Bibi harusi mtarajiwa, mama yake wafa ajalini wakielekea Kilimanjaro kwenye maandilizi ya harusi yake

Pole sana kwa familia ya marehemu, pole kwa aliyekuwa mume mtarajiwa. Ni ngumu sana kwake.
Ila hapo kuna errors kadhaa;
...una mchecheto wa sherehe unapewa kuendesha long trip, na huenda umezoea kila siku 10-50km tu.
...unakwepa shimo ghafla wakati upande wa pili Lori linakuja, lack of experience, vaa shimo kwa namna yoyote coz tayari ushachelewa..
 
Nimeelewa vizuri naongelea kuhusu age, bi harusi umri umeenda sana (RIP) halafu house girl umri wake sio wa kuajiriwa ni mtoto sana alitakiwa kuwa shule
Umeenda sana kwa mujibu wa nani mkuu, mwanamke yupo umri wa kawaida kabisa, halafu huwezi jua, jamaa nae yupo labda 40s au 50s so it was a perfect match.
 
Kuna siku wife alikuwa anaenda Arusha kutokea Dom apite road ya kondoa. Nikamwambia ni bora kupanda bus akakaza anataka aende na gari atumie kwenye mizunguko ya hapa na pale akiwa chuga. Hakutuboa kwenye zile kona ni siku yake haikufika tu.
Hizi road zinataka ujuzi wa barabara sio kujua kuendesha gari tu
 
Mwaka huu nilikua natoka Chuga naenda Mbeya pana sehemu maeneo ya Kondoa kwenye zile kona pana jamaa alikua anatupita kama yupo bara bara za mjini tuliposimamishwa sehemu bara bara ilikua inajengwa alikua na Harrier na mwingine alikua na ICT nikawaambia hizi bara bara za vumbi msiende mwendo kasi sana zina tabia ya kuvuta gari wote walishukuru sana baadae nikaikuta ile gari imepata ajali kwenye zile kokoto wanazomwaga wakisubiri waweke lami tukiitafuta mtera niliumia sana maana gari ilijifinyanga kama karatasi nilikua na mzuka wa kufika mbeya siku hiyo hiyo nikaenda kulala Iringa yaani watu ulioongea nao muda si mrefu unakuta wamepata ajali na kufariki inaumiza sana kwa kweli ila naona wengi wakinunua magari wanalazimisha kuwa madereva wakati huo huo...unakuta mtu hajui gari kabeba familia yote ndani yaani likitokea lolote kizazi kinaisha..
 
Wazazi wengi wazamani hawakuwa na hekima kabisa
 
Umakini upi mlizingatia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…