Biashara yangu inaniingizia faida ya Tsh. 200,000 kila mwezi; Je, Niiache niende chuo?

Biashara yangu inaniingizia faida ya Tsh. 200,000 kila mwezi; Je, Niiache niende chuo?

Risk ni neno linalokuzwa kuliko lilivyo lenyewe,hata kuzaa watoto ni risk kuliko kutokuzaa,lakini bado kila mtu anapambana azae,kuishi kwenyewe ni risk labda maiti ndo haina risk.

Kwa ufupi neno risk ukilitanguliza mbele utakufa bila kuishi malengo yako..verybad
Uko vizuri sana. Thanks kabisa na ujinga unaoitwa risk. Kila kitu ni risk. Kusoma. Kuishi. Kufa. Kuzaa. Kutembea. Kula biashara na vingine vyote. Ukiwa na degree unapata kazi utastaafu ukapata kiinua mgongo ukafungua biashara nayo ni risk. Hata ajira yenyewe ni risk. Tusiwatishe watu kuwa like ni risk very bad.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu habari zenu,. Mwaka 2014 nilihitimu kidato ya sita shule mojawapo nchini, nikafanya application kuingia chuo kikuu nikachaguliwa kwenda kusoma course ya uchumi pale udsm.

Kwa bahati mbaya sikupata mkopo kutoka HESLB kwa ajili ya kuniwezesha kupata elimu hiyo ya juu,

Nikatazama nyuma na mbele nikagundua sina support kutokana na umasikini uliokithili ndani ya familia yangu,

Baada ya hapo nikachukua maamzi magum, nikasafiri kutoka mkoani mpaka jijini na nikafuta na kufuta kabisa mawazo ya hiyo elimu ya chuo kikuu kwanza kwenye ubongo wangu.

Mawazo yangu na bongo langu nikahamishia kwenye neno "ajira" nikaanza kutembeza bahasha la vyeti vyangu ya secondary kutafuta ajira hapa mjini, hata hivyo sikuweze kupata ajira baada ya kuzunguka sana na bahasha hapa jijini,. Baada ya changamoto hiyo ikanifundisha tena kubadili mawazo kutoka kutafuta ajira mpaka kutafuta "mtaji" ili nijiajiri, nikiwaza ni jinsi gani niachane na suala la kutembeza bahasha kila ofisi naonekana kama bango,

nikaamua kukusanya kamtaji kwa kuanzia na kale kale ambako nilikuwa nazunguka nako kutafuta ajira nikapiga vibarua vya hapa na pale, nikasaidia sana mafundi site mbalimbali, nikapata kamtaji, nikaachana kwanza na vibarua nikaanzisha biashara fulani.

kwa sasa biashara yangu hiyo inanilipa faida tasilimu ya shilingi laki mbili kila mwezi, na mpaka dakika hii nimeweza kukusanya ada ya kuweza kujilipia university nchini.,

Je niende chuo au niendelee na biashara yangu hii.

NB nikimuachia mtu kuisimamia hii business lazima ife ndani ya muda mfupi sana maana inahitaji kujitoa sana. Japo kulingana na hela niliyonayo cash lazima chuo nimalize bila wasiwasi kabisa..

Naombeni ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo laki mbili ni baada ya kulipa mshahara? Kama vipi tafuta "online courses " lakini ni ghali zaidi ya vyuo vyetu na utahitajika uwe na Internet stable
 
STK labda nchi nzima ziko 500 tu,halafu kila mwaka wanaohitimu vyuo wako 400,000.kwa mliofaulu hesabu piga probability ya kutembelea stk hapo...

Nimekuelewa sana A2G



probability ya kutembelea STK ni 0.00125. Na hiyo ni kwa wale wanaomaliza mwaka mmoja tu, je ukiunganisha na wa miaka mingine si inakuwa balaa.
 
Najuta kupoteza muda kusoma chuo bora uwe na mtaji ufanye biashara kuliko kuwa mtumwa wa mtu.
 
Kubabake yani ukienda Chuo ukaacha Project zako nitakuona bonge la Fala... Ms***nge.
Usifanye huo ujinga.
Chuo ni kupoteza muda.
Mimi Nina Degree tena First class ya UDSM. Niulize Nina nini cha maana.
Daaah mkuu imenitouch asee...

Mi najuta asee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe mkuu upo pazuri sana kuajiriwa sio kuzuri ni utumwa tu, mi mwenyewe kuna mtego wa 30m nikifanikiwa kuzipata ntakuja kuwaomba ushauri nizifanyie nn ili ninyanyuke kibiashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bill gate aliondoka havard akiwa na 19 na amerudi kusoma akiwa na 60 tena tajiri wa dunia na hata huyu atarudi chuo akiwa ameshatoboa.......huyu sio mjinga.. huyu ni form 6 leaver.. tena aliyefaulu na kuchaguliwa udsm inshort sio kilaza...

kufaulu form 6 ni ngumu kuliko kupata degree kwa vyuo vingi....

so huyu anatakiwa apate elimu practical kwenye biashara yake maana hana ndoto za kuajiriwa...

masomo ya vyuo vikuu akiamua anajisomea hata kwa kusikiliza lecturez youtube kila siku...

elimu ni knowledge sio cheti

Huwezi kureplace elimu na pesa. Kuna watu wanafanya biashara wana pesa za kutosha lakini Maisha wanayoishi yanasikitisha. Usiache biashara. Ingia open university. Hata dropouts kama kina bill Gates waliona sababu ya kurudi Shule.
Hongera na Kila la kheri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sahihi kabisa mkuu. Kwani hiyo unamshauri asome elimu YA chuo kikuu youtube? Mimi nilishauri asome open university, Unaona youtube ni Bora zaidi sio? Manake biashara yake inamuingizia kipato cha kutosha kabisa.

(Halafu kusoma na kufaulu shule sio kutokuwa mjinga. Mukulu ameteua mawaziri wenye PhD na Kasema kitu kama vile ni wapuuza flani hivi).
huyu sio mjinga.. huyu ni form 6 leaver.. tena aliyefaulu na kuchaguliwa udsm inshort sio kilaza...

kufaulu form 6 ni ngumu kuliko kupata degree kwa vyuo vingi....

so huyu anatakiwa apate elimu practical kwenye biashara yake maana hana ndoto za kuajiriwa...

masomo ya vyuo vikuu akiamua anajisomea hata kwa kusikiliza lecturez youtube kila siku...

elimu ni knowledge sio cheti


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom