Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari ndugu,
Kwa wakat mwingi nimekuwa nikitamani sana kufungua duka la spare za pikipiki lakini bahat mbaya nimekosa taarifa zaidi kuhusu biashara hii,namna gani nitapata bidhaa na je mtaji wa chini wa kuanzia ni kiasi gan.nitashukuru kama nitapata mwongozo kutoka kwenu
Wazo zuri mimi cha kukushauri ni hivi kama unategemea kuifanya mwenyewe kama sehemu yako ya kujipatia mkate wa kila siku,tafuta sehemu wanayouza vifaa hivyo omba kufanya kazi ya kuuza pamoja nao free of charge.
Uwe muwazi kabisa lengo la kutaka kufanya nao ni nini.Uwaombe usihusike na kushika fedha wewe ni kuongea na wateja na kujua zaidi aina ya spares.Naamini hapo hapo utaanza kufahamu njia gani wanatumia kupata mzigo namna gani wanapata wateja na vitu kadha wa kadha.
Ni mawazo yangu
Upo mji/mahali gani? unataka kuuza kwa jumla au rejareja? tuanzie hapo.
Upo mji/mahali gani? unataka kuuza kwa jumla au rejareja? tuanzie hapo.