Bibi harusi mtarajiwa, mama yake wafa ajalini wakielekea Kilimanjaro kwenye maandilizi ya harusi yake

Bibi harusi mtarajiwa, mama yake wafa ajalini wakielekea Kilimanjaro kwenye maandilizi ya harusi yake


Bibi harusi mtarajiwa, Rehema Chao (37) na mama yake mzazi, Agness Chao (75) wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Raum kugonga lori.

Ajali hiyo iliyotokea baada ya Rehema aliyekuwa dereva wa gari hilo kukwepa shimo na kugongana na lori, pia imesababisha kifo cha mfanyakazi wa ndani wa mdogo wake, Irene Shija (15), huku wanafamilia wengine wawili wakijeruhiwa.

Ajali hiyo ilitokea jana Novemba 28,2023 katika eneo la Kichwa cha Ng'ombe, wilayani Mwanga, wakati Rehema akitokea mkoani Morogoro kwenye sherehe ya kuagwa (send-off) iliyofanyika Novemba 24,2023.

Rehema aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Sua, mkoani Morogoro alikuwa akirejea nyumbani kwao Marangu, Moshi akiambatana na familia yake kwa ajili ya maandalizi ya harusi iliyopangwa kufungwa Desemba 2,2023 mkoani Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alithibitisha ajali hiyo akisema wanamshikilia dereva wa lori, Joachim Meela (37) kwa mahojiano zaidi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Abdallah Mwaipaya, amewataja majeruhi kuwa, Veronika Chao (35), mdogo wa Rehema ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Nguzo Mbili, Geita na mwanaye, Jayden Erasto (2).

"Jana kulitokea ajali katika wilaya yetu ya Mwanga, iliyosababishwa na magari mawili, lori aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na mkazi wa Moshi likitokea Arusha kwenda Dar es Salaam lililogongana na Toyota Raum likitokea Morogoro kwenda Marangu,” amesema.

Mwaipaya amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Kituo cha Afya Kisangara, wilayani Mwanga, huku majeruhi wakiendelea na matibabu katika kituo hicho.

Ndugu, marafiki wanena
Ndugu wa marehemu, Elielisa Kombe ameiambia Mwananchi Digital kuwa, harusi ya Rehema ilikuwa ifanyike Oldonyosambo, mkoani Arusha.

Kombe amesema gari lililokuwa na watu watano wa familia moja, wakazi wa Msae Nganyeni, Marangu lilipata ajali wakati Rehema akikwepa shimo.

"Gari lilikuwa na watu watano, mama na watoto wake wawili, mjukuu na msichana wa kazi, ni majonzi makubwa kwa familia," amesema Kombe.

Amesema wamepanga maziko kufanyika Jumamosi, Desemba 2,2023. Amesema wanaendelea na vikao kwa kuzishirikisha pande zote mbili.

"Tunaendelea na vikao kwa sasa, kesho ni lazima tukae pande zote mbili, upande wa waoaji na sisi, lakini tunatarajia kuzika Jumamosi," amesema.

Happyness Msacky, mwalimu mwenzake na Rehema katika Shule ya Sekondari Sua, amesema wamepokea kwa masikitiko msiba huo.

Amesema walikuwa wote siku ya sherehe wakifurahi pamoja na mtumishi mwenzao.

"Msiba huu umetuuma sana, Rehema alikuwa na familia yake, yeye ndiye alikuwa dereva. Hili ni pigo kubwa kwa familia, hatuna cha kusema zaidi ni kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu," amesema.

Mwananchi
Eeh Mungu, unajua haya, unatukumbusha maringo yetu yote, kujona tumepata, kutokuwa na shukrani, kudharau wengine, kutokukushukuru havisaidii, muda wowote pahala popote unatuchukua.
Think huyu mama miaka 75 amepitia mishale mingapi? amepitia mambo mangapi lakini sasa anakuja kufa dakika moja na mwanaye.
Fikiri huyu binti amekaa muda wote hana mume, hana mtoto sasa ameamua kuolewa.
 
Yaani watu Wana vituko humu,eti umri umeenda,sijui umeenda wapi na Kwa mujibu wa nani?
Wanachekesha!
Naona tuna mawakala wa vipimo humu😅

Kabisa unaweza Kuta jamaa mkubwa
Eeeh hiyo ni ndoa ya watu wazima, binafsi sioni shida. Tena hawa wanajitambua kabisa, mwanaume mwenye 40+ kuoa binti wa 20s ni kujitafutia matatizo tu.
 
