TANZIA Bibi Susana Benjamin Mmary, binadamu aliyeishi miaka mingi zaidi Duniani kutokea Tanzania

TANZIA Bibi Susana Benjamin Mmary, binadamu aliyeishi miaka mingi zaidi Duniani kutokea Tanzania

Tutakuja kuamini umri huu tukiwekewa record za kanisani hapa(cheti cha ubatizo au register ya kanisani.Hakuna records zenye uhakika kama za wakatoriki.zina uhakika kuliko za government.
huyo Bibi Wala hana hiyo miaka waliyoitaja
 
Ooh, poleni sana
😥😥ooh bibi nitammiss Sana nakumbuka Ni Bibi aliekuwa mchesh siku zote anakumbuka u asikwambie mtu na siku zote mnajua Kama mtu akizeka Sana anakuwa Kama mtoto alikuwa anapenda tukimpelekea zawad

Na huyo mjukuu wake wa 78 anaemfata Ni babu yangu (rip) tulimzika mwaka Jana

Bibi alikuwa so funny na tulikuwa tunajivunia Sana alikuwa na watoto 9 wajukuu 92 vitukuu 300 Yan historia yake ilikuwa ndefu kwel tulimzika Jumamos na Kila mtu alikuwa na furaha hamna wakulia tuliimba tulifurah maana Bibi mwenyewe alikuwa anasema "jina lake limepotea kwenye vitabu vya mungu😄"vitukuu na vilembwe tulikiwa Kama wotee Yani

Na hakuwa anaumwa ugonjwa wowte Bali jumanne tuliamka na kukuta Mungu kampenda zaidi

Pumzika kwa amani Bibi suzan kwa jina maarufu Kama Bibi Mateti
 
Asante kwa taarifa hii muhimu na kwa kweli waafrika inabidi tujifunze kujua tunu zetu na kuzitangaza. Kuna mambo mazuri na makubwa sana Afrika ila tumeaminishwa kuwa vyakwetu havina maana, SIYO KWELI!
 
Kutokana na habari ya bibi Susana Benjamin Mmary, kuna watu wameuliza kuhusu taarifa za tarehe za kuzaliwa kwake zimepatikana wapi kutokana na ukweli kwamba wazee wengi wa zamani hawakujua miaka waliyozaliwa bali walitunza rekodi kwa kumbukumbu za matukio makubwa yaliyotokea wakati huo. Kuhusu bibi Susana rekodi zote zipo wazi. Hii sio hadithi ya kubuni.

Wakati wamisionari wa Kianglikana kutoka Uingereza wa shirika la Church Missionary Society (CMS) wanafika Tanganyika mwaka 1848 waliweka kituo chao maeneo ya Kitimbirihu (Moshi). Baada ya Berlin Conference mwaka 1984/85 Tanganyika ilipewa Ujerumani na hivyo Waingereza wa CMS wakaondoka kwenda Kenya na kupeleka injili huko maana Kenya iligawanywa kwa Waingereza.

Kwa kuwa Tanganyika ilipewa Ujerumani wakaja wamisionari wa Kilutheri akina Emil Mueller, Franz Boohme na Dr.Bruno Gutman kutoka Ujerumani. Wakahamishia kituo hicho cha misioni kutoka Kitimbirihu kwenda kijiji cha Kidia mwaka 1885. Hii ni kwa sababu kijiografia Kidia ndio ilikua katikati ya eneo lote la Old Moshi kuanzia Mbokomu mpaka Sango. Na hata jina "kiidi- aa" maana yake ni hapa ni katikati.

Kituo hicho cha kwanza cha uinjilishaji eneo la Kaskazini mwa Tanganyika kikaanza kutoa huduma za kiroho, akina Dr.Gutman wakihubiri neno la Mungu na kubatiza watu. Waumini wa kwanza kubatizwa eneo hilo ni Tomaso Ringo na Samueli Tenga waliobatizwa tar 21 Februari mwaka 1892. Miaka miwili baadae 1894 bibi Susana nae akabatizwa akiwa na umri wa miaka mitano.

