanzania ni kama ilivyo China, Huwa najiuliza kama hadi Milango tunaagiza nje ni huzuni sana wakati tuna mbao na hata Milango inayo tengenezwa na Wabongo ni Bora zaidi ya hiyo ya Kutoka Nje,

Mimi nazani imefika wakati tupende vya kwetu hata kama ni vibaya kiasi gani, China walivyo anza Kujitegemea walikuwa wakitengeneza Bidhaa mbaya na walikuwa wakichekwa sana na Nchi za Ulaya, Ila jamaa hawakukata Tamaa, kuna ile Tiper yao ambayo Ulaya waliidhihaki sana,

Ila leo hii zile Nchi zote zilizo kuwa zinaicheka China ziko mahututi na imebakia Moja tu nayo ni Ujerumani ambayo nayo itapitwa muda si mrefu,
Kaka vya kwetu viko wapi ?kila kitu Mwinyi na Mkapa waliuza sasa kuna vitu gani au ni viwanda vipi vinavyozalisha Tanzania,hata vilivyopo bidhaa zake ni aghali kuliko bidhaa za nje,au kama unasema huenda tununue asali kutoka Tabora,ilaumiwe CCM na serikali yake na si wananchi ambao hawana kauli na michongo ya 10% waliyopata viongozi kwa kuuza viwanda tulivyokuwa navyo,Urafiki ,UFI vimekuwa yard za magari na nyumba za mapopo,si asavali kununua vitu Dubai bana,Tanzania iliondoka na Nyerere wacha kila mtu aangalie ustaarabu wake,pia waambie waliohodhi hela kwenye mabenki Uswisi warudishe wajenge viwanda hapa nchini ndipo tununue bidhaa made in Tanzania
 
Back
Top Bottom