Biashara za mitandao (kuunganishana) zinavyowaliza first year vyuoni

Qnet ni mwendo wa kupigwa tu, na ukipigwa inabidi ukomae na wewe kutafuta wengine wa kuwapiga.

Good morning!!!!
 
Hawa ni kukaa nao mbali kabisa
Hao jamaa wa aina zote kuanzia GNLD, Qnet, Forever living etc wamenikaribisha, nimeshawahi kushawishiwa na watu wenye elimu na nyadhifa nijuliunge, ila issue moja in common niliona ni kuwa HAWAKUAMBII SPECIFICALLY unalipwaje.

Niliwashukuru na kuwaambia "waendelee" kutajirika mimi WANIACHE TU na ninacho pata kwa means zangu ambazo zinaeleweka![emoji23][emoji23]
 
Duh [emoji2811]
Soon na wewe utakuwa muhanga wakitaka na wewe ujiunge, na naamini utaleta mrejesho hapa.
Aaah wapi mkuu mimi hawatanipata🤣🤣🤣,

Ila nilitaka kujua tricks zao hasa ziko wapi ili nikiongea na shemeji yangu na sister wangu niwape facts za ubaya wa hiyo network business
 
Kuna jamaa alinishawishi nijiunge , nikamchana live mi borntown kitambo hizo mambo ni ujanja ujanja tu akadai we ngoja uone baada ya muda fulani nitakuwa napiga hela za maana. Nikamjuza time will tell, sasa ushapita mwaka na ushee kila tukitana ana sura ya majonzi tu
 
Dah! Wanawaibia kirahisi sana, halafu sijui ni matumaini ya maisha mazuri au kutajirika kwa njia za mkato maana dau wanaloanzia ni kubwa.

Halafu wanawa target watoto waliotoka familia za kawaida na sio za matajiri. Wazazi wa hao watoto wanajikamua sana wakidhani wanawatengenezea watoto wao maisha kumbe kipigo
 
aisee,,pole sana.mwambie dada yako Na wewe mwenyewe mtafute taarifa kuhusu 'pyramid scheme'..mtaelewa kila kitu.
hakuna biashara hapo
 
 
Kimsingi kila mtu ajue hakuna utajiri kirahisi rahisi. Wote tukatae hizo biashara za network marketing. Pia kuna hao wanaojiita LIFE COACHES hawako mbali na huu upuuzi wa network marketing.
 
Wengi tuliponda ile kitu inaitwa Bitcoin...any way kuna mtu mmoja amenisanua kuhusu S Block uzuri ama bahati mbaya app imekataa kufanya kazi kwenye Simu yangu.
 
Mimi huwa hata siwapi dk 1 yakuwasilikiza mataepeli Wakubwa hao
 
Wakati namaliza chuo ndio hizi biashara zilikuwa zinaingia kwa kasi na vile tulikuwa tunasomea afya waliteka sana watu pale chuoni

Katika maisha haya nimejifunza kuwa na makini sana na pesa yoyote inayoonekana kupatikana kirahisi.

Ukitoa sports betting za mipira hii ndio njia ambayo mtu anaweza kupata million mia na kuliwa million mia kwa dakika [emoji23][emoji23]

Jamaa alikuwa ananilazimisha kuniuzia dawa ya meno ya aloe vera mara sijui sabuni mara sijui biashara inalipa sana nikajiunge

Aliishia kunichunia na kuona sitaki kumpa sapoti katika maendeleo yake
 
"[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] acha tuu mzee kuna siku jamaa alinichota kumbe ni qnet banaa, sasa nkashangaa nimefika mchanaa lakini salamu zinazoendelea pale ni goodmorning tuuu"

 
Hivi mpk unaibiwa kiboya Hivyo inamaana hujifikirii...
 
Jaman mm nimebakia tu kujiunga na ALLINCE IN MOTION GLOBAL na anaenshawishi ni class mate wangu nliegraduate nae. Ananambia iko poa sana na nimehudhuria semina na mafunzo yao kibao na bidhaa zao nazijua A - Z asa nlikosa pesa tu mana ada yao ni laki 5. Jaman mpaka saiv anaendelea kunshawishi ila ni pesa tu sikuwa nazo, jaman hebu anaefaham kidogo pia nae aniokoe hapa nsitumbukie.
 
Anauza mifuko ya cement?
Kunaa jamaa angu nusu aniingize king q net alinipa had crown nitest kumbe sio yake et mambo ya qnet leo hii anauza mifuko yaaan yule jamaa stamsahau
 
Hivi unaweza kujua kabisa kua ni wapigaji na ukaingia kwenye ofisi zao usichomoe.
Kwa mfano kwa tahadhari hii tuliyopewa hapa halafu nikaamua kwenda kujionea mwenyew kwenye hizo ofisi zao huku nikiwa najua kabisa sina nia ya kujiunga,inawezekana humo ndani mm kubadili maamuzi kweli?
 
Nilifanyiwa hivi tena classmate wa 4yrs! Alinipangia timu km ya mtu 6 zenye high convincing power! Kosa lao ni pale waliposema Alhamis niende tena!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…