mpendwa
mitale na midimu ahsante na hongera kwa maelezo yako nimekupata uzuri sana. lakini kadili ya maelezo yako binafsi ninamaswali kama mawili tu ivi:
1: kuna mahali umedai kuwa biblia toka mwanzo mpaka ufunuo ina kila kitu na kila fomula (kwa maana kwamba imejibu kila kitu ikiwemo na sayansi yenyewe kwa jinsi nilivokuelewa mimi). swali langu ni hil: ni nini lengo la biblia kwa mwanadamu, ni nini kusudi la biblia kwa mwanadamu, Mungu alikusudia biblia iwe na kazi gani kwa mwanadamu, au kwa nini biblia ???
mpendwa
mitale na midimu kama jibu la swali hilo hapo juu kuhusu lengo la biblia kwa mwanadamu ni tofauti kabisa na sayansi na haikukusudiwa kufundisha sayansi, unafikiri ni sahihi au ni haki tunapongangania kutafuta sayansi/ kujifunza sayansi toka kwenye kitabu ambacho hakikukusudiwa kwa kazi hiyo ?.
sikitai kwamba kuna sayansi mbaya na wanasayansi wapinga Mungu/wakana Mungu uwepo wa hao hauifanyi sayansi yote kuwa ni dhambi au kuwalaumu wapinga Mungu kwa kila jambo kwa Mgongo wa sayansi sidhani kama ni sahihi. ninachojua mimi ni kuwa sayansi ni pato la AKILI na MAARIFA tuliopewa na Mungu kama zawadi itusaidie kumpenda, kujua zaidi nk katika maisha yetu ya kila siku. ndio maana imeandikwa usimwache elimu aende zake na pia mpende bwana Mungu wako kwa AKILI zako zote. sasa sayansi ndio moja ya mapato ya izo AKILI au tunaweza kusema ndo AKILI zenyewe. tulipewa mikono na miguu kwa ajili ya kazi njema ya kumtumikia Mungu na jirani lakini kuna watu wanaitumia iyo mikono na miguu kwa kuvunja amri za Mungu kama kuiba, kuumiza, kupigana nk sasa hapo sidhani kama kosa ni mikono au miguu ndivo ilivo kwenye sayansi pia.
1: Bibilia imeweka msingi wa Kila kitu hiyo ndiyo point yangu kuu katika maelezo niliyokupa. Imeweka facts za Milele ambazo uvumbuzi wowote wa kisayansi unajengwa juu yake, na haziyumbishwi na wasanasayansi na mavumbuzi yao. Na kuyumba kwa wanasayansi hakuwezi kuziyumbisha zitadumu milele hata kama zikiaminiwa na watu wawili tu dunia nzima.
Miongoni mwa facts kuu hizo au naziita evalasting principles au formula
* Mungu ndiye Muumbaji. Hili Litabaki hivyo hata dunia ikatae.
*Mungu aliyemuumbaji, Anapaswa kuaminika kwa Kauli zake mwenyewe kuliko Kauli za Kiumbwaji.
*Wanasayansi wanajaribu kuchunguza kazi za Mungu za Uumbaji, Uchunguzi huo unaweza kupelekea kuvumbua ukweli wa kazi zake au Kupotosha ukweli huo. Katika Hili Kilichosemwa wazi kwenye Maandiko Matakatifu ndio Basis ya Ukweli huo.
*Sayansi inamipaka, ya ufahamu na uelewa Juu ya Kazi nzuri ya Mungu.
Bibilia haijatoa kila formula ya kisayansi na sijasema hayo maana haijazungumzia hata pai. Ila inatoa msingi au general formula za kumsaidia Mcha Mungu asivurugwe na kuchanganyikiwa na chochote kutoka kwa Mwanasayansi haramu au Halali.
####
Lengo la Bibilia ni nini?
'' Kwa Maana Jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanaye wa pekee, ili kila amuaminie asipotee bali awe na Uzima wa Milele'' Yohana 3:16
Kwangu mimi hili ndio lengo na dhumuni kuu la Maandiko Matakatifu. Ukombozi wa Mwanadamu. Ndio maana Yesu mwenyewe alisema Maandiko Yote yanamuelezea Yeye. Hata Hiyo Mwanzo ni Yeye ndiye Muhusika wa uumbaji.
Lakini pia Bibilia inasema '' Neno Lako ndiyo taa ya Miguu yangu na mwanga wa njia yangu''. Nje ya Bibilia utatembea gizani, na Kila kilichonje ya Bibilia ikiwa kitakizana na Ukweli mkuu wa Bibilia ni GIZA.
Bibilia inatufanya Tusewe watoto wachanga tena, Tukitupwa huku na kule na Kila upepo wa Elimu na mafunzo.
Pili
Sijasema Popote Kuwa Bibilia ikikusudia Kufundisha Sayansi, Bali Nimesema na nasema Bibilia ni Kitabu sahihi Kilichoweka kanuni/Formula na Misingi zinazoweza Kumsaidia Mwanadamu Asipotoshwe na Sayansi Potoshi na Awe Bora na Imani Yake kwa Mungu Ikue kwa Mavumbuzi na sayansi Sahihi.
