Biashara za mitandao (kuunganishana) zinavyowaliza first year vyuoni

Saa 11 jioni niliskia watu wanasemaw GOOD MORNING uchochoro mmoja hv baada ya HESLB
 
Mkuu, wake up! Hao ni matapeli, watakupa maelezo ambayo kama huna ufahamu mkubwa utawaamini, tapeli anachotafuta ni wewe kumuamini.

Mwambie shemeji asithubutu kwa namna yoyote ile kuweka pesa zake humo.
 
Hiyo 200USD unaipata kwa wiki au mwezi?
 
Hizi mambo zilinikosanisha na watu..
Mimi niliungwa nikatoa pesa yangu. Na mimi nikatafuta wanyonge wangu watano nikawaunga wakanipa pesa.
Sasa tatizo likaja pale kwa wale watano niliowaunga wao wakakosa watu..

Baada ya muda wakaona mimi ndo tapeli nimewapiga wakaanza kunidai..
Mimi mwenyewe siwezi kuwapa pesa yao sababu na mimi niliungwa nikatoa pesa
Inamaana ningelipa mimi ndio ningekula loss.

Basi nikawa mbuzi tu sikuwalipa.. waliniandama kinoma lakini mwisho wa siku wakabaki kununa tu na hela nikaitafuna.

Baada ya hapo nikisikiaga mambo ya biashara za hivyo huwa hata siwasikilizi na wakikomaa nawatukana kabisa
 
Wewe kwa sbb ushapata ABC hawatakuweza! Utakuwa unawaenjoy tu! Mf unaweza kuwaambia wakukopeshe hiyo 5m afu utakuwa unawalipa kidogo kidogo kutoka ktk bonus zako! So msmamo wako unabaki hapo hapo!
 
Daaah, kuna jamaa yangu akinusurika na hii ishu, nikipata muda mzuri nitaeleza hapa.
 
Mkuu, wake up! Hao ni matapeli, watakupa maelezo ambayo kama huna ufahamu mkubwa utawaamini, tapeli anachotafuta ni wewe kumuamini.

Mwambie shemeji asithubutu kwa namna yoyote ile kuweka pesa zake humo.
Asante sana mkuu kwa ushauri. Actually baada ya mjadala wa jana hapa JF na kusoma maoni kutoka kwa watu tofauti nimeshampigia simu shemeji yangu nikamwambia astop kwanza then nitaongea nae kwa kirefu baadae
 
Hayo makitu wanapatikana sana wanachuo washamba washamba ambao wameingia mjini mara ya kwanza baada ya kujiunga chuo kikuu

Na wanafocus kwa wanachuo lwasabab wanajua wanahela za boom laki tano tano kila baada ya miezi miwil na wengi huwa ni washamba wa mji na ni washamba wa kupata hela kwa mkupuo

Kuna jamaa mmoja tulisoma nae chup ametokea Tandahimba ndani ndani huko, sijui ilikuwaje akaingia king kwa hao Alliance In Motion Global, yani yule jamaa ilikuwa kila boom likiingia tu moja kwa moja analitoa lote analipeleka Alliance, ilifikia kipindi hadi anakosa hela ya kula anakuja kugongea msosi magetoni kwa washikaji

Ilifikia kipindi ikawa anatoa boom lake lote na anakopa nyingine kwa washkaj kwa kuwaahidi malipo kede kede, ilifikia mda had UE alikuwa anashindwa kufanya kutokana na kutokulipa outstanding dues, alikuaa anafanya special exams na alikuwa hashikiki hata kidogo, ukitaka mgombane mwambie kwamba izo ishu hazifai

Yan hadi tunamaliza chuo yule jamaa alikuwa na madeni yakutosha na sijui kama alifanya hata UE ya mwisho,
 
Binafsi hii biashara ipigwe marufuku..... Ni ya hovyo kabisa..... Inafanya watu wawe wavivu wa kufikiri kwa kujengwa na ndoto zisizotekelezeka. Kuna jamaa yangu alibandika sebuleni kwake Picha ya jumba kama hekalu na magari ya maana Bentley Ferrari VX V8 kuwa atakuwa nayo ndani ya miezi Sita na kazi Ata acha. Hadi Sasa Ana baiskeli tu..... Nayo ni ya mtumba.....
 

