TANZIA Bibi Susana Benjamin Mmary, binadamu aliyeishi miaka mingi zaidi Duniani kutokea Tanzania

TANZIA Bibi Susana Benjamin Mmary, binadamu aliyeishi miaka mingi zaidi Duniani kutokea Tanzania

Sherehe ya mwisho ya bibi Susana Benjamin Mmary imefanyika nyumbani kwake huko Old Moshi Kidia, baada ya BWANA kumuita akiwa na umri wa miaka 131. Ni bahati mbaya kwamba taasisi zinazotunza rekodi za dunia haziangalii sana Afrika, lakini kabla hajafariki alipaswa kuwa ndiye mwanadamu mwenye umri mkubwa zaidi (the oldest living person).

Dunia inamtambua Kane Tanaka wa Japan kuwa mwanadamu mwenye umri mkubwa aliye hai kwa sasa (The Oldest Living person). Kane alitimiza miaka 117 tarehe 05 January mwaka huu.

Lakini Susana alitimiza miaka 131 March 23 mwaka huu. Rekodi ya kuzaliwa kwake ilipatikana katika kitabu cha kumbukumbu ya kanisa kilichoachwa na wamisionari wa kwanza wa Kijerumani waliokuja kueneza injili Kaskazini mwa Tanganyika na kujenga kituo cha kwanza cha misioni ya Kidia mwaka 1884.

Katika picha waliobeba maua ni wajukuu zake Susana ambao nao wana wajukuu na wengine wana vitukuu. Mtoto wa pili wa Susana alifariki mwaka 1999 akiwa na umri wa miaka 82 (angekua hai leo angekua na miaka 103). Mjukuu wake mkubwa ana mika 78.
Jambo la kumtukuza Mungu ni kwamba pamoja na umri wake mkubwa bado alikua na uwezo wa kusikia, kuona na kuzungumza. Pia akili yake ilikua timamu hata katika uzee wake aliweza kukumbuka na kusimulia baadhi ya matukio ya zamani. Alikua bibi mcheshi na mwenye tabasamu wakati wote.

Old Moshi imepoteza mtu muhimu sana katika historia. Dunia imempoteza mwanadamu mwenye umri mkubwa zaidi, na Kanisa limempoteza mmoja wa wakristo wa mwanzo kabisa nchini. BWANA alitoa na BWANA ametwaa jina lake lihimidiwe.
#RIPSusana
#LakuchaMkyeku
# LuanaRuwaKipfaKyapfo

Credit: G.Malisa

101428871_3039608992797439_4427129749004877824_o.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo haya yanapaswa kuanzia ndani ya nchi husika, na kuwakilishwa katika duru ya dunia kama taarifa rasmi iliyothibitishwa.
Bahati mbaya, nchini mwetu vitu hivi havipewi kipaumbele, nafikiri kwa kuwa havimnufaishi mwanasiasa, na pia hakuna rushwa kwa mfanyakazi.

Pumzika Bibi Mmary!

Sent from my LM-Q710(FGN) using JamiiForums mobile app
 
Kwenye ulimwengu wa roho namuona mtu aliyazaliwa 1700, kwenye ulimwengu wa kawaida akionekana mtoto wa miaka 10
 
Lanyeee nilikua sijui maana ya kidia !!!? Leo nimejua halafi kumbe kitimbirihu ilikua ya Anglican??? Shaa chamecha malisa
 
Wabongo banaa sijui tukoje.
Bibi alipokua hai hakuna aliehangaika kuufahamisha ulimwengu kua bibi yetu ndio binaadamu mwenye umri mrefu zaidi duniani kwa kipindi hicho, Ilya baada ya kufariki ndio tunaanza kusikia makelele kila kona.
Muacheni bibi apumzike kwa amani.
Hio rekodi haina yoyote kwake kwa sasa kama mlishindwa kumpogania kipindi akiwa hai.
Umenena kweli, ubarikiwe sana.
 
Back
Top Bottom