Lakini Kusema hili Haimaanishi hakuna tips katika Bibilia ambazo ni scientifically correct, maana Bibilia imegusia vitu kama Rain formation Mungu akimthibitishia Ayubu Kuwa Yeye ndiye fundi wa hizo mifumo, Dunia duara kama mdau Kituko kazungumzia na tips kadhaa ila sio lengo kuu la Bibilia Maana Yote hayo hayatakuwa na Maana kama ukayajua na ukachepuka kwenye Lengo Kuu Wokovu wa Mwanadamu Kupita Kristo Yesu.
tatu
Hatujifunzi Sayansi Kutokea Kwenye Bibilia. Ila kama nilivyoonyesha Huko Juu Bibilia Ni nanga ambayo itamsaidia anayeiamini asiyumbishwe na tafiti potoshi au sahihi za Kisayansi. Mfano wa Tafiti Potoshi kwa Imani Yangu ni kudanganya watu Dunia imeumbwa miaka mamilioni Kisa Sayansi imesema Imegundua huku Bibilia Imeliweka wazi Kuwa ni Siku sita ambazo kwa Genealogy za watu wa Bibilia hatufikishi huko wanakozungumiza. Pia Basis na assumptions wa hizo observation ni kanusho la kazi njema ya Mungu aliyoweka msingi wa Kuikumbuka kupitia Sabato ambayo Yesu anasema waliwekewa wanadamu ili wakumbuke hilo zoezi ingawa mabillioni hawaoni umuhimu wa kufanya hilo.
nne
Pamoja na Kazi njema ya Ukombozi ambayo ndiyo msingi wa Bibilia, Imekusudiwa kuzuia upotoshaji wote wa kisayansi, kiphilosophia, Modernism, historia, elimu etc. Na Inatutaka Kuweke kando Kila fikra ijiinuayo KINYUME NA ELIMU YA MUNGU bila kujali inatoka kwa prof,scientist,padri,mchungaji hata Malaika.
SAYANSI NA AKILI ALIZOTUPA MUNGU.
Bibilia inasema '' Moyo (Human Mind) ni mdanganyifu na Unaugonjwa wa Kufisha, ni nani awezae Kuujua? Yeremia 17:9
Hii tu, inatosha kuendea tafiti za Kisayansi na Kisomi kitaaluma kwa utulivu huku tukiwa na taadhari kwa sababu zimefanyika kwa sababu zao na watu wa kawaida wenye ubinadamu uliofungamana na dhambi wanaweza kuja na hitimisho potoshi au sahihi, Danganyifu au Lenye muelekeo sahihi.
Mfano: Utasimama upande upi katika jambo ambalo hata wanasayansi wanapingana japo ni tokeo la akili hizo Mungu alizotupatia?
Utayaacha katika viwango Vya Nadharia tu au assumptions hata kama zinaungwa na dunia nzima haimaanishi ni Kweli. Sio mimi tu nasema haya hata galileo alisema ''
KATIKA SAYANSI MAMLAKA YA MAONI YA WATU ELFU MOJA, YANAWEZA YASIWE NA THAMANI SAWA NA FIKRA YA MTU MMOJA ''.
HITIMISHO.
Sipingi Sayansi, Ila siungi mkono Kila kitu katika Sayansi kama Fact. Kwanza hata wenyewe huwa wanaziita NI NADHARIA. Ila Kauli za Mungu sio NADHARIA. Kwa nini Sayansi unaona kama naijadili kwa Kutumia Bibilia japo Bibilia ijazungumzia UKOMBOZI. Sayansi ya Sasa Inafunua Pazia na Kuingia Kwenye mambo ya Imani na Bibilia Na Kuanza kuyatafsri na Kuyatolea Matamko. Mfano hata hili La Uumbaji na Umri wa Duñia. Ninaona ni Heshima Kubwa mno Kusimama na Kauli ya Mungu na Kuweka kando nadhalia zote katika hili. Hii hainifanyi nizichukie. Mimi nimesoma sayansi japo kwa kupapasa hadi elimu ya juu ya awali, hata nikiamua kutafuta PHD ya Geology nitasoma hayo yote ya mamilioni ya miaka kama nadharia ila fact ni Kauli ya Mungu kuwa Dunia Iliumbwa Siku sita Ya Saba akapumzika. Hakuwaandikia wasomi wa theolojia aliwaandikia wakina mama na wababa waliotoka utumwani, masikini wasio na elimu, akaagiza watoto wajulishwe katika hilo nimechagua kuelewa kama hao walioandikiwa na kuambiwa Wasiyaache maana hiyo ndiyo akili yao na ufahamu wao.
mkuu nimeandika maneno mengi ili kuchambua kwa kirefu kidogo maana inainekana hunielewi vizuri naamini nini na siamini nini.