Yaani watu Wana vituko humu,eti umri umeenda,sijui umeenda wapi na Kwa mujibu wa nani?
Wanachekesha!
Naona tuna mawakala wa vipimo humu😅

Kabisa unaweza Kuta jamaa mkubwa
Watoto wa Mama ndio wanapenda kusema mambo ya umri, kwa kifupi ndoa haina umri, waswahili tuna shida sana , tushazoea kuona vitoto vikioana.
 
Kwa tabia alizoonesha bibi harusi hiyo ndoa mwanaume alikuwa anakwenda kuteseka sana, wenye kuelewa watakuwa wamenielewa.

Kuna tabia za kike zinaeleweka, ukiona mwanamke anaamini kila anachofanya mwanaume na yeye anaweza kufanya muogope sana mwanamke huyo.

Mimi nina driving experience kwa zaidi ya miaka 20, Nina international driving licence, ila safari za city to city huwa napenda kuwa na mtu au siku hizi naenjoy zaidi mtu akiniendesha.
Daktari Mato....
 
Hivi uwa ni kwanini?

Kuna hii harusi ya mtu wangu wa karibu..
Sendoff imefanyika ikaisha salama.
Bwana harusi anarudi mkoa wake kusubiri siku ya harusi wakapata ajali njiani….. akavunjika mkono na yeye peke ake ndiye aliumia ktk hiyo gari…hapakuwa tena na sherehe, ila Mungu ni mwema akapona kiasi ya kutosha kufunga tu ndoa Kanisani na kupiga picha akiwa na pop yake mkononi 🥹
Acha tu yani yanayoendelea ulimwengu tusiouona kwa macho ni magumu sana. Watu wana roho mbaya sana na lile agano ni very strong kiimani. It transforms everything in life.
 
Hivi uwa ni kwanini?

Kuna hii harusi ya mtu wangu wa karibu..
Sendoff imefanyika ikaisha salama.
Bwana harusi anarudi mkoa wake kusubiri siku ya harusi wakapata ajali njiani….. akavunjika mkono na yeye peke ake ndiye aliumia ktk hiyo gari…hapakuwa tena na sherehe, ila Mungu ni mwema akapona kiasi ya kutosha kufunga tu ndoa Kanisani na kupiga picha akiwa na pop yake mkononi 🥹
Acha tu yani yanayoendelea ulimwengu tusiouona kwa macho ni magumu sana. Watu wana roho mbaya sana na lile agano ni very strong kiimani. It transforms everything in life.
 
Hata mie nimehisi hivyo, thinking deep kwenye ulimwengu wa roho kuna mambo yalikuwa tayari yanaendelea hata sisi tulishauriwa kuwa makini sana kuelekea siku ya tukio. Vita ni kubwa sana ukizingatia kuna ambao wanaweka ngumu ili usioe au kuolewa wanatumia njia yeyote ile ili mkwame tu.
Ni kwel Kabisa ,miez kadhaa nilikuwa nafunga ndoa ,mama yangu alipitia wakati mgumu sana kabla ya harusi ,aliona vitu vya ajabu ,mara kunguni wengi wakiwa wametanda Kwa net ,gafla wanapotea ,ila Alikuwaa akisali sana Ili harusi yangu ifanyike salama,ukizangatia mm wa kwanza home ,mambo ni mengi sana katika ulimwengu wa roho,tusali sana,na pia tuwashukuru wazazi na waombezi wetu wanao tuombea bila kujua.
 
Huyo mumewe nae alifeli wapi. Mkeo mtarajiwa anasafiri mkoa m'moja kwenda mwingine unakubaliana nae badala ya kumtafutia msaada wa mtu mzoefu wa kumuendesha morogoro kwenda Kilimanjaro sio safari ndogo hiyo especially kwa mwanamke, mwanamke hawezi kaza macho safari nzima lazima atatia boko.

Wanaume hebu muwapende wake zenu ikibidi kugombana lakini una uhakika kuwa utakachomuamuru kufanya ni kwa salama yake na ustawi wake, acheni kucheka na wake zenu kwenye mambo yanayotaka userious.
 
Back
Top Bottom