Biashara ya vipuri vya pikipiki: Ushauri, michango, mawazo

Hivi maduka ya vifaa vya pikipiki Kariakoo yote ni ya vifaa vya Jumla?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bi Biashara hii inaweza kugharimu bei gani mpaka duka likamilike??
 
Mkuu naomba unisaidie maduka ya wafanyabiashara wanaouza vifaa original vya pikipiki kwa bei ya jumla kariakoo wapo mtaa gani
 
Hii kitu niliifikiria kabla sijaenda shamba but sikuweza kupata taarifa kamili kuhusu biashara inafanyikaje. Nataka nijue inafanyikaje na mtaji ni bei gani nianze nao kujaza kafremu walau ka laki moja
 
Nafikiria kuanziasha biashara ya kuuza spare za boda boda ila sija ufahamu juu ya mtaji na changamoto za biashara hyo.

naombeni ushauri
 
Biashara yoyote ile unaweza fanya ila vitu vikuu ambavyo lazima viwe checked:
1. Location
2. Capital (point kuu)
3. A,B,C za hiyo biashara.


Kama umeamua kufanya biashara hii na huna ujuzi hata wa kufungua taili nenda veta kuna short courses piga ili uwe na ABC
Maturity ya biashara yako hapa uwe mvumilivu sana maana unaweza dhani umechagua wrong business kipindi hiki kigumu unaweza fungua asubuhi mpaka jioni na usiuze hata 500.
 
asante. je kama ntamuajiri mtu anaefahamu vitu hvyo?
 
Mk Mkuu Tugusie kidogo kuhusu mtaji na Machimbo ya kupata spea kkoo..
 
Kuna rafiki yangu alianza hii biashara kwa mtaji wa mil 1.5 mambo yanaenda vizuri, yeye alitafuta location nzuri karibu na wanapopaki pikipiki na vile vile akatafuta fundi akawa anatengenezea hapo hapo.
 
Kuna rafiki yangu alianza hii biashara kwa mtaji wa mil 1.5 mambo yanaenda vizuri, yeye alitafuta location nzuri karibu na wanapopaki pikipiki na vile vile akatafuta fundi akawa anatengenezea hapo hapo.
Ni sahihi ukishafungua biashara muweke fundi pembeni kwa sharti la kumuuzia spare
 
Salaam WanaJamii forums,

Mimi binafsi sina uzoefu wa biashara ya duka, ndiyo natarajia kufungua biashara hii kwa mara ya kwanza. Ni duka dogo la spea za pikipiki.

Wenye uzoefu na biashara ya duka, naombeni mnisaidie. Nifanyeje kufuatilia bidhaa zinazotoka na mauzo yake? Namaanisha huwa mnafanyaje kuhusu management ya mauzo yote iwe ni kwa siku ama week ama kwa mwezi? Kufahamu bidhaa ngapi na ipi zimeuzwa kwa Tsh ngapi, bidhaa zipi na ngapi bado zipo kwenye shelf, n.k.

Pia naombeni mnishauri niiset vipi frem (chumba) ili iwe na mvuto wa kibiashara. Na nifanye favours zipi ama mambo gani ili kumvutia mteja akaribie tena na kuleta wenzake?

Bidhaa ni spea za pikipiki. Nitaajiri mtu wa kufanya mauzo dukani. Pia naweka Fundi pikipiki kwa nje kufanya service za pikipiki.

Naombeni mawazo yenu na ushauri.

Ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…