Kuna mdogo wangu anasoma SUA (mwaka wa kwanza) na mwingine Muhimbili (mwaka wa kwanza pia) nao wamelipia hizo online degree kwenye hicho chuo cha Malaysia, kuna siku walinipeleka huko kwenye QNet yao. Looh ni balaa tupu, sijui watu wanawezaje kudanganyika kirahisi vile na kuziingiza familia katika mizigo mizito ya kulipia gharama kubwa za masomo.

Nakumbuka mistari michache ya Fid Q isemayo:, ni mbaya kuhifadhi fuvu la kichwa cha mtu kwenye kabati, ni mbaya zaidi kuwa na ndugu halafu ni kichwa maji.
 
Hiyo 200USD unaipata kwa wiki au mwezi?
Sio Kwa mwez, ukiingiza hao watu ukapewa hyo ndo imetoka hvyo, cha msingi hao unaowaingiza wanatakiwa wapige kazi ya kuleta watu , na Wale wanaowaingiza na wenyewe wapige kazi kuleta watu, wakileta na wao watapata commission Yao na wewe utapata commission Kwa kila member anayeongezeka kupitia chain yako, wakat wanaingiza na we unapambana kuingiza kingi wengine ili chain iwe kubwa, Ila mara ya Kwanza sharti uingize watu wawili Kwanza do upate us dollar 200 na chain yako iwe activated, yaan kiufupi ili chain yako iwe activated zinatakiwa million 15 , ya kwako M5, na za maboya wengine wawili M 10, in return unapewa Dollar 200, na kazi inabaki kwako sasa kutengeneza chain sio kazi rahsi hata kidogo, labda uwe umezungukwa na middle-class people, kuna Mwamba wangu mmoja anaitwa Eliya Mroso tulipiga naye school Galanos Tanga, kampuni ya Qnet ilipoingia Tu nchini akajiunga fasta akaacha na chuo IFM, sa hv ni millionare mkubwa Sana and he is only 26yrs, advantage yake member karbia wote wa Qnet nchi nzima amekula commission zao , Ila wanaojiunga sa hv ni kimbembe kutoboa
 
Mimi nilikoswakoswa, jamaa yangu aliniambia ukiweka M10 utapata faida kubwa na kwenye maisha yako hutonisahau. Lakn hadi leo yeye ni bodaboda. Huwa najiuluza nisingemsahau kwa hasara aliyonipa. Juz juz anakuja nimuazime kilo 1.
 
Hahahaaa shemeji yangua alienda pia hapo kwenye ofisi yao Sinza. Anasema ni nyumba ipo ndani kidogo na hakuna hata fenicha sasa sijui wanasomaje

Anasema wale watoto kama wamelishwa imani flani hivi ya kimaigizo na hawajielewi. Ukiingia wanakuja wote wanazunguka mduara qanakusalimia Good morning hata kama ni saa nane mchana, kisha wanaanza kukueleza ABC za hayo mambo yao lakini hadi mwisho huelewi kitu

Wanakuingiza kwenye chumba kingine na wanakuja wanafunzi wengine eti wanakupa darasa tena ya hizo products. Kifupi yeye wameshamliza 4.5 za hiyo ada ya mwanae lakini baada ya mimi kuongea nae na kumueleza wasiwasi wangu, hawezi tena kupeleka hata shilingi huko,kwanza anahisi itampotezea concentration mtoto wake kule UD
 
Mimi nilikoswakoswa, jamaa yangu aliniambia ukiweka M10 utapata faida kubwa na kwenye maisha yako hutonisahau. Lakn hadi leo yeye ni bodaboda. Huwa najiuluza nisingemsahau kwa hasara aliyonipa. Juz juz anakuja nimuazime kilo 1.
Inamaana kuna mtu mahali flani anafaidika ja hizo pesa hao wengine wanabaki kupiga debe tu
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Hapa unanikumbusha jamaa alipotaka nijiunge DECI wakati huo maana ingekuwa sio imani yangu kunikataza nami ningekuwa miongoni mwa walioliwa noti zao
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…