Bibi harusi mtarajiwa, mama yake wafa ajalini wakielekea Kilimanjaro kwenye maandilizi ya harusi yake

Imani za hivi huwa sizikubali.Sasa km Maagano yanakuwa na nguvu kuna Sababu gani ya Kumpokea Yesu?,Ina Maana Kazi ya Yesu Kristo kufa msalabani ni ipi sasa?.Huu upuuzi waambie wasiojua nguvu ya Msalaba wa Yesu na damu yake aliyoimwaga msalabani.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Inaumiza sana wapumzike kwa amani , this is so devastating
 
Unakwepa shimo kuzuia boll joint isiharibike unalenga uso wa lory. Dereva wa masafa wanaelewa kilichotokea hapo

Serikali imeendelea kusisitiza Ukiwa na Gari yako unayotumia huku mjini Siku ya Safari kodisha Dereva akupeleke . (Udereva ni professional) Ni zaidi ya kulenga Barabara
Kuna saa unatakiwa ufikiri na upate majibu sahihi Ndani ya nusu sekunde Kati ya kuharibu boll joint Ambayo ungeenda Kwa fundi kubadili Kwa 25000 Au ulenge lory usoni ufe

Huyu alikosa Driving skills

KIROHO:
Huyu mtu amepata mume na 37 years. Unajua kwa nini alikaa muda wote huo?
Sababu zingine ni kwamba kuna watu walinenewa hawataolewa ..akilazimisha sana
Kuna Roho inaitwa kisasi Kama hajui vita vya kiroho Ndio itammaliza

So tunaweza kumuona alikuwa si Dereva mzuri ila amekoseshwa. Ulimwengu wa roho ni very technically. Ndio maana Mungu anafundisha watu wake maarifa ya rohoni. Wakolosai 1:9
Mtume Paulo anasema na Ninanukuu
Tangu tuliposikia hatuachi kufanya Dua na maombi Kwa ajili yenu Ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake Katika Hekima yote na ufahamu wa Rohoni .

So ukikosa ufahamu wa Rohoni Hutajua wakati sahihi Ni ipi wa kufanya jambo Au wakati sio sahihi ni upi usifanye Ndio maana mwisho ni hasara Kwa wengi.

Poleni wafiwa wote Mungu awape faraja.
WOKOVU NI SASA BAADA YA KUFA NI HUKUMU.
Usipoteze muda kumuombea mtu akifa Eti awekwe pema peponi Hiyo si kazi yako
Ibada ya mazishi ni Kwa ajili ya walio hai basi.
 
Akishajua kuendesha siku anasafiri nalo anakimbia hajui barabara vizuri pia bumps ziko wapi...hamadi bumps anapaa nayo mnamkuta juu ya mti
Mtihani wa safari ni kupishana na kupita magari na kujua kona zenye madhara basi wengine wanafata sana mistari ya Tanroad pana sehemu nilipita mstari wa Tanroad unaruhusu kupita gari ingine karibu kabisa na daraja na huko Njombe kwenye Kona niliona mstari unaruhusu kuyapita magari mengine na mbele kuna kona huoni kitu hapo unatakiwa ujiongeze usisema mstari unaruhusu kwa hiyo bara bara inaongea yenyewe uendeshe vip gari yako...
 
Kusafiri kifamilia kwenye usafiri mmoja wa binafsi ni kujiweka rehani hasa katika safari za mikoani kwenye barabara za Tanzania.
Unafikiri mkisafiri kwenye buss ndo hamtapata ajali, hizi fikra kama zako huwa napigana nazo sana tu, hata mkipanda ndege moja kama zimefika zimefika tu,
 
Unafikiri mkisafiri kwenye buss ndo hamtapata ajali, hizi fikra kama zako huwa napigana nazo sana tu, hata mkipanda ndege moja kama zimefika zimefika tu,
Ajali nyingi zinasababishwa na uzembe na barabara mbovu
Kama mtu huna uzoefu panda public transport. Mabasi mengi pia yana madereva vichaa ndio maana ajali nyingi.
 


Wanawake mthihan sana, Ma bus siku hizi yamejaa, mazuri, una relax, stress za kuendesha za nini?
 
Ni Kweli mkuu,siku ya kwanza mimi niliendesha gari kutoka Tunduma (Songwe) hadi Njombe maeneo ya Ludewa aisee sitasahau siku ile Yaani nilisali sana kuomba Mungu aniongoze,na nilijitahidi kwa Msaada wa Mungu kufika kule lkn nilikuwa nimechoka sana.

Na hapo ulikuwa na kipande kibaya cha Mbeya - Igawa, kina barabara mbaya ina mashimo na matuta ya lami kufimba karibia sehemu nyingi...

Kingine ni kile cha Makambako - Njombe kuna baadhi ya maeneo kuna vipande vibaya vya barabara...
 
Yaani Tena barabara ya Kondoa ilivyo na Kona Kona mweee acha kabisa,ukimaliza Kondoa km unaelekea manyara kuna Kona Kali Fulani hv pale mweee acha tuuu
Inataka umakini sana kama hautaki kuzama korongoni
 
Kuna sehemu nimesoma kuwa alikuwa anaenda kuolewa uke wenza kuwa mume aliacha kuoa ndoa na aliyekuwa naye akambwaga akaamua aoe huyo Sina uhakika kama ni kweli au la nilisoma tu mitandaoni maana mitandao habari zote za uongo na kweli pia huwemo
Inaweza kuwa kweli maana kwa umri huo aliokuwa nao bibi harusi mtarajiwa si rahisi kupata mme ambaye hajawahi kuoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…