Sol de Mayo
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 6,515
- 6,230
إنا لله وإنا إليه راجعون
Allah awape subra wafiwa
Allah awape subra wafiwa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi kuna kipindi nilikuwa naota ndoto za ajabu na kutisha, kumbe kulikuwa na mtu nyuma ya pazia, ila alichokipata hata kaa asahau. Ila maombi ni muhimu sana.Watu Kuna vitu Huwa wanavichukulia poa sn!
Wanasahau kuwa U/Roho ndo halisi na ndo msingi wa Kila kitu na hakuna kitu Cha ghafla,mipango yote rohoni.
Yaani red flag za mwilini watu wanazielewa sn ingekuwa na rohoni hivyo tungekuwa mbali sn.
Km Kuna eneo Lina vita na miungu inapigana sana ni hili la ndoa(kuoa/kuolewa),🙌🙌!
Na Kuna baadhi ya Koo, kabila nomaa
Yaani Tena barabara ya Kondoa ilivyo na Kona Kona mweee acha kabisa,ukimaliza Kondoa km unaelekea manyara kuna Kona Kali Fulani hv pale mweee acha tuuuKuna siku wife alikuwa anaenda Arusha kutokea Dom apite road ya kondoa. Nikamwambia ni bora kupanda bus akakaza anataka aende na gari atumie kwenye mizunguko ya hapa na pale akiwa chuga. Hakutuboa kwenye zile kona ni siku yake haikufika tu.
Hizi road zinataka ujuzi wa barabara sio kujua kuendesha gari tu
Watu wanajifanya wabishi ila uchawi upoo na watu wanaroga na kurogwa haswaa..hapo ukute kati Yao Kaacha mtu kampotezea muda kaenda kuoa kungine we Unadhani nini kitatokeaHivi uwa ni kwanini?
Kuna hii harusi ya mtu wangu wa karibu..
Sendoff imefanyika ikaisha salama.
Bwana harusi anarudi mkoa wake kusubiri siku ya harusi wakapata ajali njiani….. akavunjika mkono na yeye peke ake ndiye aliumia ktk hiyo gari…hapakuwa tena na sherehe, ila Mungu ni mwema akapona kiasi ya kutosha kufunga tu ndoa Kanisani na kupiga picha akiwa na pop yake mkononi 🥹
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Watoto wa Mama ndio wanapenda kusema mambo ya umri, kwa kifupi ndoa haina umri, waswahili tuna shida sana , tushazoea kuona vitoto vikioana.
Aisee, shukuru Mungu ulikuwa unaelewa taarifa hiyo kupitia ndoto!Mimi kuna kipindi nilikuwa naota ndoto za ajabu na kutisha, kumbe kulikuwa na mtu nyuma ya pazia, ila alichokipata hata kaa asahau. Ila maombi ni muhimu sana.
Nilikuwa naota kila siku, nikajisemea hii ni tahadhari ya Kiroho.Aisee, shukuru Mungu ulikuwa unaelewa taarifa hiyo kupitia ndoto!
Ni kweli bila kuomba Mungu ni balaa
Pole kwa wanafamilia[emoji174]
Bibi harusi mtarajiwa, Rehema Chao (37) na mama yake mzazi, Agness Chao (75) wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Raum kugonga lori.
Ajali hiyo iliyotokea baada ya Rehema aliyekuwa dereva wa gari hilo kukwepa shimo na kugongana na lori, pia imesababisha kifo cha mfanyakazi wa ndani wa mdogo wake, Irene Shija (15), huku wanafamilia wengine wawili wakijeruhiwa.
Ajali hiyo ilitokea jana Novemba 28,2023 katika eneo la Kichwa cha Ng'ombe, wilayani Mwanga, wakati Rehema akitokea mkoani Morogoro kwenye sherehe ya kuagwa (send-off) iliyofanyika Novemba 24,2023.
Rehema aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Sua, mkoani Morogoro alikuwa akirejea nyumbani kwao Marangu, Moshi akiambatana na familia yake kwa ajili ya maandalizi ya harusi iliyopangwa kufungwa Desemba 2,2023 mkoani Arusha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alithibitisha ajali hiyo akisema wanamshikilia dereva wa lori, Joachim Meela (37) kwa mahojiano zaidi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Abdallah Mwaipaya, amewataja majeruhi kuwa, Veronika Chao (35), mdogo wa Rehema ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Nguzo Mbili, Geita na mwanaye, Jayden Erasto (2).
"Jana kulitokea ajali katika wilaya yetu ya Mwanga, iliyosababishwa na magari mawili, lori aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na mkazi wa Moshi likitokea Arusha kwenda Dar es Salaam lililogongana na Toyota Raum likitokea Morogoro kwenda Marangu,” amesema.
Mwaipaya amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Kituo cha Afya Kisangara, wilayani Mwanga, huku majeruhi wakiendelea na matibabu katika kituo hicho.
Ndugu, marafiki wanena
Ndugu wa marehemu, Elielisa Kombe ameiambia Mwananchi Digital kuwa, harusi ya Rehema ilikuwa ifanyike Oldonyosambo, mkoani Arusha.
Kombe amesema gari lililokuwa na watu watano wa familia moja, wakazi wa Msae Nganyeni, Marangu lilipata ajali wakati Rehema akikwepa shimo.
"Gari lilikuwa na watu watano, mama na watoto wake wawili, mjukuu na msichana wa kazi, ni majonzi makubwa kwa familia," amesema Kombe.
