Sherehe ya mwisho ya bibi Susana Benjamin Mmary imefanyika nyumbani kwake huko Old Moshi Kidia, baada ya BWANA kumuita akiwa na umri wa miaka 131. Ni bahati mbaya kwamba taasisi zinazotunza rekodi za dunia haziangalii sana Afrika, lakini kabla hajafariki alipaswa kuwa ndiye mwanadamu mwenye umri mkubwa zaidi (the oldest living person).
Dunia inamtambua Kane Tanaka wa Japan kuwa mwanadamu mwenye umri mkubwa aliye hai kwa sasa (The Oldest Living person). Kane alitimiza miaka 117 tarehe 05 January mwaka huu.
Lakini Susana alitimiza miaka 131 March 23 mwaka huu. Rekodi ya kuzaliwa kwake ilipatikana katika kitabu cha kumbukumbu ya kanisa kilichoachwa na wamisionari wa kwanza wa Kijerumani waliokuja kueneza injili Kaskazini mwa Tanganyika na kujenga kituo cha kwanza cha misioni ya Kidia mwaka 1884.
Katika picha waliobeba maua ni wajukuu zake Susana ambao nao wana wajukuu na wengine wana vitukuu. Mtoto wa pili wa Susana alifariki mwaka 1999 akiwa na umri wa miaka 82 (angekua hai leo angekua na miaka 103). Mjukuu wake mkubwa ana mika 78.
Jambo la kumtukuza Mungu ni kwamba pamoja na umri wake mkubwa bado alikua na uwezo wa kusikia, kuona na kuzungumza. Pia akili yake ilikua timamu hata katika uzee wake aliweza kukumbuka na kusimulia baadhi ya matukio ya zamani. Alikua bibi mcheshi na mwenye tabasamu wakati wote.
Old Moshi imepoteza mtu muhimu sana katika historia. Dunia imempoteza mwanadamu mwenye umri mkubwa zaidi, na Kanisa limempoteza mmoja wa wakristo wa mwanzo kabisa nchini. BWANA alitoa na BWANA ametwaa jina lake lihimidiwe.
#RIPSusana
#LakuchaMkyeku
# LuanaRuwaKipfaKyapfo
Credit: G.Malisa
Sent using
Jamii Forums mobile app