Majina ya Wakristo hao wa mwanzo kubatizwa yametunzwa kwenye nyaraka zilizoachwa na wamisionari hao. Nimejulishwa na familia ya akina Mmary kwamba mwaka jana (2019) kitukuu wa Dr.Gutman alifika Kidia na alimtembelea bibi Susana ambaye alibatizwa na babu yake. Bibi Susana alimhadithia mambo mengi ya nyakati hizo za kale wakati injili inafika Afrika.!

Malisa GJ
 
Huyu bibi aingie kwenye Guinness World record book
 
[emoji26][emoji26]ooh bibi nitammiss Sana nakumbuka Ni Bibi aliekuwa mchesh siku zote anakumbuka u asikwambie mtu na siku zote mnajua Kama mtu akizeka Sana anakuwa Kama mtoto alikuwa anapenda tukimpelekea zawad

Na huyo mjukuu wake wa 78 anaemfata Ni babu yangu (rip) tulimzika mwaka Jana

Bibi alikuwa so funny na tulikuwa tunajivunia Sana alikuwa na watoto 9 wajukuu 92 vitukuu 300 Yan historia yake ilikuwa ndefu kwel tulimzika Jumamos na Kila mtu alikuwa na furaha hamna wakulia tuliimba tulifurah maana Bibi mwenyewe alikuwa anasema "jina lake limepotea kwenye vitabu vya mungu[emoji1]"vitukuu na vilembwe tulikiwa Kama wotee Yani

Na hakuwa anaumwa ugonjwa wowte Bali jumanne tuliamka na kukuta Mungu kampenda zaidi

Pumzika kwa amani Bibi suzan kwa jina maarufu Kama Bibi Mateti
Amen[emoji120]
 
Afrika tunashindwa mambo madogo sana, naamini huyu bibi hakuwa anajulikana baina ya watu wengi. Ilibidi tumtangaze sana, sidhani hata kama ana mahojiano ambayo yamechapishwa.

Apumzike kwa amani.

Nadhani ndugu hawakuona umuhimu wa hilo
 
... huyu bibi kule kwetu tungeshamkata shingo au kumchomea ndani siku nyingi sana maana tunaamini wanakuwaga wachawi! Jamani ndivyo tunavyoamini sisi usiniulize kwanini ndio imani yetu.
Ndio maana watu wengine wanakosa radhi
 
Wabongo banaa sijui tukoje.
Bibi alipokua hai hakuna aliehangaika kuufahamisha ulimwengu kua bibi yetu ndio binaadamu mwenye umri mrefu zaidi duniani kwa kipindi hicho, Ilya baada ya kufariki ndio tunaanza kusikia makelele kila kona.
Muacheni bibi apumzike kwa amani.
Hio rekodi haina yoyote kwake kwa sasa kama mlishindwa kumpogania kipindi akiwa hai.
Media za bongo wao news ni shilole kapata bwana mpya au Diamond karudiana na Zari wao ndio wanaona ni habari vitu vya muhimu hata hawavipi kipaumbele
 
Asante kwa taarifa hii muhimu na kwa kweli waafrika inabidi tujifunze kujua tunu zetu na kuzitangaza. Kuna mambo mazuri na makubwa sana Afrika ila tumeaminishwa kuwa vyakwetu havina maana, SIYO KWELI!
Media zetu hawataki hizi habari wao wakina millad Ayo wanapenda habari kama ile ya juzi ya yule mama aliyefumaniwa ndio wanaona ni habari
 
Shida maeneo mengi hakuna record za uhakika juu ya tarehe za kuzaliwa za hawa wazee lakini 100+ zinapigwa kama kawaida.
 
Wewe uliyefiwa na bibi tuwekee picha yake na historia fupi tuanze kumtangaza duniani.
 
Back
Top Bottom