Amesema wamepanga maziko kufanyika Jumamosi, Desemba 2,2023. Amesema wanaendelea na vikao kwa kuzishirikisha pande zote mbili.
"Tunaendelea na vikao kwa sasa, kesho ni lazima tukae pande zote mbili, upande wa waoaji na sisi, lakini tunatarajia kuzika Jumamosi," amesema.
Happyness Msacky, mwalimu mwenzake na Rehema katika Shule ya Sekondari Sua, amesema wamepokea kwa masikitiko msiba huo.
Amesema walikuwa wote siku ya sherehe wakifurahi pamoja na mtumishi mwenzao.
"Msiba huu umetuuma sana, Rehema alikuwa na familia yake, yeye ndiye alikuwa dereva. Hili ni pigo kubwa kwa familia, hatuna cha kusema zaidi ni kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu," amesema.
Mwananchi
soma vuzuri habari, huyo mtoto sio wa kwake ni wa mdogo wake aliyekuwa nae kwenye gariHalafu Bibi hharusi ana mtoto wa miaka 2
Rudia kusoma basiHalafu Bibi hharusi ana mtoto wa miaka 2
Itakua alikata kona zile za kolo kwa speed halafu sio mzoefu ...gari ikamshindaKuna siku wife alikuwa anaenda Arusha kutokea Dom apite road ya kondoa. Nikamwambia ni bora kupanda bus akakaza anataka aende na gari atumie kwenye mizunguko ya hapa na pale akiwa chuga. Hakutuboa kwenye zile kona ni siku yake haikufika tu.
Hizi road zinataka ujuzi wa barabara sio kujua kuendesha gari tu
Akishajua kuendesha siku anasafiri nalo anakimbia hajui barabara vizuri pia bumps ziko wapi...hamadi bumps anapaa nayo mnamkuta juu ya mtiMwaka huu nilikua natoka Chuga naenda Mbeya pana sehemu maeneo ya Kondoa kwenye zile kona pana jamaa alikua anatupita kama yupo bara bara za mjini tuliposimamishwa sehemu bara bara ilikua inajengwa alikua na Harrier na mwingine alikua na ICT nikawaambia hizi bara bara za vumbi msiende mwendo kasi sana zina tabia ya kuvuta gari wote walishukuru sana baadae nikaikuta ile gari imepata ajali kwenye zile kokoto wanazomwaga wakisubiri waweke lami tukiitafuta mtera niliumia sana maana gari ilijifinyanga kama karatasi nilikua na mzuka wa kufika mbeya siku hiyo hiyo nikaenda kulala Iringa yaani watu ulioongea nao muda si mrefu unakuta wamepata ajali na kufariki inaumiza sana kwa kweli ila naona wengi wakinunua magari wanalazimisha kuwa madereva wakati huo huo...unakuta mtu hajui gari kabeba familia yote ndani yaani likitokea lolote kizazi kinaisha..
Unapotangaza kuoa tu tayari kuna signal inakwenda kwenye ulimwengu wa roho na wako watu hawatafurahia hilo. Hila zinakuwa nyingi maana kuna milango ya baraka hufunguliwa baada ya ndoa kufungwa tu. Mtajaliwa watoto ambao nao wanakuja kufungua milango ya mafanikio yenu zaidi hapo ndipo shida huanzia.Hivi suala la ndoa nalo linakuaga na changamoto za ajabu ajabu kumbe duuh
Sasa suala la ndoa ni la kumuonea mtu wivu na kumtakia mabaya kweli hatari sana
Ni Kweli,haikupaswa Bibi Harusi Mtarajiwa aendeshe gari,bora wangetafuta dereva wa kumlipa ambaye ni mzoefu.Udereva wa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine sio kama town trip. Pole kwa wanafamilia kwa msiba mzito sana Mungu awape faraja wafiwa na marehemu wapumzike kwa amani.
Mbona unafika mbali sana mkuu?.Ujue mimi namzidi bibi Harusi mwaka mmoja kwa hiyo na mimi ni mzee?.Bibi harusi ana miaka 37, halafu house girl ana miaka 15.
Bibi harusi mzee, house girl katoto. Wapumzike kwa amani
Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Ni Kweli mkuu,siku ya kwanza mimi niliendesha gari kutoka Tunduma (Songwe) hadi Njombe maeneo ya Ludewa aisee sitasahau siku ile Yaani nilisali sana kuomba Mungu aniongoze,na nilijitahidi kwa Msaada wa Mungu kufika kule lkn nilikuwa nimechoka sana.Salamu za pole kwa wanafamilia...
Wito:
Madereva wasio wazoefu wa safari ndefu za mkoa hadi mkoa si vyema kusafiri kwa kuendesha gari mwenyewe...
Hizi safari ndefu huwa zinahitaji umakini sana na muda wote akili inapiga kila aina ya hesabu uwapo barabarani kuepukana na majanga...
Kudance na mashimo barabarani kama sio mzoefu unaweza hata ukapindua gari au ukachochora...
Kha!kha!,Mmeanza kuchokonoa mambo.Apumzike kwa amani tu.
Nilitaka kujua imekuaje bibi hharusi wa miaka 37
Mmeshaanza hbr zenu za maagano,ila Waafrika wakikalilishwa Jambo kila kitu watahusisha na kile walichokalili.Hebu fikiri nje ya kisanduku.Hapa inaonyesha ana agano la kutokuolewa...
Hilo agano ndio limeondoa uhai wake...
Vita baada ya kupata...